Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Hawa watu kama si wamechanganyikiwa basi watakuwa na matatizo ya akili. Wakati Msanii Wema Isack Sepetu anajiengua CCM na kujiunga chama la Makamanda, CHADEMA ijapokuwa hajakabidhiwa kadi mpaka leo, alisema kuwa amezunguka nchi nzima kuinadi CCM na kumtafutia kura Rais Magufuli. Akalalamika kuwa kitendo cha yeye kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya si fair kwake kwani alitaraji CCM na Serikali watakumbuka mchango wake ndani ya CCM. Alitaraji mbeleko na kuonewa huruma.
Ameibuka huyu Nape Nnauye ambaye hata ushindi wake mwaka 2015 jimboni Mtama ulitokana na bao la mkono. Kama hiyo haitoshi Nape Nnauye akashinikiza Mwenyekiti wetu Suleiman Mathew kuhukumiwa kwa sababu tu Nape anataka kupita bila kupingwa mwaka 2020. CHADEMA bado tungali na hasira naye na bado tutaendelea kumchukia ijapokuwa kwa sasa nimeona dalili za kujipendekeza kwetu. Nape anaibuka na madai eti kura za Rais Magufuli kwenye uchaguzi wa 2015 zimetokana na juhudi zake na kwamba CCM itapata shida mwaka 2020 eti kwa vile tu katikiswa.
Haya ni maneno ya mfa maji. Siamini kama Nape Nnauye ni muhimu sana ndani ya CCM na kwamba bila yeye hakuna kura. Siamini pia kuwa Wema Sepetu ni muhimu sana ndani ya CCM na kwamba kuondoka kwake lazima chama KIKAE. Siamini na sitakuja kuamini katika personalities. Siasa za Personalities zipo ndani ya chama chetu, CHADEMA ambapo ndipo tunaamini kuwa bila mtu fulani chama hakiendi. Ndio maana mwaka 2004 tulifanya mabadiliko ya katiba ili kumruhusu Mbowe awe Mwenyekiti Milelel ila hayo hayapo kwa CCM. Kabla ya Nape wamepita wengi na kuondoka kwao hakujafanya chama chao kiyumbe.
Sasa sijui nani kamshauri mwenzake kati ya Wema na Nape. Maana inaonekana walikuwa wanajadiliana wakiwa wawili tu juu ya nini cha kusema kwa wananchi baada ya madhila yaliyowakuta. Wameshindwa kuchunga mdomo wao mwisho wa siku wamenaswa na ndoana.