Hivi kati ya wanawake wanaouza miili yao ili kupata fedha na wale wanaonunuliwa ili kupata vyeo,kuna tofauti?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Jamii yetu mara nyingi imekuwa ikikemea na kulaani tabia ya dada zetu kuuza miili yao kwa lengo la kujipatia fedha biashara ambayo hata serikali imekuwa ikiipiga vita na kuiilani.

Si hivyo tu,bali hata dini zetu haziruhusu kabisa jambo hili na bila shaka hii ni laana kabisa mbele za Mungu.

Kwa bahati mbaya,hivi sasa yameibuka madai au tuhuma za watu kunuliwa kwa maana ya kuhongwa ili waasi vyama vyao kwa minajili ya kupewa vyeo au kupata ulaji,n.k huko wanakokwenda/wanakohamia.

Nachojiuliza iwapo madai haya ni ya kweli,wenzetu hawa wanaonunuliwa kwa ahadi za aina hii na wanawake wanaouza miili yao ili kupata fedha,watu hawa wana tofauti gani linapokuja swala la utu na thamani ya utu wa mtu kulinganisha na fedha?

Hawa watu na wateja wao, hawadhalilisha utu wa mwanadamu?

Kwanini na wao wasisomewe Albadili?
 
Kuna watu wanasema, kila binadamu ni "changudoa" wa aina fulani, tofauti ni kiungo gani kinatumika kutoa huduma.
 
Back
Top Bottom