Hivi kati ya Roman empire na Marekani ni nani haswa anayeitawala dunia?

UFUNUO 13. YOTE SOMA MZEE USIWE MFIFU.

Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Mtu akiwa na sikio na asikie.
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
 
ROMAN EMPIRE NDO BABA WA DUNIA YEYE NDIO KACHORA RAMANI YA DUNIA .

NA ANAITWALA DUNIA KUPITIA ROMAN KATOLIKI AMBAO NDIO SUPER POWER WA DUNIA YA LEO
NDIO MAANA KILA KINACHOFANYIKA DUNIANI KINA MKONO WA ROMAN EMPIRE.

HATA HUU MWAKA MPYA TUNAUSHEREKEA LEO HII TUNAUSHEREKEA KWA SABABU TUNAFATA CALENDER YA ROMAN KATOLIKI
Hayo majina mnayojipa muwe mnaangalia sasa jibu zuri kama hili umelitoa ila shaka inakuja mchangiaji ni msela wa masenze nashindwa kuamini fulani hi msela na haya mambo wap na wap
 
Kuna ukweli juu ya hili la Roman Empire ndio hao hao roman Catholic tangu zamani kumbuka story ya Mfalme Henry wa uingereza alitaka kuoa mke wa pili akaomba kibali kwa papa akamtosa akaruhusu bible itafsiriwe kwa lugha tofauti na kilatini kilichompata alikiona

Huo ni mfano mmoja ila Roman Empire ipo imevaa koti la kidini na ndio wanaopanga watawala duniani
Kilimpata kitu gani mkuu? Naomba utujuze tafadhali
 
KWA KIFUPI TUU ROMAN EMPIRE ILIANZA MIAKA YA ZAMANI SANA KIPINDI CHA 30 B.C YAANI BEFORE CHRIST .

KWA MIAKA YA ZAMANI ROMAN EMPIRE ILITAWALA BARA LA ULAYA PEKEE LAKINI BAADA YA MIAKA KWENDA ROMAN EMPIRE KATIKA KUJITANUA NGUVU ZAKE ILIBIDI WAANZISHE DINI ILI WAENDELEZE NGUVU ZAO KUITAWALA DUNIA HIVYO ILIBIDI WAIVUNJE ROMAN EMPIRE NA KUANZISHA ROMAN CATHOLIC KWAIYO ROMAN KATOLIKI KAMA DINI LAKINI IMEVAA KOTI LA ROMAN EMPIRE ILI WAENDELEE KUITAWALA DUNIA.

BAADA YA KUANZISHA ROMAN KATOLIKI HAWAKUISHIA HAPO PIA WALIANZISHA MFUMO WA SERIKALI NDANI YA KATOLIKI KUWA KITU KIMOJA LAKINI SERIKALI INAKUWA IPO CHINI YA KANISA KATOLIKI NA HAPO NDIPO WALIPOFANIKIWA KUITAWALA DUNIA.

LAKINI PIA WAKATOLIKI WAMETENGENEZA SYSTEM ZA KIJASUSI AMBAYO KIONGOZI WA NCHI YOYOTE DUNIANI NI LAZIMA AFUATE MFUMO WA KIKATOLIKI NA UKATOLIKI UNAVYOTAKA NA ENDAPO KIONGOZI YOYOTE YULE ATAJARIBU KUUPINGA ULE MFUMO BASI ATAUWAWA KUPITIA KITENGO CHAO CHA UJASUSI CHA JERSUIT HIVYO HAWA JAMAA WANA POWER OVER GOVERMENTS DUNIA NZIMA
Ina maana ata yule wa uchina XIN JIN PING anaweza kuuawa asipofata mfumo wa kikatoliki , haufati vip mbona awajamuua ?
 
hamna lolote mbona DRC kafeli na Fayulu wake pia viongozi wakubwa wana connection na Freemason na sio Roma may be Roma nayo iwe ni Masonic
 
Mkuu unajiaibisha tu

Roman empire ilishakwisha siku nyingi

Dini ya Roman catholic haina ushawishi wowote juu ya serikali za dunia baada ya ukristo kugawanyika between Roman and protestant

Uprotestant hasa uanglikan na u Lutheran ndo uliofuta ushawishi wa catholic huko ulaya na baadae duniani kote

Mfano Tanzania Kuna watu wanaamini Marais wanatokea katholik kwasabab kanisa Lina ushawahish kitu ambacho sio kweli ila tu kwasabab ya Bahati ya mtu na ushawishi wa nyerere

Tatizo sisi wabongo wazembe wa kusoma vitabu

Kanisa katholik Lina nguvu kwa wa uamin wake ila sio serikali za dunia
Vipi kuhusu Congo? Mvutano wa Joseph kabila na RC kuhusu nafasi ya uraisi.
 
MBONA BIBLIA IMEELEZA VIZURI...



Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza,naye alikuwa na pembe kumi.”

Danieli 7:8 “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama,pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.”

Je “pembe ndogo” iliyozuka na kuzing’oa “pembe tatu” katika zile “pembe kumi” za mwanzo ni nini? Danieli akiwa katika maono, katika sura ya 7, aliona wanyama wanne ambao walikuwa; wa kwanza kama simba, wa pili kama dubu, wa tatu kama chui, na wa nne alikuwa tofauti na wale wanyama watatu wengine. Malaika alipomtafsiria Danieli kuhusu wanyama hao, katika Danieli 7:17 alisema, “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Hivyo wanyama hao wanne ni falme nne ambazo zingetawala juu ya dunia. Ifuatayo ni orodha ya falme hizo nne zinazowakilisha wanyama wanne aliowaona Danieli, kama ukitaka ushahidi wa Maandiko na historia kuhusu wanyama ambao ni falme hizi nne; tafadhari bonyeza hapa.

MnyamaUfalme1Babeli2Umedi/Uajemi3Ugiriki4Roma

Mnyama wa nne ambaye ni ufalme wa Roma/Rumi, Danieli 7:7 inasema “alikuwa na pembe kumi”. Je “pembe kumi” za mnyama huyo zinamaanisha nini? Malaika alipomfahamisha Danieli kuhusu hizo pembe kumi alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi;…” Danieli 7:24. Hivyo, pembe zake kumi zinawakilisha falme au mataifa kumi ambayo yangetawala ndani ya ufalme huo mmoja; baada ya ufalme wa Rumi kuanguka mwaka 476BK uligawanyika katika mataifa kumi ambayo yanawakilisha pembe kumi za mnyama huyo wa nne. Ifuatayo ni orodha ya mataifa kumi yanayowakirisha pembe kumi za Rumi.

1. Saxon, kwa sasa ni
taifa la Uingereza.2. Frank, kwa sasa ni
taifa la Ufaransa.3. Alamanni, kwa sasa ni taifa la Ujerumani.4. Visigoth, kwa sasa ni taifa la Uhispania.5. Suevi, kwa sasa ni taifa la Ureno.6. Lombard, kwa sasa ni taifa la Italia.7. Burgundia, kwa sasa ni taifa la Uswidi.8. Heruli, liling’olewa na pembe ndogo 493 B.K.9. Vandal, liling’olewa na pembe ndogo 534 B.K.10. Ostrogoth, liling’olewa na pembe
ndogo 538 B.K.

Baada ya kutokea pembe hizi kumi katika ufalme wa Rumi, Danieli 7:7 inatuambia kuwa katikati ya pembe hizo kumi, ingetokea “pembe ndogo” ambayo ingezing’oa pembe tatu katika zile kumi za mwanzo, na Je pembe hii ndogo ni nini? Malaika alipomfafanulia Danieli kuhusu hiyo pembe ndogo alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine [ambaye ni pembe ndogo] ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Danieli 7:24.

Je ni taifa au ufalme gani mdogo ulioinuka baada ya ufalme wa Rumi kugawanyika katika mataifa kumi yanayowakilisha pembe kumi? Kwa hakika taifa au ufalme mdogo ulioinuka wakati huo katika dola la Rumi ni Upapa wa Vatikani, Upapa ndio unawakilisha pembe ndogo ya Danieli 7:7 na unabii unasema, pembe hii ndogo ingezing’oa pembe tatu katika pembe zile kumi zinazowakilisha mataifa kumi. Je Upapa uliyaondoa mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo?

Baada ya kupitishwa rasmi fundisho la utatu katika baraza la pili huko Konsitantinapoli mwaka 381bk, baraza lilitoa amri kuwaangamiza watu wote watakaopinga imani ya utatu, hii ilisababisha kuangamizwa kwa mataifa matatu ya Waario (Arians); watu ambao hawakuamini imani ya utatu. Mataifa ya Waario yaling’olewa na kanisa Katoliki; Heruli liliangushwa mwaka 493 B.K., Vandal, liliangushwa 534 B.K., na Ostrogoth, liliangushwa 538 B.K. Upapa ulipata mamlaka yote ya kiserikali mwaka 538bk ambapo taifa la mwisho liliangushwa. Hivyo fundisho la utatu lilikuwa ni sababu kubwa iliyouwezesha Upapa kupata mamlaka kuu ya kiserikali na kuwaangamiza Wakristo wasio na hatia, leo Mkristo yeyote mwaminifu hapaswi kuamini imani ya utatu iliyosababisha kuinuka kwa Upapa kama mpinga-Kristo. Na Je unajua kwamba hata imani ya utatu inampinga Kristo kwa sababu inafundisha kwamba Kristo hayupo Yeye kama Yeye binafsi, bali ni Mungu yuleyule mmoja? Na kama hujui, basi jihadhari usikutwe ukiwa upande wa mpinga-Kristo kwa kushikia mafundisho yake.

Hivyo Upapa ni pembe ndogo, nao ulizing’oa pembe tatu, ambazo ni mataifa matatu ya Roma. Danieli 7:25 kuhusu pembe ndogo inasema, “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”

Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu; – Maneno haya yaliyo kinyume na Aliye juu, ni makufuru ambayo yanafanywa na kuongelewa katika Upapa; Ufunuo 17:3 inasema, “…nikaona mwanamke ameti juu ya mnyama…mwenye kujaa majina ya makufuru…”, Ufunuo 13:1 “…nikaona mnyama…mwenye…vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”, na Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena makuu, ya makufuru…” Kukufuru katika Biblia inaelezewa kama hali ya mtu kujifanya yeye mwenyewe kama Mungu (Yohana 10:33), au mtu kujidai kwamba ana uwezo wa kusamehe dhambi (Marko 2:7); katika mfumo wa Upapa, papa na makuhani hujidai kuwa wao ni miungu duniani, tena wanauwezo wa kusamehe dhambi bofya hapa kuthibitisha.

naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; – Hii inamaanisha kwamba, Upapa ungewatesa na kuwaua Wakiristo wa kweli; bofya hapa kuthibitisha.

naye ataazimu kubadili majira na sheria; – Hii inamaanisha kwamba Upapa ungebadirisha majira na sheria za Mungu, sheria za Mungu zilizobadilishwa na Upapa ni sheria ya Sabato na sheria inayokataza kuchonga sanamu yoyote ile; pia majira yalibadilishwa na Papa Gregory XIII, ambaye mwaka 1582 alianzisha kalenda mpya ambayo siku inaanzia usiku saa 6 badala ya jioni saa moja; bofya hapa kuthibitisha.

nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati; Watakatifu wangetiwa mikononi mwa Upapa kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati; Ufunuo 13:5 inaunataja muda huo kama miezi 42, wakati Ufunuo 12:6 inautaja muda huo kama siku 1260. Ukiangalia kwa makini hapa utaona kuwa, wakati = mwaka 1, nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka, ambayo jumla ni miaka 3.5 (1 2-0.5=3.5), au miezi 42 au siku 1260 za kiunabi ambazo Upapa ungewatesa Wakristo; bofya hapa kuthibitisha.

Tunaruka kutoka sura ya 7 ya kitabu cha Danieli hadi sura ya 8 ambapo tunaona Danieli alibarikiwa kupata maono mengine yanayohusu pembe ndogo.

Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”

Je huyu kondoo mwenye pembe mbili ni nani? Malaika alipomfafanulia Danieli kuhusu kondoo huyu alisema, “Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.” Danieli 8:20. Hivyo kondoo huyo mwenye pembe mbili ni ufalme mmoja unaotawaliwa na wafalme wawili; mfalme wa Umedi na mwingine wa Uajemi, tena Danieli aliona kwamba “pembe moja ilikuwa ndefu kuliko nyingine”, hii inawakilisha kwamba mfalme mmoja angekuwa na mamlaka kuu kuliko mfalme mwingine; na hii ni kweli kwa sababu pembe ya Uajemi ilikuwa na nguvu kuliko Umedi.

Danieli 8:4 “Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.”

Kusukuma upande wa magharibi, kusikazini, na kusini; hapa inamaanisha kwamba ufalme wa Umedi/Uajemi katika enzi zake ungeshinda vita maeneo yote, na wala usingekuwepo ufalme wala mnyama mwingine wa kushindana nao; kwani “kusukuma pande nne za dunia” inaweza kufananishwa na “upepo kuvuma kuelekea pande nne za dunia” ishara ambayo inawakirisha “vita” (Yeremia 25:32). Katika Ufunuo 7:1-3 tunaona malaika wameamuriwa kuzishikilia “pepo” nne; yaani kuzuia vita hata Mungu atakapomaliza kuwatia mhuri watu wake. Hivyo upepo katika unabii = vita, tufani au dhoruba. Na ufalme wa Umedi/Uajemi ungeshinda vita wala usingekuwdpo ufalme mwingine ambao ungeweza kupokonya mikononi mwake.

Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”

Je beberu huyu mwenye pembe mashuhuri ni nani? Malaika alipomfahamisha Danieli kuhusu beberu huyu alisema, “Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.” Danieli 8:21. Hivyo yule beberu ni ufalme wa Uyunani/Ugiriki ambao ulifuata baada ya ufalme wa Umedi na Uajemi kuanguka, na ile pembe yake mashuhuri ni mfalme wa kwanza kutawala katika ufalme huo, ambaye alikuwa ni Aleksanda Mkuu.

Danieli 8:6 “Naye [beberu] akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake.”

Hapa inamaanisha ufalme wa Ugiriki ukaenda kufanya vita kwa ghadhabu dhidi ya ufalme wa Umedi na Uajemi.

Danieli 8:7 “Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake.”

Ufalme wa Ugiriki ungezivunja pembe mbili za kondoo ambazo ni wafalme wa Umedi na Uajemi, na wala asingekuwepo mnyama mwingine yeyote wa kuwasaidia, bali Ugiriki ilishinda na kuuchukua ufalme ikatawala juu ya dunia.

Danieli 8:8 “Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.”

Je pembe nne zilizozuka baada ya ile pembe moja kuvunjika zinawakilisha nini? Malaika alipomfafanulia Danieli kuhusu pembe hizo alisema, “Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.” Danieli 8:22. Hivyo pembe iliyovunjika inawakilisha kuisha kwa utawala wa Aleksanda mkuu, na zile pembe nne zilizozuka baada ya utawala wa mfalme Aleksanda kuisha, zinawakilisha falme nne ambazo ziligawanyika ndani ya ufalme huohuo mmoja. Ingawa ufalme wa Ugiriki uligawanyika na kutawaliwa na wafalme wanne, lakini haukuwa na nguvu kama zilizokuwepo wakati wa mfalme Aleksanda.

Danieli 8:9 “Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.”

Je pembe hii ndogo “ambayo inatoka katika moja ya pembe hizo” ni nini? Baada ya ufalme wa Ugiriki kugawanyika katika falme nne zinazowakilisha pembe nne, ulipungua nguvu na baadaye ulihusuriwa na dola la Rumi na ufalme ukarudi katika mikono ya mnyama Rumi, hivyo ni kitu kisichowezekana kwa pembe ndogo kutokea katika ufalme wa Ugiriki; kwa maana, Ugiriki ilianguka wakati wa wafalme wake wanne wanaowakilisha pembe zake nne, na hivyo pembe ndogo ambayo ingeinuka baada ya zile pembe nne, kwa hakika pembe hiyo ingeinuka katika ufalme ambao ulifuata kutawala baada ya Ugiriki kuanguka, na ufalme huo uliofuata baada ya Ugiriki ni Rumi, hivyo pembe ndogo ingezuka kutoka katika ufalme wa Rumi na sio Ugiriki; kwa maana Ugiriki ilianguka wakati bado ikiwa na zile pembe nne peke yake bila pembe nyingine yoyote. Malaika alimfafanulia Danieli kuhusu unabii huu, alisema, “Na wakati wa mwisho wa ufalme wao [wale wafalme wanne wa Ugiriki], wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.” Danieli 8:23

Zingatia katika fungu la 22 malaika alisema kuwa zile pembe nne ni falme nne za taifa moja la Ugiriki, harafu katika fungu la 23 akasema kuwa wakati wa mwisho wa ufalme wa zile pembe nne utakapofika ndipo “mfalme ajuaye mafumbo” ambaye ndiye pembe ndogo atainuka. Tunachopaswa kuzingatia hapa ni maneno “ufalme wao”, hii inamaanisha kwamba ufalme wote wa Ugiriki pamoja na falme zake au pembe zake nne, harafu zingatia maneno haya pia “utakapofika mwisho”; hii inamaanisha kwamba ufalme wote wa Ugiriki pamoja na falme zake nne utakapokufa kabisa, ndipo mfalme ajuaye mafumbo ambaye ni pembe ndogo anatokea. Hapa swali la kujiuliza ni kwamba, Je inawezekanaje pembe ndogo atokee katika ufalme wa Ugiriki wakati ufalme wa ugiriki umefika mwisho na umekufa? Kwa hakika jibu ni hapana! Hivyo, Je pembe ndogo anatokea wapi sasa? Lazima pembe ndogo anatokea katika ufalme ambao ulitawala baada ya Ugiriki kufika mwisho, na ufalme huo ni dola la Rumi. Hivyo uhakika na hitimisho ni kwamba pembe ndogo inatoke katika mnyama Roma.

Tukiwa na ukweli huu kwamba pembe ndogo inatoka katika mnyama Roma, hebu tuangalie Je pembe hiyo ndogo ni nani katika dola la Roma? Tunapaswa kuelewa kwamba dola la Roma tangu lianze kutawala mwaka 168 K.K., lilitawaliwa na mfalme mmoja tu aliyetawala juu ya ufalme wote, ambaye anawakilisha pembe moja, na pembe hiyo haiwezi kuchukuliwa kama ni pembe ndogo; kwa maana pembe ndogo inamaanisha “kiufalme au kitaifa ambacho ni kidogo”, lakini Rumi lilikuwa ni dola kubwa lililotawala karibu juu ya dunia yote. Baadaye dola lilipoanguka liligawanyika kuwa pembe kumi ambazo ni falme au mataifa kumi ya dola hilo moja, taifa moja katika yale kumi haliwezi kuchukuliwa pia kama pembe ndogo, bali pembe ndogo inawakilisha Upapa unaotawala juu ya kitaifa kidogo cha Vatikani, ambacho kimo ndani ya pembe moja ya Italia ambayo ni moja ya zile pembe kumi za Roma. Ukilinganisha na ushahidi tulioupata katika Danieli sura ya 7, kwa hakika pembe ndogo inawakilisha ni kimji kidogo ambacho kimo ndani ya dola la Roma, na kimji hicho ni Uatikani, ambacho kinatawaliwa na serikali ya Upapa. Danieli 7:8 inatuambia kuwa Kimji hiki kidogo au kipembe hii kidogo kiko tofauti na zile pembe kumi za mnyama Roma kwa sababu chenyewe kina mamlaka ya kidini na kisiasa (kanisa na serikali) kwa wakati mmoja.

Tumegundua kuwa pembe ndogo ambayo ingezuka ingezuka katika mnyama Roma, na pembe hiyo ni serikali ya Upapa wa Vatikani, hivyo ngoja tuangalie sifa na mambo ambayo pembe hii ndogo ingeyafanya baada tu ya kuzuka kwake.

Danieli 8:23 “Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.”

Ufalme wa serikali ya Upapa, ni ufalme unaojua mafumbo na mitego, wanatumia mafumbo ili kudanganya watu wadhani kwamba Upapa ni mitume wa Kristo, lakini kiukweli ni mfumo wa shetani mwenyewe ulioandaliwa kwa ajili ya kumpinga Kristo.

Danieli 8:10 “Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.”

Kwa sababu pembe inawakisha ufalme au taifa na wala sio pembe halisi, hivyo kukua kwake mpaka mbinguni pia sio kwa uhalisi, bali kukua mpaka mbinguni hapa inamaanisha kukua na kutukuka kwa taifa hilo dogo la Vatikani na kutambulika mpaka miisho ya dunia (Danieli 4:22). Na nyota na jeshi la mbinguni linaloangushwa na kukanyagwa havipaswi kuchuliwa kwa uhalisi kwa maana hata pembe yenyewe inayoliangusha jeshi hilo siyo pembe halisi bali ni taifa, hivyo kuangusha nyota na jeshi la mbinguni na kulikanyaga hapa inamaanisha ni kuwatesa na kuwauwa watakatifu wa Mungu. Kwa hakika malaika alifafanua vizuri maelezo haya aliposema, “Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.” Danieli 8:24 Hivyo kukua hadi kulifikila jeshi la mbinguni ni kama tu kuwa na “nguvu nyingi mno”.

Danieli 8:11 “Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.”

Danieli 8:25 “Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.”

Kwamba Upapa ungefanikisha hira za uongo na madanganyo matupu, na kwa sababu hiyo ungewaangamiza watu katika hali yao ya salama – kuangamiza katika hali ya salama; hapa inamaanisha kwa sababu ya madanganyo yanayofanywa na mfumo wa Upapa, ambayo wengi hawayaelewi, kwa hiyo wengi wanakuwa katika hali ya kupotea huku wakidhani wataokolewa. Mfano mfano mfupi ni ubatizo, ubatizo unaofanyika katika Upapa ni ubatizo wa kumdanganya mtu, na hivyo kumwangamiza kwa njia ya salama. Lakini mamlaka hii ya Upapa Yesu ataivunja bila kazi ya mikono.

Danieli 8:12 “Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.”

Kuiangusha kweli hata chini; hiki ndicho Upapa umekuwa ukifanya kwa miaka mingi sasa, mafundisho yote ya kanisa la Upapa ni maneno ya mwanadamu na mafundisho ya mashetani, ambayo Bwana Yesu anasema ni “ibaada ya bure”, Neno la Mungu limekanyagwa na Upapa, na watu wengi wamefuata njia ya mfumo huu wa mpinga Kristo, kweli ya neno la Mungu imeangushwa, na kuibiwa kutoka kwenye akili za watu. Lakini Bwana anatuambia kwamba atakuja na kuiharibu mamlaka ya Upapa hata milele isiwepo tena, na ufalme atawapa watakatifu wake watawale milele yote.

Danieli 7:26 “Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.”

Danieli 7:27 “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.”

Danieli 7:28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.”
Ubarikiwe sana
 
BIBLIA PIA IMEELEZA VIZURI KUIBUKA KWA U .S .A NA KUMSAIDIA KWAKE ROMAN CATHOLIC

Ndio maana nawashangaaga waislamu wanaposhindwa kuiamini biblia wanabaki wanaikashfu tu,

Marekani Katika Unabii

Biblia yasema hivi;”-Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.

Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. [Ufu13:11-18].

Mnyama huyu wa pili anapanda kutoka nchi kavu, kinyume na yule mnyama wa kwanza, apandaye kutoka Baharini. Kiunabii mnyama anamaanisha taifa ama ufalme; Soma [Dan7:17]. Bahari humaanisha watu wengi, ama makutano ama mataifa, SOMAUfu17:15. Kama bahari humaanisha watu wengi, nchi kavu humaanisha watu wachache. Mnyama wa kwanza yaani Ufalme wa Rumi, na baadaye Utawala wa upapa wa kirumi,Uliibikamiongoni mwa mataifa mengi mwaka 168BC mpaka 476AD, Na Baadaye upapa mwaka 538AD-1798AD. Mnyama huyu wa pili

1. Anawakilisha ufalme uliotokea baada ya mnyama [ufalme] wa kwanza Kupata jeraha la mauti na baadaye kupona. Upapa ulikomeshwa mwaka 1798, ambapo kamanda wa ufaransa katika french revolution aitwaye, Berthier Alimkamata papa na kumfunga gerezani. Baadaye upapa ukarudishwa tena.

2. Pia anawakilisha ufalme uliotokea sehemu yenye watu wachache.

3. Ufalme huu pia unaibuka kama taifa la kikristo [Mwanakondoo anamwakilisha kristo],na pembe zake mbili huwakilisha Kanuni kuu mbili ambazo Taifa hilo linatawala kwazo.

Hapa taifa la marekani linatabiriwa.Taifa la marekani lilitokea mwaka 1776AD-1789, kama taifa la kikristo la waprotestanti. Upapa ulipata jeraha la mauti mwaka1798AD, Nyakati ambazo taifa la marekani lilikuwa taifa jipya linalokua. Pia liliibuka katika bara lililokuwa na watu wachache[RED INDIANS]. Marekani ilitokea kama taifa lenye kuongozwa na kanuni kuu mbili, Serikali pembeni, na dini pembeni. Havichangamani pamoja na dini haiingiliani na serikali. Unabii unatabiri kuwa Siku za mwisho, Marekani utakuwa sauti ya JOKA. Unabii pia unatuambia kuwa marekani, itaungana na Upapa [yule mnyama wa kwanza]. Marekani itakuja kutumia uwezo wake kuwatesa watu wa Mungu kama upapa wa kale ulivyofanya, Pia utawaamuru watu wote wakaao juu ya nchi, wausujudie Upapa.
Asomae na aelewe. Mungu akubariki sana
 
Huo ni mfano mmoja ila Roman Empire ipo imevaa koti la kidini na ndio wanaopanga watawala duniani
Hizi ni Imagination tu, na story ambazo sizikatai moja kwa moja maana zinaweza kuwa kweli ikiwa kutakuwepo na ushahidi, lakini hakuna ushahidi wa kutosha juu ya unalolisema;
Je wanapanga duniani au kwenye baadhi ya nchi? Ndio kusema Roman Empire wanapanga mpaka hawa Presidents wetu wa huku Africa?
Nadhani pia usomaji wa Vitabu watanzania wengi hatuna, Roman Empire ilishakufa longtime, ivi sasa story zinachanganywa na Roman Catholic; ndio mnaita empire.

Ila sichangai, maana hata huku Africa utasikia mtu eti anasema yeye ni Roman Catholic akimaanisha ndio dini yake; Lakini kimsingi Yeye ni mkatoliki, Roman Catholic ni kanisa katoliki la Roma.
 
Back
Top Bottom