Hivi kati ya Roman empire na Marekani ni nani haswa anayeitawala dunia?

Katika pitapita zangu nilikutana na mjadala kuhusu maswala kuhusu Marekani na utawala wa Roman empire ndani ya kanisa katoliki.

Wapo wengine wanafikia hatua wanasema kiongozi yoyote au rais yoyote ambae anaenda kinyume na itikadi za Roman anaweza ondolewa au kuuawa.

Wapo wanaosema Roman katoliki chini ya Roman ndio ana nguvu ya kutawala dunia na wengine wanasema Marekani ndio baba wa dunia

Hebu wana JF naombeni mawazo yenu kuhusu utawala wa Roman empire katika hii dunia na Marekani.
Utawala wa Roman empire hautofautiani sana na Barabara ya Nyerere road ila tuendelee kujadili hoja
 
sababu tumepitia mengi n tunaendelea pitia mengi!!, kifupi sisi ndio mti nyie wengine ni vijitawi tu tukiamua kitu mtayumba!..
ayumbe nani wewe..endeleeni kuchangishana sadaka za lazma..maana hali mbaya,kondoo hawaji machungani
 
Kuna ukweli juu ya hili la Roman Empire ndio hao hao roman Catholic tangu zamani kumbuka story ya Mfalme Henry wa uingereza alitaka kuoa mke wa pili akaomba kibali kwa papa akamtosa akaruhusu bible itafsiriwe kwa lugha tofauti na kilatini kilichompata alikiona

Huo ni mfano mmoja ila Roman Empire ipo imevaa koti la kidini na ndio wanaopanga watawala duniani
Ndio maana huwa siamini kama kuna mtu mweusi atakuja kuwa papa
 
KWA KIFUPI TUU ROMAN EMPIRE ILIANZA MIAKA YA ZAMANI SANA KIPINDI CHA 30 B.C YAANI BEFORE CHRIST .

KWA MIAKA YA ZAMANI ROMAN EMPIRE ILITAWALA BARA LA ULAYA PEKEE LAKINI BAADA YA MIAKA KWENDA ROMAN EMPIRE KATIKA KUJITANUA NGUVU ZAKE ILIBIDI WAANZISHE DINI ILI WAENDELEZE NGUVU ZAO KUITAWALA DUNIA HIVYO ILIBIDI WAIVUNJE ROMAN EMPIRE NA KUANZISHA ROMAN CATHOLIC KWAIYO ROMAN KATOLIKI KAMA DINI LAKINI IMEVAA KOTI LA ROMAN EMPIRE ILI WAENDELEE KUITAWALA DUNIA.

BAADA YA KUANZISHA ROMAN KATOLIKI HAWAKUISHIA HAPO PIA WALIANZISHA MFUMO WA SERIKALI NDANI YA KATOLIKI KUWA KITU KIMOJA LAKINI SERIKALI INAKUWA IPO CHINI YA KANISA KATOLIKI NA HAPO NDIPO WALIPOFANIKIWA KUITAWALA DUNIA.

LAKINI PIA WAKATOLIKI WAMETENGENEZA SYSTEM ZA KIJASUSI AMBAYO KIONGOZI WA NCHI YOYOTE DUNIANI NI LAZIMA AFUATE MFUMO WA KIKATOLIKI NA UKATOLIKI UNAVYOTAKA NA ENDAPO KIONGOZI YOYOTE YULE ATAJARIBU KUUPINGA ULE MFUMO BASI ATAUWAWA KUPITIA KITENGO CHAO CHA UJASUSI CHA JERSUIT HIVYO HAWA JAMAA WANA POWER OVER GOVERMENTS DUNIA NZIMA
Mkuu unajiaibisha tu

Roman empire ilishakwisha siku nyingi

Dini ya Roman catholic haina ushawishi wowote juu ya serikali za dunia baada ya ukristo kugawanyika between Roman and protestant

Uprotestant hasa uanglikan na u Lutheran ndo uliofuta ushawishi wa catholic huko ulaya na baadae duniani kote

Mfano Tanzania Kuna watu wanaamini Marais wanatokea katholik kwasabab kanisa Lina ushawahish kitu ambacho sio kweli ila tu kwasabab ya Bahati ya mtu na ushawishi wa nyerere

Tatizo sisi wabongo wazembe wa kusoma vitabu

Kanisa katholik Lina nguvu kwa wa uamin wake ila sio serikali za dunia
 
MTOA HOJA MAJIBU YAKO HAPA. Daniel 7. soma yote , halafu soma Ufunuo 13. Ufalme wa Rumi unapokea mamlaka kutoka kwa Joka (Ibilisi) na Marekani wanapokea Mamlaka kutoka kwa Rumi (Sasa ni rumi ya Kidini). Itaenda hivyo hadi mwisho wa dunia, hakuna cha china, korea, sijui Urusi hivyo ni viini macho tu. ITS WRITTEN BEFORE. HERI ASOMAE

Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.

Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.

Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.
Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Basi, mimi Danieli, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha.
Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo.
Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.
Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.
Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;
hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.
Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.
Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom