Hivi kati ya Roman empire na Marekani ni nani haswa anayeitawala dunia?

Gerasmus

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Messages
401
Points
500

Gerasmus

JF-Expert Member
Joined May 23, 2016
401 500
MKUU MAREKANI HATA MWENYEWE NI MTOTO MDOGO MBELE YA MFUMO WA KIKATOLIKI

NA MAREKANI MWENYEWE IWE ISIWE KIONGOZI YOYOTE YULE ATAKAEITAWALA MAREKANI NI LAZIMA ATAFUATA MISINGI YA ROMAN EMPIRE NA KATOLIKI.

NAKUMBUKA KUNA RAISI MMOJA WA MAREKANI KWA JINA LA KENNEDY ALIUWAWA NA MAJASUSI WA KIKATOLIKI NA INASEMEKANA KUNA MAMBO ALIKUWA HAKUBALIANI NA WAKATOLIKI WAKAJA KUMUUA .

HIVYO ROMAN NI KITU KINGINE KABISA
Unaogopa sana ukatoliki wewe, umedanganywa ili ukadanganye kwa niaba ya waliokudanganya.,acheni kutiana hofu za bure.
 

Gerasmus

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Messages
401
Points
500

Gerasmus

JF-Expert Member
Joined May 23, 2016
401 500
Ukisoma kwenye kitabu cha ufunuo,anzia 12-18.

Halafu badilisha wale wanyama kua nchi za sasa.

Utaona ametajwa joka jekundu lililotaka kummeza mtoto alikua anasubili azaliwe kutoka kwa mama mjamzito,

Baada ya kushindwa kummeza,kwa hasila,likaenda kukaa ukingoni mwa bahari.huyo ndio ROMA EMPAYA.

kisha akatokea mnyama anaefanana na dubu,kutoka ufukweni,mwenye pembe kumi,mnyama huyu ufunuo umemtaja kama ni mnyama mwenye makufuru,matukano,hata kuzihaki mungu,kupigana na watakatufu na kuwashinda na hata ataesababisha gadhabu ya mungu,lakini mnyama huyo amepewa kiburi na lile joka jekundu. HUYO NI MMAREKANI, tunashuhudia mambo anayofanya,hadi ushoga ameamua kuutangaza ,

Kisha akatokea mnyama mwingine huyu ametajwa kama mpotoshaji,maana atasema maneni ya kustaajabisha katika ulimwe.
huyu ni israel
Malizia "By Helen G White"
 

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Messages
12,853
Points
2,000

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2014
12,853 2,000
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu nani ni mtawala wa sasa wa huu ulimwengu kati ya MAREKANI NA ROMAN CATHOLIC kwa mwamvuli wa WHITE POPE NA BLACK POPE,

Nabii Yohana alioneshwa yote haya...

Huwa nawasikitikia sana wale wasemao biblia imebadilishwa, mara biblia sio kitabu cha Mungu, Rafiki, nakupa siri leo BIBLIA nikitabu chenye historia hadi ya mwisho wa huu ULIMWENGU...

Tuanze, NABII YOHANA akiwa katika kisiwa cha Patmo, alioneshwa haya...

Ufunuo 13:11-12 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.”

Je mnyama huyu wa pili anaeifanya dunia na wote waikaao wamsujudie yule mnyama wa kwanza aliyepata jeraha la mauti ni nani? Ili kumtambua mnyama wa pili, ni lazima kwanza tumtambue kwanza mnyama wa kwanza.Mnyama wa kwanza aliyepata jeraha la mauti ni kanisa la Romani Katoliki na Upapa. Hapa tutapitia kidogo sifa za mnyama wa kwanza katika Ufunuo 13.

…Aliinuka kutoka baharini.

Ufunuo 13:1 “Kisha nikaona mnyama akitoka katikabahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Mnyama = Taifa/ufalme.

Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”

Bahari/maji = Watu, jamaa, lugha, na mataifa.

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”

Ukatoliki wa Romani ulitokea ulaya ya magharibi pamoja na makutano ya “watu/jamaa, mataifa, na lugha.” Na kwa wakati huu kanisa la Romani Katoliki lina idadi kubwa ya “watu, mataifa, na lugha,” kuliko kanisa jingine lolote duniani mwote.

…Ana pembe kumi.

Pembe = Ufalme/taifa

Danieli 7:24 “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.”

Zile Pembe zake kumi ni mataifa/falme kumi zilizogawanyika baada ya ufalme wa Rumi kuanguka 476BK.

…Ana vichwa saba.

Vichwa = Milima.

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”

Mwanamke katika unabii huwakirisha kanisa, hivyo vile vichwa saba ni milima saba ambayo kanisa katoliki limekalia, au ni milima saba ya dola la Roma. Hii inathibitishwa katika historia, pia katika dokomenti za kanisa la Roma lenyewe linasema…

“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.

ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma
“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine

(#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline,
(#2) Quirinal,
(#3) Viminal,
(#4) Esquiline,
(#5) Caelian, (#6) na Aventine
(#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –http://www.britannica.com/seo/s/seven-hills-of-rome/
…Atapokea jeraha la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake lake la mauti likapona…”

Utawala wa upapa ulipata jeraha la mauti mwaka 1798BK baada ya kutawala miaka yake 1260 iliyotabiriwa katika unabii, iliyoanzia mwaka 538BK hadi 1798BK. Napoleon alipomtuma Jemedari wake Berthier kumuuondoa Papa madarakani.

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Sasa wakati huu huu wa jeraha la mauti ni kama ule unaoelezewa katika Ufunuo 13:10 kwamba, “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga…”

Upanga = Vita

Papa alifanya vita na kuteka na kuwaua Wakristo zaidi ya milioni 100,000000 wakati wa utawala wa upapa wa miaka 1260. Hivyo yeye pia angechukuliwa mateka, na kuuwawa kwa upanga(vita), vile vile kama yeye alivyokuwa amefanya kwa wengine.Jambo hili lilitimia mwaka 1798BK wakati Berthier alipokuja kufanya vita juu ya Upapa, na kuuondolea mbali kabisa. Na mwaka uliofuata; yaan, 1799BK Papa alikufa; kwa maana “yeye alikuwa amechukua mateka, naye akachukuliwa mateka, yeye alikuwa ameua kwa upanga (vita), naye akauwawa kwa upanga(vita).


Hapa ndipo tunaanza kupata wakati sahihi wa kuanza mnyama wa pili; kwa sababu baada ya Upapa kupata jeraha la mauti, au kuchukuliwa mateka na kuuwawa kwa upanga(Ufunuo 13:10) mwaka 1798BK, ndipo katika Ufunuo 13:11 tunaona mnyama mwingine akiinuka kutoka katika nchi. Wakati/muda wa kuzingatia ni mwaka 1798BK baada ya Upapa kuuwawa kwa upanga(vita) ndipo na mnyama wa pili anainuka wakati huo huo kama Ufunuo 13:11 inavyosema…

Ufunuo 13:11-12 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.”

Mnyama wa pili angeinuka kutoka katika nchi baada ya mnyama wa kwanza ambaye ni Upapa kupokea jeraha la mauti, au kuuwawa kwa upanga mwaka 1798BK. Huko nyuma tuligundua kuwa mnyama katika unabii huwakilisha ufalme/taifa, hivyo wakati wa mnyama wa kwanza (upapa) anapata jeraha la mauti, lingeinuka taifa lingine kutoka juu ya nchi. Je kuna taifa lolote lililoinuka wakati huo? Kwa hakika ni taifa la Marekani (USA) pekee lililoinuka katika nyakati hizo. Hapa tutajaribu kulinganisha sifa za mnyama wa pili, na taifa la Marekani ili tuone kama taifa hilo la Marekani linatimiza unabii huu wa mnyama wa pili kwa ukamilifu.

…Angeinuka kutoka katika nchi.

Ufunuo 13:11 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.”

Kutoka katika nchi(sehemu kavu) ni kinyume cha kutoka katika bahari(sehemu yenye maji). Huko nyuma tuliona kuwa “bahari” inawakilisha “sehemu yenye watu wengi tofauti”, hivyo “nchi” ni kinyume chake na inawakilisha “eneo lisilo na watu wengi.” Jambo hili linafaa kwa taifa la Marekani, liliinuka mwishoni mwa karne ya 18, miaka ya 1776BK likiwa na watu wachache. Mwandishi mmoja aliandika kuwa taifa la Marekani…

“Siri ya kuja kwake kutoka katika sehemu tupu, kama mbengu ya kimya kimya tulikua hadi kufikia kuwa dola.” -Vandeman, GeorgeDestination Life, (Mountain View: Pacific Press Pub. Assoc., 1980), p. 74

…Angekuwa na sifa za mwana-kondoo, lakini angenena kama joka.

Ufunuo 13:11 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.”

“‘Naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo’ Pembe mfano wa mwana-kondoo zinaashiria ujana, na umakini, na zinawakilisha uhuru wa kiraia na kidini. Utangazaji wa uhuru na kanuni vinaakisi maandhari haya ya uadilifu. Kwa sababu ya kanuni hizi kabisa, taifa letu limekuwa kuu. Walionewa na kuteswa katika nchi zote walipaangalia U.S (Marekani) kwa tumaini.” -White, E.G.Cosmic Conflict, (Washington: Review & Herald Pub. Assoc. 1982), P. 388

Karibu kila mmoja anafahamu historia hii. Wakati wa utawala wa Upapa mwaka 538-1798BK, uliua Wakristo wa Kiprotestanti zaidi ya milioni 100,000000, hivyo wakati wa miaka ya 1776BK Wakristo wengi walikimbilia katika nchi ya Marekani ambako kulikuwa na uhuru wa kuabudu. Kwa hakika hali hii ya uhuru wa kuabudu, na kutetea haki na uhuru wa dini, ndiyo inawakilishwa na kuwa na “pembe mbili mfano wa mwana-kondoo.” Karibu kila mmoja anajua Wakristo wa kweli katika Maandiko huwakilishwa kama “kondoo,” lakini Wakristo wa uongo huwakilishwa kama “mbwa-mwitu.” Hivyo, taifa la marekani liliwakilishwa kwa mfano wa mwana-kondoo kwa kitendo kabisa cha Wakristo wa kweli walioteswa na Upapa kukimbilia huko, na kwa kitendo cha taifa lenyewe kulinda uhuru wa dini kwa ajili ya watu wa Mungu.


Lakini Ufunuo 13:11 inasema tena kuwa, taifa hili hili lenye mfano wa mwana-kondoo litanena kama joka.

Joka = Shetani/ibilisi

Ufunuo 13:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”

Kama taifa la Marekani lingekuja kunena kama joka, hii inaashiria kwamba lingekuja kufanya mambo ya kishetani yasiyopendeza mbele za Mungu. Taifa la Marekani lina pembe mbili kama za mwana-kondo, lakini linanena kama joka. Ukiangalia hatua za taifa la Marekani; matendo yake, na maneno yake utaona kabisa kuwa taifa hili linanena kama joka. Jinsi linavyoua watu katika vita, linavyoua watu kwa kutumia sumu, linavyotoa amri kwa mataifa mengine yafanye kama linavyotaka lenyewe, hii ni wazi taifa la Marekani linafanya mambo mengi ya kishetani. Lakini unabii hauishii hapa, bali unasema zaidi kuwa taifa la Marekani (mnyama wa 2), na Vaticani (mnyama wa 1) wataungana ili kulazimisha alama ya mnyama.

Ufunuo 13:12 “Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.”

Unabii unasema Marekani inatumia uwezo wa yule mnyama wa kwanza (Vatican), na itawafanya watu wote wamsujudie mnyama wa kwanza (Vatican) ambaye alipata jeraha la mauti. Ukiangalia hatua zinazofanywa na taifa la Mrekani na Vatican, utaona kuwa kanisa Katoliki linaitumia Marekani ili kukamilisha anachokitaka mnyama wa kwanza, Marekani itatumiwa na Upapa ili kuwalazimisha watu wasali siku ya jumapili,kulazimisha ndoa za jinsia moja .

Vatican na Marekani zinashirikiana ili kulazimisha alama ya mnyama, sheria za bluu (blue law) za taifa la Marekani, na Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Change) ajenda ya Papa vyote lengo lao ni moja kupitisha sheria ya jumapili ulimwenguni. ,kupitisha ndoa za jinsia moja, kupunguza idadi ya watu ulimwenguni, na mengine mengi, .Mwisho...


TUJIANDAE KUMLAKI YESU MAWINGUNI
 

ngoroki

Senior Member
Joined
Jun 7, 2015
Messages
154
Points
225

ngoroki

Senior Member
Joined Jun 7, 2015
154 225
Roman empire wanatawala dunia ila America ni superstar tuu kama walivyo wasanii wake wa music wanajulikana kuliko ata viongozi wa serikali ya marekani
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Messages
690
Points
1,000

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2011
690 1,000
ukiongelea roman catholic, it comes from vatican na roma its from italy, vatican ni kama nchi ndani ya italy inajitegemea kwa killa kitu. ROMAN EMPIRE died so many years ago. soma kitabu IN GOD'S NAME cha DAVID YALLOP utailewa vizuri Vatican
 

Madikizela

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2009
Messages
519
Points
250

Madikizela

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2009
519 250
MFUMO WA HAWA JAMAA UMETISHA SANA HEBU FIKILIA KWANZA TUU....

1.CHRISMASS WAMEANZISHA WAO WAKATOLIKI.

2.CALENDER TUNAYOITUMIA DUNIANI TUNATUMIA CALENDER YA KWAO .

3.MWAKA MPYA TUNASHEREKEA KWA SABABU NI WAOO.

4.MFUMO WA KISERIKALI KUTAWALA WANANCHI WAMEANZISHA WAO .

5.PASAKA SIJUI MWAKA MPYA NI WAO .

YAANI KARIBIA MIFUMO YOTE TUNAYOIFATA HAPA DUNIANI TUNAIFATA KWA KUWASIKILIZA WAO SASA HAWA JAMAA UNAFIKILI UTAWAKWEPA KWEPA VIPI AISEEE NA HADI LEO HII TUNAVYOZUNGUMZA HAKUNA KIONGOZI ALIYESIMAMA NA KUPINGA MIFUMO HIII
Kwa hivyo,hata mwaka wa kiislamu utasema ni wao, idd el Hadji na fitri itakuwa ni wao? Mwishoe mtadai na BAKWATA pia ni wap
 

1kush africa

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Messages
6,501
Points
2,000

1kush africa

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2016
6,501 2,000
Katika pitapita zangu nilikutana na mjadala kuhusu maswala kuhusu Marekani na utawala wa Roman empire ndani ya kanisa katoliki.

Wapo wengine wanafikia hatua wanasema kiongozi yoyote au rais yoyote ambae anaenda kinyume na itikadi za Roman anaweza ondolewa au kuuawa.

Wapo wanaosema Roman katoliki chini ya Roman ndio ana nguvu ya kutawala dunia na wengine wanasema Marekani ndio baba wa dunia

Hebu wana JF naombeni mawazo yenu kuhusu utawala wa Roman empire katika hii dunia na Marekani.
soma story inaitwa Queen Monica, ipo humu utajua mambo mengi
 

fidel castro wapili

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Messages
951
Points
500

fidel castro wapili

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2017
951 500
Kwa hivyo,hata mwaka wa kiislamu utasema ni wao, idd el Hadji na fitri itakuwa ni wao? Mwishoe mtadai na BAKWATA pia ni wap
BAKWATA ni wao kwasababu ilianzishwa na Mkatholic J K NYERERE. Amri ilitoka makao makuu akaamrishwa vunja Jumuiya ya kiislam ya Afrika mashariki uwaundie baraza ambalo utalitawala na usilipe Ruzuku ili likiwa halina uchumi utalitawala kiulaini.
 

blue bahari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Messages
444
Points
250

blue bahari

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2016
444 250
KWA KIFUPI TUU ROMAN EMPIRE ILIANZA MIAKA YA ZAMANI SANA KIPINDI CHA 30 B.C YAANI BEFORE CHRIST .

KWA MIAKA YA ZAMANI ROMAN EMPIRE ILITAWALA BARA LA ULAYA PEKEE LAKINI BAADA YA MIAKA KWENDA ROMAN EMPIRE KATIKA KUJITANUA NGUVU ZAKE ILIBIDI WAANZISHE DINI ILI WAENDELEZE NGUVU ZAO KUITAWALA DUNIA HIVYO ILIBIDI WAIVUNJE ROMAN EMPIRE NA KUANZISHA ROMAN CATHOLIC KWAIYO ROMAN KATOLIKI KAMA DINI LAKINI IMEVAA KOTI LA ROMAN EMPIRE ILI WAENDELEE KUITAWALA DUNIA.

BAADA YA KUANZISHA ROMAN KATOLIKI HAWAKUISHIA HAPO PIA WALIANZISHA MFUMO WA SERIKALI NDANI YA KATOLIKI KUWA KITU KIMOJA LAKINI SERIKALI INAKUWA IPO CHINI YA KANISA KATOLIKI NA HAPO NDIPO WALIPOFANIKIWA KUITAWALA DUNIA.

LAKINI PIA WAKATOLIKI WAMETENGENEZA SYSTEM ZA KIJASUSI AMBAYO KIONGOZI WA NCHI YOYOTE DUNIANI NI LAZIMA AFUATE MFUMO WA KIKATOLIKI NA UKATOLIKI UNAVYOTAKA NA ENDAPO KIONGOZI YOYOTE YULE ATAJARIBU KUUPINGA ULE MFUMO BASI ATAUWAWA KUPITIA KITENGO CHAO CHA UJASUSI CHA JERSUIT HIVYO HAWA JAMAA WANA POWER OVER GOVERMENTS DUNIA NZIMA
Uko vizur, na ndio uharisia. Watakubishia tu.
 

Forum statistics

Threads 1,344,660
Members 515,970
Posts 32,831,179
Top