jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mimi binafsi nasema ni jambo la kumshukuru Mungu kwasababu amejibu maombi yetu na tumeishinda corona.
Hatahivyo ninafahamu kuwa kuna wale ambao nyungu imewasaidia. Kuna member humu waliotoa ushuhuda.
Kwa hali inavyoendela, dawa tunazo za kutosha zimezinduliwa na wataalam wetu na kuthibitishwa na serikali. Mtaani maisha yanaendelea fresh kabisa na watoto wanarudi Shule karibuni huku tukiendelea kuchapa maombi na dua!
Lakini mafanikio haya ya kuishinda corona, wengi wamempa sifa rais kwa sababu hakuweka lockdown kama mataifa mengine na kwahiyo apewe sifa anazostahili. Pia ni yeye aliyetutaka tufanye maombi na baadaye kujifukiza. Kwahilo pia anastahili sifa zake kwakuwa tumeishinda covid-19.
Lakini swali langu hili ni la muhimu kwasababu kuna wale waliokuwa wakiamini kuwa maombi yatasaidia na kwamba yamesaidia, lakini pia, kwa upande wa pili, kuna wale waumini wa nyungu! Hao nao wanadhani ndiyo imesaidia kuishinda covid.
Hata hivyo kuna wale wanaodai mambo ya nyungu ni uchawi. Hii sijui imekaaje? Hao lazima wanaamini ni maombi na siyo hizo nyungu. Lakini pia tusiwasahau na wataalam wetu ambao wamegunduwa dawa za corona.
Ni wazi kuwa mataifa mengine yatakuja kutaka kujifunza kutoka kwetu na pengine kupata dawa nk. Wengi wetu kusema kweli tulishangazwa na hatua za rais kukubali mikusanyiko ya kuliombea Taifa na hata sasa mikusanyiko hiyo bado ipo na corona imefutiliwa mbali. Hivyo maoni yangu mimi, ni MAOMBI yamefanya kazi.