Hivi karne hii bado waafrica tunahitaji elimu, elimu, elimu?

kivangaukali

Member
Jan 8, 2016
72
26
Naomba kujua tunahitaji nn na turudi nyuma nakuona tulikosea wapi na bado tunaendelea kukosea. Kwa kuamini elimu ni kitumwa iko siku itatukwamua kimaendeleo hivi. Kunaingia darasani kwa muda wa zaidi ya miaka 18 mwisho wa hiyo elimu ni kutumwa.

Je na sio umefika wakati wa kujitambua na kuanza kufikiri turudi kwenye zama zetu za kale na kuona babu zetu walifanya nini na kupata mafanikio amabyo leo sisi tumeyafanya makumbusho. Naanza kwa mfano viwanda vile viwembe, visu, majembe, vijiko nk ambavyo tumevihifadhi kama kumbukumbu.

Kule Isamila badala ya kujifunza walifanyaje na kuboresha kwa kujiongeza na kupata kilichobora sisi tunafanya kumbukumbu. Tunaacha kujifunza namna gani maliasi zetu zikoje na kuziendeleza tunajenga madarasa ya kuongeza watumwa zaidi. Tufikirie na kufanya uvumbuzi na kuandaa masomo yanayoweza kutusaidia kutokana na rasilimali zetu.

Tunaendelea kutegemea mawazo na maligafi kutoka ughaibuni jamaa walitutaiti na elimu ya kitumwa. Na sisi tunapiga makofi na usomi usiokuwa na tija kwa Taifa zaidi ya kutengezeza majitu mabinafsi na yasiyo na mapenzi ya nchi yao. Hatuna sababu ya kufundisha vitu tukiwa watu wazima tuanze na shule za chini kabisa mtoto aandaliwe akiwa na umri wa miaka 3 aanzishwe kujua kufanya kitu cha kuleta hela na na si shule ya kusoma akimaliza afanywishwe kazi apate pesa.

Tubadilishe mfumo wa elimu ya kitumwa na tuanze kutengeneza elimu ya kujituma. Wandugu nina mambo mengi ila yanahitaji majadala mpana naomba watanzania wenzangu tuanze kutafuta dawa ya hili tatizo kwa kuanza. majadiliano ya pamoja kwani ili tupate ufumbuzi wa kudumu na ni ushauri wangu tuanzishe kongamano kuhusu ELIMU YA KITUMWA NA ELIMU YA KUJITUMA.

Karibu kwa mjadala.
 
Nafikir ingefaa kutafakar nililoandia kuliko kukusoa maandishi labda uwe hajelewa kilichoandikwa ongezeni uwezo wa kufikir mtapata jambo la kutafakar katika hiyo hoja
 
Nafikir ingefaa kutafakar nililoandia kuliko kukusoa maandishi labda uwe hajelewa kilichoandikwa ongezeni uwezo wa kufikir mtapata jambo la kutafakar katika hiyo hoja
Ndugu yangu hivi umesoma somo la historia vizuri kweli mpaka hapo ulipofikaia na umri huo?
 
Back
Top Bottom