Hivi kama vijana wanaambiwa wafanye kazi yoyote kwanini wanaenda chuo?

"Sasa hivi ajira ya kuaminika ni kubeti tu, ukishazijua ligi kama 3 vizuri, ukiweka mkeka wako lazima utoboe, huko shule ni kupotezeana muda tu" alisikika kijana mmoja aliyehitimu chuo kikuu
 
Sasa hiyo si akili yako wewe unamlaumj nani?wewe na wazazi wako ndo mnaochagua usome nini,sasa unachaguliwa na mwingine au unalazimishwa? Hv waTanzania mna shida gani kichwani? Toka unasoma wewe na washauli wako hasa wazazi ndo wanakuchagulia na wewe unakubali,sasa shida na lawama ni kwa nani
Kama ulipata bahati ya kushauriwa na wazazi basi hongr lkn wengine wazazi wao hawajaenda shule ndo yeye ameanzisha kwenda shule.
Halafu asilimia kubwa kozi na combination watu wanachaguliwa mpaka kozi watu wanachaguliwa wasizo zichagua hujawahi ona hilo???
 
Serikali iweke somo la LIFESKILLS liwe compulsory kwa kila mtu anayepita chuo kwa kipindi chote anachokua chuo ili waweze kujifunza

Focus and Self-Control. Children need this skill to achieve goals

Perspective Taking

Communicating

Making Connections

Critical Thinking.

Taking on Challenges.

Self-Directed, Engaged Learning.

+Money savings
+Time management
+Entrepreneurial skills
+selling

Pamoja na mtu kuwa na profession yake ili aweze kuwa na plan B ni lazima awe na ujuzi huo ambao wengi wanaukosa.
Hili ni LA lazima mkuu..!!

#YNWA
 
Sasa hiyo si akili yako wewe unamlaumj nani?wewe na wazazi wako ndo mnaochagua usome nini,sasa unachaguliwa na mwingine au unalazimishwa? Hv waTanzania mna shida gani kichwani? Toka unasoma wewe na washauli wako hasa wazazi ndo wanakuchagulia na wewe unakubali,sasa shida na lawama ni kwa nani
Doh!
 
Ndo ujue kusoma ni kupanua mawazo tu na si kupata pesa,tambua ya kwamba kazi si lazima iendane na ulichosoma,wanaofanya kazi inayoendana na elimu yao ni wachache na hazipo office za kuajilii wote hao,serikali na nchi zote duniani watu wamesoma lakini wanaendesha mambo yao mengine kabisa,na haipi serikali yoyote itakayo ingilia mamlaka ya MUNGU aliyo mpa mwanadamu kua kwa jasho la uso wake atakula,then ije serikali ikulishe au ikuoe kirahisi eti kwa sababu mlisoma,ondoeni fikra mfu za kua ulisoma unapaswa kuishi vzr,waingereza mliwasikiliza sana na hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni na sasa mnahangaika huku mkiwa mmepoteza pesa na kupewa karatasi na fikra za kujiita boss.

Elimu haikupi pesa ila inakurahisishia kupata pesa na maisha mazuri na ndio maana watu wengi wa kipato cha kati ni wale wenye kada maalumu....

Nachokiona wengi wanawalaumu wasomi kwa sababu kuna mawazo mfu sana kuwa kila anaeingia chuoni bhasi automatically ni mjasiriamali. Huu ni uongo, chuoni kuna kada nyingi na zingine zinahitaji ofisi ONLY

Ajira si kitu kibaya na serikali haiwezi kuajiri watu wote much less kwa sasa ambapo ajira hazitolewi kwa wingi hivyo, Serikali ikiweka mazingira mazuri ya uwekezaji nadhani sekta binafsi inaweza kusaidia sana...

Narudia, huwezi kumlaumu mtu aliyesomea ualimu kutokua na maarifa sahihi ya kuendesha biashara..sio kada yake na hana tofauti na wewe ambaye hujasomea biashara
 
Habari za saizi
Samahani niko nje ya mada
Mimi ni msichana wa miaka 20 natafuta kazi mjini elimu yangu ni form six niliwahi kufanya kazi internate cafe
Naweza kutumia computer
Naweza kuongea kingereza
Naweza kuongea kiswahili
Pia nilisoma clinical officer mwaka 1 ila nikaacha sababu ya kifedha kwaiyo nina knowledge ya kupima vital signs na kuelimisha jamii kuhusu nutrition
Pia naamini kuna kazi za kueleweshana kikubwa uaminifu na kujituma katika kazi
Nawezo wa kufanya kazi mapokezi,kwenye internate cafe,na zingine nyingi

Nitafurahi sana nikisaidiwa
Nipo dar es salaam
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom