Hivi kama kodi zinajikata zenyewe kwa njia ya mitandao kuna haja ya kujaza watu wa kodi maofisini?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,293
8,204
Kwa nilichokuja kugundua ni kwamba kodi nyingi sasa zinatokea kwenye miamala ya simu tunayotuma na kupokea.

Kwa njia hiyo inamaanisha kwamba zikijikata tu zinaingia, moja kwa moja kwenye akaunti ya kodi hivyo automatically zinajihesabu zenyewe. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Sasa kama mambo mazuri ndio hayo nilikua nawaza na kuwazua hapa.

Hivi kama kodi zinajikata zenyewe kwa njia ya mitandao na kujihesabu kuna haja ya kujaza watu wa kodi maofisini.

Yaani hamjanielewa, ni kwamba hivi kunahaja ya kuweka watu wa hesabu ili kuhakiki hizo hesabu wakati zinajikata zenyewe automatically. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Napenda maswali ya kejeli.
 
izo kodi unazoongelewa wewe hazikuwepo mwanzo na amna watumishi wapya walioajiriwa kwajili ya kuzisimamia. na hata hizi kodi ambazo zipo toka zamani kama VAT kodi ya mapato nk. bado watumishi hawatoshi kabisa.

kazi ya kodi sio ndogo... sio suala la kukusanya tu kuna masuala ya kuhasibu ambayo ni kufanya ukaguzi wa walipakodi kama wanacholipa ni sahihi.

kwa watumishi walipo TRA kule bado ni wachache sana. kampuni nyingi zinapitisha hata miaka minne hazijawai kukaguliwa kutokana na uhaba wa watumishi
 
Ukiona sehemu kuna foleni kubwa ya kungojea huduma,jua ya kuwa watumishi na vitendea kazi havitoshi
 
Back
Top Bottom