Hivi kama JK ngalichukua uongozi baada ya Mwinyi tungelikuwa wapi leo hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kama JK ngalichukua uongozi baada ya Mwinyi tungelikuwa wapi leo hii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serendipity, Dec 22, 2009.

 1. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wana JF, Huwa najiuliza, pamoja na mabaya yote aliofanya Rais mstaafu,Ndg BW Mkapa, lakini aliweze angalau kufufua uchumi(ambao ulikuwa kama umekufa vile- yaani nikaribia tungeifikia hali ya sasa Zimbabwe)
  Mkapa aliweza kulipa madeni nje, alijenga barabara, ali control inflation n.k
  Sasa kutokana na utendaji( au mwenendo wa utendaji) wa Mh. JK, je angechukuwa nchi kutoka kwa Mzee Mwinyi angetufikisha wapi? Au ndo tungekuwa kama Zimbabwe ya leo?
  Japokuwa sina data kamili, lakini nahisi katika muda JK aliokaa madarakani hali ya uchumi imezidi kuwa mbaya kuliko wakati alivyo kabidhiwa na Mkapa.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Sasa kama huna data.unaongea vipi?
  Kwa nini usiwe na data kwanza?????
  Ni lini tz ilikaribia zimbabwe?
  Labda wakati wa nyerere ndo tanzania ilikaribia zimbabwe......
  No research,no right to speak..........
   
 3. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  The BOSS, nimesema sina data kamili, hii inamaanisha kwamba data ninazo lakini hazijakamilika( wadhungu wanaita raw data!)
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tanzania ingekuwa kwenye deathbed.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wewe ni mshabiki zaidi.
  Huongei ukweli.....
  Wakati wa nyerere ndio watanzania
  walikuwa na foleni ya unga na sukari.....
  Hakukuwa hata na colgate....
  Sasa kufanana na zimbabwe ndio ilikuwa
  enzi hizo.sio sasa wala wakati wa mwinyi
   
 6. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sasa hivi watu wangetembea na nepi au zile chupi 007
   
 7. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bandugu,

  The guy is right, tujaribu kuwakilisha issue kutokana na jinsi unavyoweza kuiona kwa sasa, sijui tunaposema uchumi unakua tuna maana gani? comparing imports over exports?, inflatiotion issues? security capabilities, making more friends out? being politically stable? kujitoshereza kwa mahitaji muhimu kama foods, drugs, infrastructures and so on?

  Kwa nyerere I think he managed to balance between imports and exports? and that is why we had a kind of respect we deserved. there were no inflation and our currency had value. Nafikiri what gave us problems by then was education and self awareness to many citizens. sidhani kama kufoleni kwa ajili ya mchele ni umasikini just taratibu and control measures.

  Mwinyi completely destroyed our country, he lost control ya kukusanya kodi, hakufanya kitu tu me zaidi ya kuwapa madaraka wananchi kufanya watakavyo. hali hiyo ilipelekea hata mishahara ya serikari kulipwa na wahindi. kumbuka vinoti vichafu wakati wa mishahara. education lost its value, people decided to be politician and wafanyabiashara rather than working.

  Mkapa did a lot in reinstating the situation. Ni kawaida kwa wanadamu hawaridhiki.

  Huyu ndugu yetu anatuua kabisa sidhani kama anazijua economic indicators:confused:
   
 8. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  pumba tupu
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mzee unameza misemo yako...
  No research,no right to speak..........
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mnaopinga hebu muwe wakweli, four years in office after mkapa who took the office with dead economy na akaufufua, Jk mpaka leo amekuwa na strategy gani mpaka sasa? I think TZ isingekuwa kama ilivyo sasa maana I am sure hata jk anakula hazina aliyotunza Mkapa. Jk mhhhhh...........?
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ya kutaka data kwa kila kitu mara nyingine yanatumika kuficha uvundo! Unaweza kuwa na data za kitu au tukio kama vinaweza kupimika[ quantifiable] lakini kuna mambo mengine yanaweza kuwa observed qualitatively, nikiwa na maana kuwa huwezi kupima matukio hayo!! Sasa kutoweza kuyapima sio maana yake hayapo la hasha, kwahiyo mtu anaweza kufanya qualitatve observation na kujenga hoja bila kuwa na data! Mfano ni wingi wa watoto wanaoishi katika hali ngumu hapa DSM, ingawa unaweza kuwahesabu lakini kwa kuangalia tu utagundua kuwa hawa pamoja na omba omba wameongezeka kwa kiwango kikubwa ukifananisha na hapo nyuma!! Hapo mtu hawezi kusema kuwa huna right ya kulizungumzia hilo simply because hujawahesabu hao omba omba na hao watoto!
   
 12. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  zipi ulizoandika au ? toa hoja tukuelewe !!!!!111

  wajameni.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tusingekuwa kwingine kokote tofauti na hapa tulipo
   
 14. kibanzi

  kibanzi Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  achani kuongelea ki ushabiki , eti mwinyi kaipeleka nchi pabaya mmesahu kuwa watu wote wa tz tulikuwa tuvaa nguo za aina moja , ilikuwa issue kubwa mtu akimiliki TV unaonekana kama umetoka mbinguni amekuja mwinyi kila kitu kimekuwa hamna shida ya watu kuhangaika na mahitaji kama hayo kwa hiyo tuache hizo hoja za kusema mkapa kafanya nini na jk nae kafanya nini kila mmoja amekuja kawa wakati wake na mda wake wote walifanya mazuri na mabaya.
   
 15. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mwaga point basi!
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tungelikuwa labda tumekufa kabsaaaa
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Huyu ndiye rais wa kwanza mchumi TZ halafu unasema hajui economic indicators. Periorties tu ndiyo zina tofautiana kutoka awamu mmoja kwenda nyngine.

  Periority ya sasa ni kufuja hela na kusafiri nje kujifunza wengine wanaishije. Swala la kujenga uchumi ni after 2015. hakuna haraka TZ tunakimbilia wapi.

  Visingizizo vyetu kwa nini hatujaendela ni vingi tu kama vile tulisaidia ukombozi wa bara la Africa; Waingereza hawakuindeleza nchi; Waingeleza hakutupa elimu kama wenzetu; siasa za ujamaa zimefail; Mikataba ya madini ilikosewa; Tatizo la umeme ni mpango wa mungu (Hakuleta mvua) n.k.
   
 18. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Aisee hapo umenena. Ila..... why accepting more risks
   
 19. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Ana elimu ya chuo kikuu(UDSM) KATIKA FANI YA Uchumi!!!sasa sijui kama hajui economic indicators!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ki msingi hawa viongozi wetu wengi ni wababaishaji ukiondoa Nyerere ambaye atalindwa kwa nia njema ya kuipenda nchi yake na hakuwa na wa kumuiga ki utawala ili kulinganisha kwamba mwenzake alikosea wapi ili yeye ajirekebishe. Kipindi ambacho nchi haikuwa na wataalamu wa kutosha kwa kuwa idadi ya watanzania waliokuwa wamesoma enzi hizo walikuwa wachache na ndio maana wengine (viongozi) waliokuwa wanafanya makosa madogo madogo walikuwa wanahamishwa badala ya kufukuzwa hii ilitokana na hali halisi. Na mengi ya makosa tunayoweza kuyaona leo katika awamu hiyo angalau tunaweza kusema mambo yalifanyika kwa nia njema ya nchi hii na kuzingatia uhalisia wa Tanzania ya wakati huo.

  Mkapa alianza vizuri lakini akaja boronga kutokana na kuwa na washauri wabaya na baadaye kuwa dictetor fulani ambaye ni washauri wachache tu waliweza kumpa ushauri. Tunavishukuru vyombo vya habari havikufumbia macho mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika wakati huo pamoja na misukosuko waliyopata. Mambo mengi yalisemwa Mkapa alifunga masikio, na alifikia hatua ya kuwaambia wananchi wake wana wivu wa kijinga na uvivu wa kufikiri. Binafsi sina cha kumsifia mkapa kama mfano wa kiongozi kwa sababu kiongozi huwa hapewi sifa za kitoto, kiongozi anapaswa kuwa mtu timamu na anafanya mambo kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria alivyoapa kuvilinda. Kwa hiyo kusema kwamba alifanya mambo mazuri halafu baadaye akaanza kuchukua chake mapema hizo sio sifa za kiongozi. Tumtetee kiongozi kwa wizi aliofanya akiwa ikulu ya wananchi, wananchi wengine muwapeleke mahakamani hii ni unfair. Haki elimu ilifungiwa kulikuwa na sababu zozote za kitaifa au ilikuwa kero tu masikioni mwake na wapambe wake.

  Kikwete naye naona matatizo yanatokana kwa kiasi kikubwa na ushkaji uliopo serikalini, kwa sababu kuna mambo ambayo hata kiranja wa shule angeweza kuyatolea tamko yeye analala usingizi wa pono na serikali yake ya kishkaji.

  Ushauri: Ni vyema angechagua watu bora wenye taaluuma zao na awape uhuru wa kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma zao tungesogea mbele. Kilichopo sasa inaonekana kwamba analipa fadhila kwa gharama za kodi za wananchi na hii imepelekea kuchagua bora watu bila hata kujali taaluma, sifa kubwa ikiwa ni wanamtandao, matokeo ndio haya tunayaona inafika wakati waziri mkuu analalamika bungeni, katika mazingira ya namna hiyo unategemea nini hapo, utasema kuna serikali hapo?

  Tuombe mungu labda kiongozi maalum kwa ajili ya TZ bado hajazaliwa.
   
Loading...