Hivi kama CCM wangetumia 3 bil. kupuleka maendeleo Igunga wangefanya kampeni tena??

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,690
625
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mmrefu sasa kwamba ikiwa kiasi kikubwa cha pesa ( 3 bil. kam ni kweli) kilichotumika ktk kampeni za CCM kingetumika ktk shughuli za maendeleo pale Igunga, kungekuwa na haja gani tena kufanya kampeni? Wanaigunga wanahitaji maji safi & salama, barabara, huduma za afya nk. Si kwamba CCM haikujua shida ya barabara(ndio maana walikodi helcopter). Naamini kiasi hicho cha pesa kingweza kuleta mabadiliko makubwa pale Igunga.Naamini hitaji la wanaigunga halikuwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM kuhamia pale,bali maendeleo yao. CCMisingehaha kusambaza mahindi yachakula kwa wananchi siku mbili kabla ya uchaguzi. Naamini wanaigunga wanahitaji kuwezeshwa kuzalisha chakula chao wenyewe, kwa kujengewa miundombinu ya umwagiliaji.

Pili, wangeongea na Rostam akawasidia hata nusu ya mabilioni haya tunayotarajia kuilipa dowans angalau tukajua kuna wenzetu wamenufaika na malipo haya. Naamini kwa kufanya hivyo CCM wangekuwa wamemaliza kampeni yao, wangebaki tu kusubiri kutangazwa washindi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom