hivi JOTI wa zecomedi ni mwanaume?

Jamani, Joti huwa anapatia sana kuvaa uhusika. Anaweza kuigiza kama mzee sana, kama kijana, kama kilema, kama mtoto wa shule na kama mtu mwenye pengo, na kama mwanamke pia. Kwa hiyo ni kipaji alichomjalia Mungu, na kwa njia hiyo ya maaigizo halali anayofanya inamudu kuendesha maisha yake. Tusimtafasiri kwenye eneo moja tu la kuwa kama mwanamke!
 
Nashukuru ndugu zanguni kwa mada hii inaonekana ya kitoto lakini ukweli mtaujua baada ya maelezo haya hapa chini
1- Joti ni msanii, na mara nyingi msanii anaigiza mazingira ya watu wa jamii yake au karibu na jamii yake,mfano afrika muvi nyingi zinaongelea mambo ya kishirikina kwani ushirikina umetawala sana africa. Sasa kama mtu anaigiza kitu ambacho hakipo anakifanya kizoeleke ktk jamii husika inayoona kitu hiki.Mfano Zamani kulikuwa hamna tv za kuonesha miziki y magharibi sana(rap,hip hop etc ndio maana watu walijikita kupenda nyimbo za zipompapompa na za kina chidumule,lakini punde tv,video zilipo kuja kwa kasi watu ndo wakaanza kiuwajua kina Mc Hammer,tupac etc. Hapa joti anauingiza ushoga taratibu katka kizazi chetu huku watu wakichekelea,
2- Kwa hapo juu kuna mtu anasema kuna wengine wanaigiza ujambazi na kutumia silaha, hata kama huyu mtu si jambazi mtoto wako au wa jirani yako atajifunza kwamba kuua ni kawaida kupitia msanii huyu kama tunavyoona marekani mtoto alipoamua kutekeza mwalimu na wanafunzi wenzake.
3- Joti anapanda mbegu ya ushoga ambapo wewe bado kuona matunda yake kupitia mwanao ambaye hajakuwa tuu na hii roho kutenda kazi ndani mwake.

Angalizo: Huyu joti,movie za ujambazi,na tamthilia kwako wewe unaweza kuweka limit kwani akili yako imekomaa lakini kwa kizazi kidogo au mtu mzima ambaye hajakomaa fikra inakuwa ni hatari ( Kuwa mwangalifu)
 
...hiivi, kipaji cha muigizaji wa kiume hakiwezi kuonekana kwa yeye kuigiza kama mchawi, jambazi, kibabu, mwanafunzi nk hadi mpaka aigize UKIKE ???:thinking:
 
Hivi Joti anaigiza kama shoga au kama mwanamke?
Mbona akiigiza kama katoto ka kike hamsemi?
Heshima kwako Silent Whisper,

Mkuu nakubaliana na hoja yako lakini zekomedi kwanini hawatafuti wasichana waigize sehemu ya wanawake.Unajua kupitia Joti Tanzania inaweza kuzalisha mashoga kibao jamaa anafanya kazi ya shetani kabisa.Nimeangalia filamu na komedi nyingi sana za majuu mwanaume akiigiza sehemu ya mwanamke zinakuwepo sababu za msingi huku kwetu kina Joti wanabinua midomo na kupepesa macho tunashangilia badala ya kuwatandika viboko siku ukikutana na mwanao anajishebedua utaoana kawaida kumbe mambo yameshaharibika.
 
Anadhalilisha hata mavazi ya kike kuna baadhi ya nguo huwezi kumnun ulia mkeo au mpenzi wanaziita za joti. Lile bwabwa kudadeki zake. :doh:
 
Anadhalilisha hata mavazi ya kike kuna baadhi ya nguo huwezi kumnun ulia mkeo au mpenzi wanaziita za joti. Lile bwabwa kudadeki zake. :doh:

kama Hauna uthibitisho huwezi kumwita bwabwa, Joti ni Msanii aliyekamilika hapa Tanzania, sijawahi kumwona Msanii mwingine kama JOTI hapa Tanzania, JOTI ni msanii anayeweza kuiginza kila kipande kwa uhakika na kwa ufasaha, JOTI akiigiza kama mzee kama ndio mara yako ya kwanza kumwona unaweza kusema huyo ni mzee wa kweli kabisa, JOTI akiigiza kama mwanafunzi pia anafit kabisa na kweli unaweza kuzani ni mtoto, JOTI akiigiza kama Mzenji (mdebwedo) ukimuona kwa mara ya kwanza unaweza jua kweli ni wa huko na JOTI pia anafit vizuri mno akiigiza kama Mwanamke
Tubadilike wakuu, hiyo ni sanaa tu na huyo(JOTI) ni Msanii tu
 
bado swali lipo, yeye hayupo hapa, hebu aje hapa ajibu hili swali, kwanini anapenda sana kuigiza ukikekike badala ya ukiume..hawaoni wale wenzie wa FUTUHI star tv? anaharibu jamii.
 
wakuu, mmeongea sana lakini Joti ni msanii. sifa moja ya msanii ni kuiteka hadhira na kuuvaa uhusika wa kile anachosanii. kwa hilo Joti amehitimu. Let him be what he is, but the fact remains he is an excellent comedian.
 
kile ni kipaji adimu mkuu...! NDO MAANA WANAITWA WAIGIZAJI...!!

kama vile mtu safi anaweza akaigiza kama jambazi lenye roho mbaya ...lakini in reality he is not..! ITS NO BIG DEAL..!

kuvaa wigi, sketi , wanja na hereni ndo kipaji adimu? give us a break! anatakiwa avae character wa kiume na pale wanapotaka character wa kike atafutwe msichana, jinsi gani joti anaweza kuvaa character wa kiume na akawasilisha vizuri mada na sifa ya mwingizaji, huko tuendako itakua mwanaume ukivaa gauni basi ushakua mchekeshaji
 
mimi binafsi naiomba serikal;i yetu ipige mafufuku kipindi hicho kime haribu saana watoto tukubari tusikubari,ni hatari sana kwa nyakati za leo, mwanamke ananafasi yake katika uigizaji,mwanaume anapo igiza kama mwanamke anamaanisha nini??ili iweje wakati mwenye nafasi yupo?
sipati picha hapo.
 
mimi binafsi naiomba serikal;i yetu ipige mafufuku kipindi hicho kime haribu saana watoto tukubari tusikubari,ni hatari sana kwa nyakati za leo, mwanamke ananafasi yake katika uigizaji,mwanaume anapo igiza kama mwanamke anamaanisha nini??ili iweje wakati mwenye nafasi yupo?
sipati picha hapo.

Thubutuuuuuuu serikali gani ya kukipiga marufuku kipindi hicho, tena kipo TBC1......labda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom