Hivi JK utaacha lini kutudharau watanzania ambao ni maboss wako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi JK utaacha lini kutudharau watanzania ambao ni maboss wako?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bobby, Dec 10, 2010.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kuna mambo rais wetu amekuwa hayachukulii hatua zinazostahili dhidi ya wateule wake kwa wakati mwafaka kwa sababu ambazo sisi wananchi wa kawaida hatuzielewi so tafsiri ya haraka ya hali hii ni dharau kwetu tuliompa dhamana ya kutuongoza. Naomba nitoe mifano michache:

  (i)Mtakumbuka alipounda baraza la mawaziri mwaka 2006 alikuja na mawaziri lukuki wapatao 60. Tulilalamika na kulalamika mpaka tukachoka aliweka pamba masikioni pasi na kuchukua hatua. Mungu bariki ikaja issue ya Richmond ndio hapa sasa akaitumia nafasi kupunguza idadi ya mawaziri. Juzi kaja tena jamani na mawaziri wengine 50 kutoka 47 nadhani wa 2008. Amekuja mpaka na waziri wa mahusiano wassira (nina hamu sana ya kuiona job description yake) Ni ajabu na kweli kwamba wafadhili wetu kama UK wako busy kupunguza matumizi ya serikali sisi watembeza bakuli tuko busy kuongeza matumizi.

  (ii) Wakati wa sakata la Richmond 2008 miongoni mwa maazimio ya Bunge letu ilikuwa ni kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa AG wa wakati huo na boss wa PCCB bwana Hosea hilo halikufanyika asilani. AG aliachwa mpaka astaafu kwa mujibu wa sheria na Hosea anadunda mpaka leo. Hii ilikuwa ni dharau ya waziwazi ya rais kwa bunge na wananchi kwa ujumla. Kama haitoshi juzi tena Hosea kaivua nguo ofisi ya rais ambako ndiko PCCB iliko kwa kumsafisha Chenge kinyume cha sheria. Nashindwa kuelewa kwamba aibu yote hii bado rais anaona si kitu. Hii pia ni dharau kwetu watanzania kwamba kuna watu wanaweza kufanya lolote wakati wowote na still wasiguswe, Hosea ni mmojawapo. So JK Hosea naye anasubiriwa mpaka astaafu kwa mujibu wa sheria? Tunshukuru sana kwa dharau zako kwetu sisi maboss wako uliopita juzi na kukaa nasi mpaka sakafuni ili tu tukupe kura zetu.

  (iii) Mfano wa mwisho kwa leo ni wa bwana mrema aliyestaafu juzi Tanroads. Ni bahati mbaya sana kwamba kuna watu pasipokujua wanampa credits Magufuli asizostahili. Mrema hajafukuzwa kazi na Magufuli bali amestaafu kwa mujibu wa sheria. Mrema naye kama ilivyo kwa Hosea alifanya vituko vya ajabu sana hapo Tanroads lakini hakukuwa na wa kumgusa akiwemo rais wa nchi. Tumepiga kelele weeeeh wapi hakuna wa kutusikiliza. Hiki si kingine bali ni dharau za rais kwa maboss wake. Ni dharau kwani hao wote kwa mujibu kwa katiba yetu iliyoaachwa mbali na wakati ni wateule wake so hakuna mwingine wa kuchukua hatua zaidi yake.

  Nahitimisha kwa kumuuliza tena swali Jk, so Hosea naye pamoja na madudu yote anayofanya anaachwa mpaka astaafu kama Mrema wa Tanroads na former AG Mwanyika? Kama ndivyo kuna haja gani ya kuwa na wewe kama kazi yako ni kuteua tu na kwaacha watu wafanya wafanyavyo pasipokuchukiwa hatua yeyote?
   
 2. njiwamanga

  njiwamanga Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ataacha baada ya katiba mpya ambayo itapunguza madaraka yake na kuweka vipegele vya kumwajibisha
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mpaka sisi wenyewe tutakaposema basi inatosha vinginevyo atatudharau mpaka tukome wenyewe ,ni sisi tumemruhusu kwa hiyo tusilalamike
   
 4. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Siwez mulaum jk hata kidogo kwa hayo yote na mengineyo. Regea maandamano ya UK sasa hivi juu ya kupanda kwa tuition fees na ya Msumbiji juu ya kupanda bei kwa ngano. Unadhan sisi tukisimama wote na kusema, 'Rais acha madudu haya. Hatumtaki huyu...' ataendelea na upuuzi? Tumemlea wenyewe kama yai kwa kisingizio cha aman na utulivu. Ukondoo wa kijinga unatumaliza na mwishowe tunaishia kulalamika.
  Mpaka hapo tutakuwa na mshipa wakusisima imara na kusema 'no. We can't take this nonsense' ndio utakuwa mwisho wa dharau zake. Kwa sasa tujilaum wenyewe
   
 5. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kweli mnategemea NGEDERE amuadhibu NYANI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  JK ni fisadi na anawajibika kwa mafisadi wenziwe kina RA &EL hivyo kufikiri kuwa anaweza kusikiliza kilio cha watanzania ni ndoto ya mchana
   
 7. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  si yeye tu,na serikali ya ccm kwa ujumla,siwezi kusahau lile sakata la mishahara,ambapo raisi alisema kuwa hata wafanyakazi wagome kwa miaka 8 mshahara hautaongezeka,na baadae alipopandisha mshahara kinyemela Makamba alisema kwa kiburi kikubwa kwamba rais ndie mwajiri mkuu,hivyo ana madaraka ya kuongeza mshahara muda wowote anaotaka.ila nilifarijika sana na majibu waliyoyapata kutoka kwa mh J.Mnyika kwamba ''majibu ya Makamba yanaonyesha ulevi wa madaraka,na raisi ndiye mwajiriwa namba moja wa wananchi'' hongera mh J.Mnyika ulitutuliza kutoka kwenye dharau ile nasi hatukukutupa.
   
Loading...