hivi jk akistaafu, watu watamkumbuka kwa kusema heri aliepita???

YoungCorporate

JF-Expert Member
Apr 30, 2010
391
113
kuna hali fulani ya wananchi kumchoka raisi akiwa bado madarakani mfano mwinyi, mkapa na sasa jk. Lakini baada ya kuchaguliwa raisi anaefuata mambo huwa tofauti na wananchi wengi husema afadhali aliyepita...kwasasa watz wengi wanasema heri ya mkapa angalau hata hotuba tulikuwa tunazielewa, alikuwa na maamuzi fedha ilikuwa inathamani n.k....sasa hivi najiuliza hii trend itaendelea kwa mkulu wa sasa, sijui tutasema afadhali kwa lipi??
 
Kikwete mzee wa Kikwere kutoka msoga maeneo ya mkoa wa pwani , hahahaaaaah nitamkumbuka kwa lipi mie Mzalendo wa Taifa hili, labda kwenye Mabembea Jamaika alikoenda na kupimwa afya ya akili kuona mwenendo wake barabara, hahahahaaaaah Vasco da Gama w Kikwere, , ukimuwaza lazima utabasamu na kuangua kicheko......


oKgEyTZvcd8AAAAASUVORK5CYII=
oKgEyTZvcd8AAAAASUVORK5CYII=
 
Kwa nature ya majority ya kupenda mambo yasolviwe bila kua involved... ndo hufanya kusema bora raisi fulani....
 
Ndie raisi wa kwanza tanzania kumtimua waziri mkuu mbadhilifu na kupeleka Ex mawaziri wawili mahakamani. Hili ni jambo kubwa sana . Pili kapunguza kilio cha mtoto wa mkulim amsikini kurudia rudia darasa la saba mara kumi kwa ajili ya kutafuta secondari.

Ingawa hizo secondari bado zinalega lega sisawa na kuwacha watoto wazulule na kuja kuwa ma house boys na mahouse girls. Jifikilie sana kuwa wewe umefika secondari, ila sasa ona wale wenzako uliowaacha vijijini waliokosa bahati ya kusoma secondari maisha yao yalivyo hivi sasa. Sasa kiwete kawakomboa hao wanaaoachwa vijijini.

Mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpatieni! Raisi ni mtumishi wa wanachi na utaona tuu jinsi alivyowagusa wananchi kwa huduma fulani fulani,kama shule, michezo na elimu ya vyuo vikuu. Ndio maan Kikwete karudisha hati miliki kwa watu wenye vipaji vya sanaa mbalimbali ikiwemo muziki. Hakuna mwanamuziki ambaye muziki wake ukavuma sana na akaja kufa masikini katika kipindi cha Kikwete. Tazama mwenyewe jinsi kina marijani rajabu walivyokufa masikini. Tazamane jinsi mwanamuziki Ahmadi kipande alivyozikwa kimasikini. Ilifikia mahala mpaka majirani ilibidi wachangie sanda na uji wakati wa mazishi ya ahmadi kipande.

Hii yote ni kwa sababu ya kuwanyima wanamuziki haki zao za kutajirika katika miaka hiyo ya zamani na muziki wao. Nenda zaire, senegal, Nigeria, Ghana na Cameroon, ona wanamuziki wa nchi hizo walivyo matajiri.

Sasa Kikwete kawarudishi haki zao za kuwa na hati miliki na matokeo yake wanaopiga Bongo flavor huja mpaka marekani kutanua.

Tazama katika soka alipotuletea kocha kutoka Brazil kuja kuinua kiwango chetu cha soka mpaka tukacheza Fainali za CHAN kule Ivory Cost. Ona sasa vijana wetu wapo katika ajira nzuri za kimataifa. Nizar Khalfan, Henry Giusepe, Na mbwana mataka. Wachezaji mpira wa yanga na simba, wanamuziki, wasanii wakuigiza sinema, hawakai vyumba sita kabisaa bali wanajenga majumba yao ya kisasa na kumiliki magari.

Bado sijakutajia, Haki za wafanyakazi chini ya TUCTA na jinsi migomo ya wafanyakazi ilivyowanyima raha waajiri mbalimbali nchini chini ya Utawala wa JMK. Wapi uliona wafanyakazi wanaodai haki zao na kupata kama ilivyo kwa uawala wa JMK? hili nalo humsifii tuu! Miaka ya nyuma uliona hilo?

Yanga na simba kutoa ajira za kitaifa mpaka za kimataifa! wewe huoni kama hayo ni malezi mazuri ya Jakaya K? Yaani ni watu wa mboga saba mezani. wewe huoni katika miaka hamsini ya uhuru kikwete kawagomboa sana wanyonge kama hao ambapo wenzao wa zamani waliokuwa kama wao waliishia kuwa masikini. wewe kama haya unaona hayana maana , basi hutampenda raisi yeyote atakaye tawala Tanzania.
 
Back
Top Bottom