Hivi jimbo la Ukonga kuna mbunge na madiwani kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi jimbo la Ukonga kuna mbunge na madiwani kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bakuza, May 18, 2012.

 1. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi ila majibu sipati kuhusiana na kuzorota kwa maendeleo ya jimbo la ukonga lenye jumla ya kata 8 na viongozi wa kuchaguliwa yaani mbunge wetu Mh. Eugene Mwaiposa [/FONT][FONT=&quot]ambaye amekuwa kama mbunge wa viti maalum na si wa jimbo pamoja na madiwani akiwamo mstahiki Meya Wa manispaaya Ilala Mh.Jerry Slaa asiye na manufaa kwa kata yake ya Ukonga na hata kata jirani na hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kipindi chote cha uongozi wao tangia waingie madarakani sijaona mimi kama kuna jambo lolote la maana na la kimaendeleo walilolifanya zaidi ya kuendelea kufisadi pesa za walala hoi kwa kulipana na kula bila hata kufanya kazi(mfano:pesa ya mradi wa maji ,uzoaji wa taka,kusainiwa document pale ktk ofisi za kata,…nk).Tangia waingie madarakani kero zilizokuwepona ambazo hazijawahi pata ufumbuzi zaidi zaidi zinazidi kuwa kubwa ni kama ifuatavyo:-[/FONT]
  [FONT=&quot]1.Barabara[/FONT]
  [FONT=&quot]Barabara kutoka Mombasa kupitia Mazizini hadi Mkolemba[/FONT][FONT=&quot] kwenda mpaka Kivule ambayo imekuwa kero kupita kiasi na kulazimisha watu kutembea kwa miguu kiasi cha kilometa zaidi ya 10 asubuhi na jioni wanapoenda na kurudi toka kujitafutia riziki na wakibahatika kupata gari basi nauli huwa mara dufu.Japokuwa barabara hii Rais Kikwete alihaidi kuwa itajengwa kwa kiwango cha lami ndani ya siku 100 tangia siku aliyoingia madarakani.Hii iliwapa moyo wananchi na wakajua kuwa karibia nao wanaishi maisha kama ya wenzao wa sehemu mbali mbali za jiji hili na hivyo kujikuta wanasahau ulaghai wa CCM na kuwachagua wao kuanzia kiongozi wa chini kabisa hadi mbunge.Cha kushangaza sasa ni miaka imepita hakuna matengenezo kinachoonekana ni porojo huku tatizo likizidi kuwa kubwa na raia kupata mateso makubwa.Hii inashangaza maana Taarifa za kuaminika kwa kusikiliza bunge na kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ni kuwa pesa ya barabara hii zilishatengwa lakini sababu za kutojenga hazina mashiko kwa mtu mwenye akili timamu.[/FONT][FONT=&quot]Ukosefu wa mifereji ya kupitisha maji machafu kwa machinjio ya ng’ombe Mazizini hivyo kupelekea harufu mbaya kwa wakazi wa eneo hilo.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]b)Barabara ya kutoke Banana kwenda Kivule,Nyangandu na Nyantila,….nk nazo ni kero kubwa hasa katika kipindi cha mvua kama hiki ambapo magari huadimika na machache yaliyopo nauli huwa za juu sana[/FONT]
  [FONT=&quot]c)Barabara ya kuelekea Mongolandege [/FONT][FONT=&quot]kutoka Mombasa imekuwa ni tatizo kutokana na wakazi kutokuwa na njia ya kupita na kuwabidi kuzunguka sana wakati kuna nyumba chache tu kama tatu zinahitajika kuondolewa ili kupatikana njia hiyo[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]d)[/FONT][FONT=&quot] Barabara zilizopo katika mitaa ni mbovu hazipitiki kwa kipindi chote chamwaka. Vilevile Barabara ya Mazizini kuelekea Moshi Bar magari yamekuwa yakipaki hovyo bila taratibu husika[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]2.Maji[/FONT]
  [FONT=&quot]2.Maji katika jimbo hili ni tatizo kubwa pia maana hata visima vilivyo katika jimbo hili ni vichache na hili husababisha watu wengi kukosa maji safi na hivyo kutumia maji yasiyo safi na salama kwa afya yao.[/FONT][FONT=&quot] Kata ya Ukonga kumekuwa na kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi. Maji yaliyopo hayatoshelezi kutokana na upungufu wa visima virefu katika mitaa na visima hivyo vilivyopo katika mitaa vimekufa [/FONT][FONT=&quot]Hii ilipelekea wakazi wa ukonga kuchangishwa pesa na diwani wao Mstahiki Meya wa manispaa ya ilala Jerry Slaa kwa ajiri ya Mradi wa maji wa Ukonga Mzambarauni,kila kaya ilichangia kiasi cha Tsh.5000/= lakini pesa hiyo iliishia matumboni mwa diwani huyo mndokozi na washirika wake.[/FONT]
  [FONT=&quot]3. Zahanati/matibabu[/FONT]
  [FONT=&quot]4.Sehemu ya kupaki magari pale mombasa yatokayo kwa mkolemba,moshi bar na kwa diwani haipo na hili huchangia kuwepo kwa foleni zisizo za lazima pale Mombasa.[/FONT][FONT=&quot] USHAURI:[/FONT][FONT=&quot] Mabasi yote yatokayo Mkolemba/Diwani yageuzie soko la Ubena ili kutatua kero hiyo[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]5.Hakuna masoko la kuwahudumia wakazi ktk maeneo yao.[/FONT]
  [FONT=&quot]6.Hakuna viwanja vya michezo na maeneo ya wazi kwa ajiri ya matumizi mbalimbali kama viwanja vya michezo kwa watoto na ujenzi wa hospitari na huduma nyingine za jamii.[/FONT]
  [FONT=&quot]7.[/FONT][FONT=&quot].[/FONT][FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]Shule za msingi zilizopo katika jimbo la Ukonga hazikidhi mahitaji hivyo kupelekea shule kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi,kutokana na kuwa na kasi kubwa ya wanaohamia huku sababu eneo kubwa ni makazi mapya. Vilevile ukosefu wa madawati katika Shule za Msingi pamoja na matundu ya vyoo umekuwa ni tatizo katika Shule zetu za Msingi.[/FONT]
  [FONT=&quot]8.[/FONT][FONT=&quot]Wafanyabiashara kandokando ya Barabara ya Pugu (Road Reserve). wafanyabiashara hao waondolewe na kupewa eneo maalumu ili kuacha eneo la barabara wazi kwani wamekuwa wakiondolewa bila kupewa eneo mbadala na hivyo kurudi tena na kuwa tatizo sugu katika eneo hilo.[/FONT]
  Shime wananchi wa jimbo la ukonga unganeni na kuwawajibisha viongozi hawa walio mzigo kwetu kwa zaidi miaka nenda rudi na kuweka viongozi makini tutakao shirikiana nao kuleta maendeleo.
   
 2. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwani na Ukonga kuna Mbunge, maana huyu Mama yeye ni misele tu na wala hata anaogopa kuonana na wapiga kura wake. Maeneo ya Mwanagati tunafikiria kujitenga ili tujitangaze yatima wasio na mwakilish maana wakati huu sisi tumekuwa kisiwani na Dar.
  Kamwe Mbunge huyu asijaribu kufikiria kuomba kugombea ubunge tena maana cha moto tumekipata na tunaendelea kukupata ktk swala la usafiri mbovu usababishwao na barabara mbovu za ng'ombe tunasema.
  Siyo siri anachokifanya huyu mbunge anajua fika kuwa hajatutendea haki. Huyu ni mbuge wa viti maalum maana ni mbuge Bubu anaogomba hata kuombe fedha za maendeleo jimboni mwake.
  Tunamwomba aendelee kukaa kimya maana sisi huku tumeshajipanga kujiongoza kibubu bubu. Tutajipanga kuleta hata maroli ya kifusi kuziba makorongo haya lakini hatutegemei kumwalika kwenye Harambee yetu hii. Kwa kheri Mbuge bubu kwa kheri CCM.
  2015 siyo mbali tutajua style ya kunyoa maana hii ya kunyoa kifisadi tumechokana nayo.. Tumeamua kuvua Gamba na miyoni mwetu tumeshavaa Gwanda.
   
 3. D

  Dina JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Bakuza umeyasema yote yafaayo kusemwa kwa mtu mwenye hasira lakini anayeweza kuizuia hasira yake. Manake kwa mtu anayetawaliwa na hasira, huu ujumbe ungekuja kivingine kabisa ukiwa umesheheni maneno makali ambayo hata wahusika wangebaki vinywa wazi.

  Hivi barabara ya Ukonga Mombasa kweli inastahili kuitwa barabara jamani? Nauli ya kutoka Moshi bar - Mombasa ni shs 1,000 katika kipindi hiki ambacho mvua zimezidi kuivuruga hiyo barabara. Sasa kweli si kuongezeana mzigo wa maisha tena hapa? Yaani hao madiwani wangekuwa hata creative ku-mobilise kampeni ya nyumba kwa nyumba angalau kiwekwe kifusi cha mana na mitaro ya maji, si tungewaona wa maana jamani....

  Ama wananichosha....
   
 4. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bakuza

  CCM
  Kwa kweli sisi wananchi wa Ukonga tunasikitisha sana, huyu Mama Mwaiposya nilibahatika kumwona ktk kampeni mwaka 2010, hajui kujenga hoja hata moja, kiufupi ni bonge la kilaza, nikajiuliza mwenyewe hata ktk hizo kura za maoni za ccm kapita vp? nina uhakika hata hafahamu yeye kama mbunge wajibu wake ni nini?

  CHADEMA
  kwa upande wa CDM ambacho chama changu nacho nilibahatka kumsikiliza mgombea wa ubunge mzee Binagi wakati wa uchaguzi mwaka 2010, huyu mzee naye hajui hata kujenga hoja, anaongea papara tu hakuna anachokisimamia, Dr Slaa alikuja kuomba kura na kunadi wagombea wa CDM ktk kampeni uwanja wa kampala gongo la mboto.
  Siku iyo ndiyo ilikua mara yangu ya kwanza kumsikiliza Dr akiongea uso kwa uso, kabla ya hapo nilikua nikimuona ktk TV tu, Dr akampa mic mgombea ubunge wa CDM mzee BInagi akamwambia, "nakupa dakka 1 nikuone uwezo wako wa kujenga hoja na kama haujui nitakuazibu", mzee Binagi akachukua mic akatueleza wananchi kwamba tukimchagua yeye tutakuwa tumepata waziri kwa sababu Dr lazma amchague ktk baraza lake la mawaziri, alivyomalza akarudsha mic kwa Dr.

  uwezi amini Dr akamchana pale pale kwamba hajui na hana uwezo wa kujenga hoja kwa mtihani aliompa ka fail, Dr akaendelea kuzungumza yeye hatokua Raisi wa kujuana juana na kupeana uwaziri kama Binagi anavyosema, uwaziri na vyeo avipewani kw misingi hiyo, kwa kweli tokea siku iyo namkubali sana Dr Slaa, ni mtu muwazi na hana unafiki, kama una uwezo anakuchana LIVE hata kama ni mgombea wa chama chake, kwa kweli tunaitaji viongozi aina ya Dr, Dr alishangiliwa sana na wananchi.

  Mytake: uchaguzi ujao CDM tucmamishe mtu mwenye uwezo na anayekubalika.

  UKONGA HATUNA MBUNGE
  ni mimi mkazi wa Ukonga.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Wakichangisha si watakula tena ndugu yangu,ama hujui kuwa huyu Diwani wa ukonga na ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa alishachangisha Tsh.5000/= kwa kila nyumba kwa ajiri ya Mradi wa maji na akaila yeye na wapambe wake?Cha kushangaza na watu wa eneo hilo wamekaa kimya siku zote.Hawa ni wezi na wanyan'ganyi hawafai hata kwa dawa.Let them goooooo.
   
 6. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Una kumbukumbu sana ndugu yaani siku hiyo nilikuwepo uwanjani pale.Huu ni wakati wa kujipanga na keleta watu makini.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mbunge wa ukonga alafu anaishi mbezi/mikocheni/masaki mnafikiri mtakua mnamuona huko jimboni......
   
 8. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2014
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  UKONGA HAKUNA MBUNGE WALA DIWANI, wote ni wakimbizi
   
 9. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2014
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jimbo la Ukonga ni kati ya majimbo ambayo CCM ina hali ngumu sana na hii ni kutokana na maendeleo duni katika jimbo hilo. Mbunge wa Jimbo hili Eugene Mwaiposa ni kati ya wabunge ambao hawaongei chochote cha kupigania Jimbo lake. Ni mbunge ambaye ameshindwa kufanya mkutano wowote wa hadhara Jimboni kwake kwa aibu ya kuzomewa na kushindwa kujibu kero za wananchi.
  Jimbo la Ukonga barabara zake asilimia 90% ni mbovu na hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.Kutokana na ubovu wa barabara hizo kipindi cha mvua wananchi wanatozwa mpaka shilingi 1000/- kutoka kituo kimoja hadi kingine. Hali hiyo imekuwa ni kicheko na mbeleko kubwa kwa chama cha CHADEMA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. k

  kabalizuka Member

  #10
  May 27, 2014
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Habari zenu wakuu,napenda kuungana nanyi kuongelea masahibu yanayotupata wakazi wa jimbo la ukonga,Mimi ni mmojawapo wa wakazi wa jimbo hili na ambaye nimekuwa nikiumizwa na maendeleo duni ya jimbo letu.
  Barabara!
  Hali ya barabara za jimbo letu ni mbaya sana,barabara toka mombasa kwenda kivule kupitia kwa mkoremba haifai kabisa,pia toka banana kwenda kivule au benana kwenda mwanagati hazifai kabisa,hizo ni chache tu kati ya barabara za jimbo hili,barabara zina mashimo utafikiri mahandaki yaliyokuwa yakichimbwa enzi za vita ya kagera kwa ajili ya kujificha,kipindi hiki cha mvua barabara zinajaa maji mpaka kupita na gari unaanza kujishauri,spea za magari tunanunua karibu kila wiki hasa stabilizer linki.Ukiendesha gari katika barabara hizi kipande cha dakika tano hadi sita wewe utatumia nusu saa kwa gari na ukifika kama ni nyumbani mwili wote unauma hata hamu ya kukutana kinyumba na mwenzio wa ndoa unakuwa huna,nimekuwa nikijiuliza kuhusu aina ya viongozi tulionao,nafikiri uelewa wao wa kujenga hoja ni mdogo sana na hii yote inatokana na watu kufuata mkumbo wa kuchagua vyama badala ya mtu wa kujenga hoja mpate maendeleo,kwa kweli jimbo hili hatuna viongozi kabisa,kuanzia diwani,mbunge mpaka meya wa manispaa ambaye pia anatoka katika jimbo hilihili.
  Fidia 1!
  Kuna watu ambao wanatakiwa kulipwa fidia kupisha njia ya umeme toka kilwa hadi dar bado hawajalipwa fidia zao toka mwaka 2010 hadi leo hii,tumekuwa tukishuhudia ubabaishaji tu ukifanyika katika mradi huu toka kipindi hicho,watu wanapita kufanya valuation mali za wahusika inapita zaidi ya miezi sita bila taarifa yoyote wakati huo watu mnashindwa kufanya maendeleo kwa kuogopa kupata hasara zaidi matokeo yake wahuka wa mradi wanakaa kimya na hamna cha mbunge wetu kufatilia zaidi ya porojo anazopita na kuwapa wananchi wake,akionekana kwenye vyombo vya habari ndo anajua kafanya kazi kumbe watu tunamwangalia tu,ajue siku zinazidi kuhesabika.
  Fidia 2
  Kuna mradi mwingine wa upanuzi wa barabara toka mombasa mpaka kivule ikielekea bandarini,huu nao umebaki kuwa wa kufikirika,alama katika nyumba za watu zimewekwa zaidi ya miezi nane sasa lakini hakuna lolote linaloendelea na watu wamesimamisha maendeleo,tunaye mbunge,madiwani na meya ambao wote wako kimya kuhusu hili pia,hizo ni baadhi tu ya kero katika jimbo hili bila kutaja zote.
  Mimi kwa kuona kwangu nafikiri viongozi wa aina hii hawatufai kabisa,ni bora tujipange hasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu tuanze kuwashikisha adabu.
   
 11. PAPAA JIWE

  PAPAA JIWE JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2014
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 801
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi ninachojua ni kwamba mbunge wa ukonga alikuwa ni mmoja kati ya abiria waliokuwa kwenye ile ndege ya malaysia iliyopotelea baharini.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2014
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Naona watu wa Ukonga mmeamua kufunguka....... Mwita Maranya jimbo lipo harijojo hili...... wapi bwana Kabati........ Ukonga chukueni maamuzi magumu 2015
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. p

  pilipili kichaa JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2014
  Joined: Sep 3, 2013
  Messages: 6,275
  Likes Received: 2,236
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli mama aliyeko kwa sasa anapigania sana hilo Jimbo tena kwa Nguvu sana, nafikiri na yeye akifunguka mtaona namna ambavyo amefanya makubwa.

  Msemeni pia kwa mazuri mengi aliyoyafanya ktk jimbo la Ukongo wana JF
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2014
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu MTAZAMO, bakuza, Godlisten Masawe na wakazi wengine wa Ukonga.

  Tuache sasa kulalamika kwakuwa hakuna kitakachobadilika. Tuunganishe nguvu wanamageuzi wote pamoja na wapenda maendeleo wote ili tuhakikishe kwamba come 2015 tunawaweka benchi mbunge na madiwani wote wa ccm.
  Matatizo ya ubovu ama ukosefu wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, masoko na huduma nyingine za kijamii katika jimbo letu ni makubwa sana. Ukienda kata za Pugu, Chanika, Msongola na Majohe kote huko hali ni mbaya sana.

  Uongozi wa Chadema Jimbo la Ukonga kwasasa tunachokifanya ni kukiimarisha chama kwa kukijenga kuanzia ngazi za grass roots (CHADEMA NI MSINGI). Tunatengeneza misingi ambayo inatakiwa kuwa na wanachama angalau 30 ili hao ndio watakaotusaidia kuratibu shughuli za ukuaji na uimarishaji wa chama kwa wananchi katika ngazi za kaya/familia, na katika ngazi za misingi ndipo tutapata kutengeneza strong base ya wanachama na supporters.

  Rai yangu kwenu ni kuunganisha nguvu na Chadema ili tuweze kusaidiana kuweka mikakati imara na kabambe kuhakikisha kwamba kwanza wananchi wanaelimishwa ili waweze kubaini hila na udanganyifu wa ccm na hatimaye waweze kufanya chaguo sahihi kwa maendeleo yao kwa kutuchagua Chadema 2015 tuwatumikie.

  Tunao wanachama wengi wenye nguvu, nia na uwezo wa kuwatumikia kwa dhati wananchi wa Ukonga na kuliletea jimbo maendeleo na wananchi wakaondokana na hadaa za ccm ambazo wananchi wamesubiri utekelezaji wake miaka zaidi ya miongo mitano.

  Nakubaliana na wadau wa Ukonga ambao kwa kubaini hila na uwezo mdogo sana wa mbunge wetu wameamua kuja na slogani kwamba "UKONGA HATUNA MBUNGE".
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2014
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Hebu kuwa mfano kwa kuanza kutiririsha hayo mzuri.......kula lunch na yatima?
   
 16. PAPAA JIWE

  PAPAA JIWE JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2014
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 801
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sisi tunazungumzia Jimbo la Ukonga, hilo jimbo la Ukongo unalijua wewe sisi hatulijui. Usipende kuzungumzia mada ambazo huzijui maana utaanika halmashauri ya kichwa chako.
   
 17. n

  newazz JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2014
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Hoja zilizojaa hapa ni ondoa mbunge wa CCM, weka mbunge mwingine labda CDM au chama chochote.

  Lakini hakuna anayeanisha kwamba, kutokana na vyanzo kadhaa wa kadhaa vingeweza kujenga hizo barabara.

  Je huyo mbunge mpya au yeyote akija atajenga barabara kwa kutumia mafungu gani.

  Habari nyingi zilizoandikwa ni za jumla jumla tu.

  Watu hawafuatilii masuala ya msingi, lakini ni wepesi kutoa lawama ambazo haziendi kutibu tatizo la msingi, bali ushabiki wa kivyama pasipo kuleta suluhisho la kweli kwa wanachi.

  Ok, kama watu wangekuwa wanataka kujua ukweli, basi wangeenda kwenye kiini cha tatizo.
  Kiini cha tatizo kiko wapi?

  Ni mfumo wa kiutawala Tanzania.

  Mfumo wa kiutawala, kuna serikali ya Jamhuri ( au serikali kuu) halafu kuna serikali za mitaa ( ambazo ndio kuna halmashauri, jiji, nk nk.)

  Serikali kuu imekumbatia madaraka yote na haitoi madaraka yoyote kwa serikali za mitaaa ambazo ndio zipo karibu na wananchi kutatua matatizo yanayojitokeza.

  Hebu mfano kama hili la barabara zinazolalamikiwa za Ukonga au hata pengine maeneo mengine. Je serikali za mitaa wametenga hela zozote kwa barabara hizo?

  Barabara mfano za Kutoka Ukonga Mombasa kwenda Mazizi, Kwa Mkolemba au Barabara za Kivule,Nyantira, Nyangandu, Mwanagati nk.

  Je halmashauri ya wilaya ya Ilala inazo pesa za kujenga barabara hizo. Wengi watasema pesa zipo! Je hizo pesa ni kutoka kwenye vyanzo gani vya mapato?

  Vyanzo vya mapato ya serikali za mitaa ni kidogo na mara nyingi zinaporwa na serikali kuu.

  Ninapoongelea mfumo , namaanisha mfumo wa kiutawala ni mbovu , ambao unasababisha yeyote atakayekuja kwenye madaraka wa chama chochote, hatawajibika bali atafanyafanya anachoweza na kuchukua posho kama wanavyolalamikiwa hawa madiwani na wabunge.

  Mfumotunamaanisha katiba ya Nchi, hii ndio tatizo kubwa kwani inatengeneza mazingiraya viongozi wasiowajibikia kukaa madarakani bila kufanya cha maana.

  Haya tazama mfumo kwenye serikali za mitaa. Kila serikali za mitaa anachaguliwa kiongozi na wasaidizi wake, ambao hawawajibiki kwa wananchi mojamoja. Nani anaweza kwenda pale serikali za mtaa kuhoji mapato yaliyokusanywa kwenye mtaa wake?

  Kwa mfumo uliopo ambao unatakiwa ubadilishwe kwa kupitia katiba yenye manufaa kwa wananchi, ndio inaweza kuwa suluhisho la viongozi uchwara na serikali uchwara zisizowajibika.

  Nakubali CDM walikuja na sera za majimbo. Watu wengi hawajazielewa, kuwa ingekuwa ni mfumo mbadala mzuri katika uendeshaji wa serikali za mitaa. Nyerere kwa kujua nguvu ya serikali za mitaa ( serikali za watu) alizipiga marufuku mwaka 1972 na kuua utawala wa wananchi ambao ndio walikuwa na uchungu na maendeleo yasehemu zao. Serikali hizi mfano Bukoba, Mbeya, Moshi nk walikuwa na uwezo wa kukusanya kodi katika maeneo yao kwa maendeleo yao wenyewe.

  Hata mfumo wa ukusanyaji kodi kupitia serikali kuu ni mfumo ambao hauwezi kufanyakazi kwa ufanisi katika kukusanya kodi.Kwani bado mfumo mbovu, unaruhusu ulaji rushwa kuanzia ngazi za juu hadi chini.

  Suluhisho liko wapi? Suluhisho ni kwa umoja wetu wananchi wote Tanzania kupigania katiba ya wananchi, ambayo italeta kuwapa madaraka wananchi kuiwajibisha serikali kupitia taratibu za kikatiba na majukwaa mengine ya haki kwa raia.

  Wananchi wengi wa Tanzania hawajawa tayari kusimamia kupatikana kwa katiba mpya , yenye kuwapa wananchi nguvu angalau ya kukataa mambo yasiyo sawa yasiendelee kwenye maeneo yao ya makazi au kiutawala.

  CDM waliposema juu ya serikali za majimbo walikuwa wanamaanisha kwamba, madaraka yarudishwe kwa wananchi katika maeneo yao. Kwa mfumo wa sasa hata zingekusanywa shillingi ngapi kutoka eneo fulani, eneo hilo halipati faida ya moja kwa moja kutokana ya kuwa wamiliki wa chanzo hicho cha mapato. Hata ukiangalia katika halmashauri za wilaya au majiji kwa sasa, maeneo husika yenye vyanzo vyamapato hawafaidiki moja moja. Bali mapato huchanganywa katika kapu la wote halafu linawekwa kwa walafi wachache kugawana. Nani anaweza kuwasimamia hawa na kuwawajibisha hawa viongozi? Hata akija kiongozi wa chama chochote atatumia mianya hiyo hiyo kujinufaisha.

  Utakapokuwa na katiba imara na yenye muelekeo wa kuleta madaraka kwa wananchi, basi wananchi angalau wanakuwa na nguvu za kitaasisi au mfumo kuondoa uozo katika mifumo ya kiutawala.

  Tunahitaji mahakama huru, vyombo mbalimbali huru ambavyo vitapewa uhuru huo kwa kupitia katiba mpya ya wananchi.

  Tunachotakiwa kubadilisha ni mfumo, la sivyo tutabadilisha vazi lakini mvaaji ni yule yule.

  Wananchi tunatakiwa tujishirikishe na mambo ya maendeleo ya mitaa na utawala ya maeneoyetu kwa kuanzia huko tunaweza kubadilisha angalau mambo anuani , endapo wananchi tutaanza kuwafuatilia viongozi na kuhudhuria mikutano au kudai mikutano ambapo , wananchi wanaweza kuwaonyesha hawa viongozi kuwa , tunatambua udhaifu uliopo na hatupo tayari kuendelea kukumbatia udhaifu
   
 18. singsong

  singsong Member

  #18
  May 27, 2014
  Joined: May 7, 2014
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimeshawagundua mnalitaka hilo jimbo ubovu barabara ni swala la dsm nzima hivi mmekwenda posta , kariakoo barabara ya uhuru haipitiki. Mbona hiyo mama tunamwana kwenye magszeti, bungeni, kwny mikutano ninyi mnakaa wapi au ni like kabila lisiloongozwa na wanachama ua mnalo lenu jambo. Nakuambia mama huyu ni Mchapa kazi na lazima tutamrudisha. Acheni unafiki na mjiandaa kama mnalitaka jambo let u hatukupi
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2014
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mbunge wenu yuko busy italian house wanamshika shika mbupu na akina mere na zai
   
 20. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2014
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mlichagua hovyo, sasa mnalalamika hovyo
   
Loading...