hivi jikoni hausikii maneno mengine zaidi ya jina??!!

stevoh

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
2,921
1,104
Bakari ni house boy mara nyingi
huiba wine ya boss wake na kisha
kuongeza maji kwenye chupa ili
boss asigundue.
Mara kadhaa boss
alihisi ladha tofauti anapokunywa
wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.

Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua
wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia
mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari
maswali. Siku hiyo Bakari alikua
jikoni, boss na mkewe walikua
sebuleni.

Boss:Bakariiii!

Bakari:Naam baba!

Boss:nani anakunywa wine
yangu?

Bakari kimyaaaa hajibu kitu!

Boss:Bakariiiii!

Bakari:naam baba!

Boss:nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!

Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko
jikoni.

Boss: Kwanini nikikuita unaitikia,
nikikuuliza unanyamaza?

Bakari:baba huku jikoni ndo
kulivyo, unasikia jina tu likiitwa
lakini maneno mengine husikii, na
kama huamini baki jikoni mi
niende
sebuleni. Bakari akaenda sebuleni akaanza
kuita.

Bakari:Babaa!

Boss: naam Bakari!

Bakari:Saa sita usiku huwa
unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss kimyaaaa!

Bakari:Baba babaa!

Boss:ndio Bakari!

Bakari:Nauliza hivii, chumbani kwa
house girl saa sita za usiku hua wafuata nini?

Boss kimyaaaaaaa!

Boss akatoka nje:

Bakari huku
jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya
jina! Dah!
..from masanja
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom