Hivi JF kama Taasisi, Hatuwezi kuwa na maoni ya pamoja kuhusu Katiba Mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi JF kama Taasisi, Hatuwezi kuwa na maoni ya pamoja kuhusu Katiba Mpya?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by STK ONE, Aug 6, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana Jamvi ni maoni yangu tu, hivi hatuwezi kuwa na maoni ya pamoja juu ya katiba mpya? Maoni hayo tunakuwa tunayawakilisha kwenye tume sehemu mbali mbali punde inapofika. Hii itapelekea maoni yetu kufikiriwa na kuwekwa kwenye katiba mpya. Ni maoni tu, kama inawezekana, tuna wanasheria wengi sana humu tuchangie na watuandikie conclusion ya maoni yetu. Asanteni. Nawaomba tusilete U CCM na U CDM katika hili, TANZANIA NI YETU SOTE.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  "Maoni ya pamoja" ni tofauti na spirit ya uhuru wa maoni.

  Tuko watu tofauti sana kuweza kuwa na "maoni ya pamoja".
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  mbona umeanza kujistukia mkuu,we ni gamba? Livue kwanza kama bado kaka...
   
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi sina mengi ya kusema, soma signature yangu chini...lakini Katiba ni ya nchi, na ni vyema kwenye jambo ambalo linahusu nchi, tusiweke itikadi za vyama vyetu vya siasa.
   
 5. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafahamu our differences, but yet as Tanzanians, we can have common ideas on what we ought our country to be in the near future. THis is only possible if we have common ideas for common good. Tofauti zetu hazituzuii sisi kuwa na maoni ya pamoja juu ya katiba mpya. Tukiweka itikadi za vyama vyetu vya siasa kando, tunaweza kuwa na maoni ya pamoja juu ya katiba mpya as GREAT THINKERS.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  The very idea that a membership as diverse as this forum has must somehow have common ideas is what made us to wallow in poverty for so long.

  We had the so called "common idea", it was called "Ujamaa and Kujitegemea" under CCM. It failed.

  Now let's embrace a little diversity.

  Should a commonality emerge naturally, that will be welcome news.

  But please do not try to herd a population with such divergent views as JF to converge on "common ideas" by design.

  It is the height of thought control, which is totally against the spirit of freedom embraced by JF.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,137
  Trophy Points: 280
  Si wazo baya kwamba WanaJF wakusanye mapendekezo ya nini kinachostahili kuwemo kwenye katiba mpya toka kwa wadau mbali mbali kisha mapendekezo hayo kuwakilishwa katika hiyo tume ya kukusanya maoni. Tunaweza kusema mapendekezo hayo yakusanywe kwa muda wa miezi miwili/mitatu.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Huyu anataka "maoni ya pamoja" kama JF.

  Last time I checked JF si chama cha siasa, sasa maoni ya pamoja tutayatoa kwa itikadi gani ya pamoja tuliyo nayo?

  Kama issue ni kukusanya maoni JF ndiyo kazi yake kila siku.

  Angalizo liko hapo "ya pamoja". Maana watu wasije kuwa na maoni yao wanataka kutumia jina la JF, wanaungunga support ya wawili watatu, halafu wanasema "maoni ya pamoja ya JF ni haya".

  Weka maoni kwanza, halafu watu watajadili watajua haya ni ya pamoja au la.

  Ukishaanza kuwapelekapeleka watu kwenye "maoni ya pamoja" kabla hata maoni yenyewe hayajajulikana utakuwa unaenda kinyumenyume huku unaangalia mbele, hukawii kugonga.
   
Loading...