Hivi JF hakunaga wachawi wa kutoa mbinu bora za kukabiliana na kuishi na jamii za kichawi?

Nina swali naongezea kuwa tunaambiwa uchawi unarithishwa je unarithishwa vip na anaerithishwa anajuaje kama tayari ana vitu na je anaupenda au haupendi je anaweza kuukataa au uchawi una utamu wake ukirithishwa tu huwezi kuuacha kwa hiyo ina maana mchawi anaweza tu kujistukia ni mchawi bila kupenda!!!?
 
Nina swali naongezea kuwa tunaambiwa uchawi unarithishwa je unarithishwa vip na anaerithishwa anajuaje kama tayari ana vitu na je anaupenda au haupendi je anaweza kuukataa au uchawi una utamu wake ukirithishwa tu huwezi kuuacha kwa hiyo ina maana mchawi anaweza tu kujistukia ni mchawi bila kupenda!!!?
Watusaidie majibu
 
Uchawi na wachawi limekuwa ni tatizo kubwa katika jamii tangu kuwepo kwa Dunia. Watu wengi katika jamii wanapenda kujua mengi kuhusu uchawi maana kwa wengine ni jambo la kusadikika kutokana na usiri mkubwa juu ya uchawi na wachawi na mbinu zao, kusudio lao, kwamba uchawi ni dini, ushirika, Chama au ni muunganiko wa namna gani?

Hapa JF Kuna mada nyingi kuhusu watu wakieleza uzoefu wao juu ya mambo ya kichawi. Ni bahati mbaya zaidi sijawahi kuona hata mmoja akikiri kuwa yeye ni mchawi na akatuelimisha mengi kuhusu uchawi kama:-

1. Ni sababu gani inayoweza kufanya mtu ashambuliwe na wachawi au mchawi?

2. Kuna kinga yoyote ninayoweza kuchukua ili nisiadhibiwe na wachawi?

3. Uchawi ni zao la urithi, je wanaangalia sifa gani ya mtu wanaetaka kumrithisha katika familia?

4. Kuna uhusiano wa kirafiki au kiuadui kati ya wachawi na waganga wa jadi?

5. Ikiwa waganga wanatibu madhara ya uchawi ndio kusema waganga wa jadi wana maarifa zaidi ya wachawi?

Juu ya hayo ningeomba kwa faida ya wengi hapa JF kama sehemu ya kupata elimu ya jamii wajitokezee watu ambao ni wachawi bila hofu nikiamini vile wapo nyuma ya maandishi hawatapata athari zozote, kutusaidia kutoa elimu kubwa juu ya uchawi, wachawi, walengwa wa uchawi, waganga na Siri nyingine ambazo jamii ipo gizani juu ya uchawi.

Ahsanteni
Hapa JF Kuna mada nyingi kuhusu watu wakieleza uzoefu wao juu ya mambo ya kichawi. Ni bahati mbaya zaidi sijawahi kuona hata mmoja akikiri kuwa yeye ni mchawi na akatuelimisha mengi kuhusu uchawi kama:-

Mimi nadhani naweza kuwa ndio mwenye mada nyingi za uchawi kuliko mwingine yoyote hapa JF.. Sikubakisha kitu kwenye ushirikina .Naujua ndani nje kwa kuusomea na kuufanya lakini si kama mimi ni mchawi kamili.. Mimi nilichokuwa nafanya ni fantasy witchcraft

Uchawi ni imani ya siri yenye matendo kificho yasiyo ya uwazi, uchawi ni kaliba
Kongwe tangu kuumbwa kwa ulimwengu na uchawi ni sehemu ya uumbaji, yaani ni ukamilifu wa uwili kwenye mwanga na giza, uchawi ukiwa ni upande wa giza..!

Uchawi ni aina ya sayansi kinyume cha sayansi ithibati na formula, uchawi hupimwa kwa matokeo na si mchakato...kwa maana ya kwamba huwezi kuthibitisha uchawi kwa formula bali kwa matokeo
Uchawi ukiwa umewekwa kwenye ulimwengu wa kiroho wa giza ni kinyume cha ulimwengu wa roho wa mwanga kwahiyo kwa namna yoyote ile hauwezi kuwa na faida wala manufaa kwenye dunia ya macho ya nyama na mwanga
Uchawi upo kwa ajili ya kutesa, kuharibu kupotosha na kudanganya, kati ya yote haya je kuna lenye faida?? Jibu ni hapana

Zaidi uchawi ni tawi tu kwenye mti shina wa USHIRIKINA, Ushirikina ndio unabena uchawi, ulozi kuwanga na matendo yote yanayofanana na hayo!
Uchawi una madaraja na matabaka.. Kuna uchawi mwepesi ama rahisi na kuna uchawi mgumu ama mzito kuna uchawi kwa nia ya kujifurahisha lakini pia kuna uchawi wa kuumiza na kuharibu..!

Uchawi ni imani pia yenye mkuu na madhabahu zake nitakuwekea mada kadhaa ujifunze zaidi
 
Elimu zote zipo google kuhusu uchawi,codes zake,na Kinga zake,miiko na Kazi zake,kurogwa na kutorogeka,Elimu ni pana uchawi unajifunza unafundishwa vyuoni ukitaka na unahitimu kipo chuo Temeke kinafunza uchawi miaka 5 then uganga miaka 2.Ili uwe mganga ni lzm ujifunze uchawi.
Mchawi na mganga ni kampuni moja SAwa na coca na fanta maana wote boss wao ni mmoja anaewapa nguvu za kutenda.
Mchawi anaweza akamroga mganga na viceversa.Mchawi umuua mganga na mganga umuua mchawi hapa ni uwezo binafsi wa nguvu aliyonayo muhisika na nguvu hizi wanapewa na shetani kama asante ya kumfurahisha shetani ikiwemo ikiwemo kutoa watu kafara.
Kadri mchawi na mganga wanavyoua Sana na ndivyo vyeo vyao na nguvu zao uongezeka sana.
Mganga akimuua mganga mwenzake anapanda cheo.Mchawi akimuua mganga cheo kinapanda, mganga akimuua Mwenyekiti wa wachawi cheo kinapanda.
Mganga umroga mteja wake asiishiwe magonjwa Ili apige pesa.
Mganga akimuwekea kinga mtu aliyerogwa na wachawi au kujifanya kumtibu wachawi wanaungana kumuua mganga, mganga umuomba ruhusa au umpa pesa mchawi auondoe ugonjwa aliouweka kwa mtu waliyemroga na mchawi akiridhia uuondoa uchawi na mgonjwa huwa mzima.
 
Elimu zote zipo google kuhusu uchawi,codes zake,na u kipo chuo Temeke kinafunza uchawi miaka 5 then uganga miaka 2..
Mkuu ubarikiwe kwa haya madini hiki chuo minaitwaje na kipo Temeke sehemu gani?
 
Back
Top Bottom