Bwajilo
JF-Expert Member
- Dec 5, 2021
- 345
- 880
Uchawi na wachawi limekuwa ni tatizo kubwa katika jamii tangu kuwepo kwa Dunia. Watu wengi katika jamii wanapenda kujua mengi kuhusu uchawi maana kwa wengine ni jambo la kusadikika kutokana na usiri mkubwa juu ya uchawi na wachawi na mbinu zao, kusudio lao, kwamba uchawi ni dini, ushirika, Chama au ni muunganiko wa namna gani?
Hapa JF Kuna mada nyingi kuhusu watu wakieleza uzoefu wao juu ya mambo ya kichawi. Ni bahati mbaya zaidi sijawahi kuona hata mmoja akikiri kuwa yeye ni mchawi na akatuelimisha mengi kuhusu uchawi kama:-
1. Ni sababu gani inayoweza kufanya mtu ashambuliwe na wachawi au mchawi?
2. Kuna kinga yoyote ninayoweza kuchukua ili nisiadhibiwe na wachawi?
3. Uchawi ni zao la urithi, je wanaangalia sifa gani ya mtu wanaetaka kumrithisha katika familia?
4. Kuna uhusiano wa kirafiki au kiuadui kati ya wachawi na waganga wa jadi?
5. Ikiwa waganga wanatibu madhara ya uchawi ndio kusema waganga wa jadi wana maarifa zaidi ya wachawi?
Juu ya hayo ningeomba kwa faida ya wengi hapa JF kama sehemu ya kupata elimu ya jamii wajitokezee watu ambao ni wachawi bila hofu nikiamini vile wapo nyuma ya maandishi hawatapata athari zozote, kutusaidia kutoa elimu kubwa juu ya uchawi, wachawi, walengwa wa uchawi, waganga na Siri nyingine ambazo jamii ipo gizani juu ya uchawi.
Ahsanteni