Hivi je wazo kama hili ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi je wazo kama hili ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Jul 24, 2009.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Wataalmu wa mambo haya naomba kuwakilisha hoja.

  1.kurekebisha miundo mbinu ya bandari ya mtwara, Tanga na Dar es salaam. Harafu kwa bidhaa yoyote ambayo destination yake ni TZ haitozwi ushuru inakuwa huru na bure.

  2. tunajenga reli kutoka tanga hadi Musoma na tunajenga bandari kubwa Musoma, harafu reli tunaijenga kutoka msoma tunaunganisha Mwanza na upande wa pili wa mwanza tunajenga reli kuunganisha burundi na rwanda.

  3.Tunajenga reli ya kati hadi kigoma na pale kigoma tunajenga bandari nzuri.

  4. Tunajenga reli kutoka mtwara tunaunganisha msumbiji ,malawi na nchi mwa kusini huko.
  Harafu bidhaa yoyote destination yake ambayo iko nje ya Tanzania tunaitoza ushuru NUSU ya bei ya sasa, yani kama saizi tunaitoza bidhaa hiyo TSH 10 basi tutaitoza Tsh5.

  Swali hii soln itajenga nchi ama itabomoa kabisa uchumi wa nchi.?

  Mods naomba ibaki hapa kwa mda .
   
 2. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  1. Suggestion ya kwanza haifai hata kuifikiria achilia mbali kuifanya!!! Ikiwa hivyo awali ya yote TZ itakuwa ni nchi ya wachuuzi badala ya wazalishaji!!! Aidha, hata wafanyabiashara wa nje watatumia mwanya huo kwa kushirikiana na wa-tz wenzetu ili kupitishia bidhaa kwa kujifanya zinaishia tz na baadae kuvushwa nje kupitia njia za panya!! But all in all, mapato ya serikali ni kodi, na kv watu hawataona haja ya kuzalisha then serikali itapata wapi kodi wakati hata huku nako hamna kodi?

  2. Kujenga reli ya kati hadi Kigoma? Au unamaanisha kuiboresha?Reli ya kati ipo, na tatizo ni jingine kabisa, sio reli!!!
  3. Nazani unachojaribu kusema katika kupunguza ushuru kwa 50% ni ili uvutie mizigo mingi zaid kupitia kwenye bandari zetu!! Kama huduma ni bora basi hata kama utaongeza ushuru zaidi ya huu wa sasa bado watu watapitishia mizigo yao tz. Aidha, unapofikiria kupunguza hiyo 50% lazima uangalie utavutia wateja wangapi ambao si miongoni mwa wateja wako!!!
   
Loading...