Hivi Jamani Press Confrence Room Ya Taarifa za Serikali Na Ikulu Yetu Kwa Umma Ni Wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Jamani Press Confrence Room Ya Taarifa za Serikali Na Ikulu Yetu Kwa Umma Ni Wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Oct 23, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Jamani Kadri siku zinavyozidi kwenda siku hizi kumeanza kuwa na tabia ya Watendaji wa Serikali kuwa na Matamko Muhimu ya Serikali na hata Ya Ikulu Katika Mazingira Tata yasiyo kidhi hadhi ya Taariifa husika.Moja ya taarifa ambayo nitaitumia hapa ni hii ya Kifo cha Dikteta wa Taifa la Libya Gadhafi,Waziri wetu wa Mambo ya Nchi za Nje katoa eti taarifa yaani msimamo wa serikali kuhusiana na kifo cha dikteta huyo wa Taifa la Libya, ameitoa akiwa kasimama kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.

  Hakika taarifa hiyo ambayo inaonekana haikuwa na matayarisho yoyote manake kaongea kama mtu aliekuwa anatoa maoni binafsi na si waziri au kiongozi mwenye dhamana ya utoaji wa taarifa hiyo muhimu yenye kuonesha msimamo wa umma.

  Ukiona watoaji wa taarifa nyingi za Serikali za wenzetu kunakuwa na maeneo maalumu ya kutoa taarifa muhimu za Serikali na kuipa hadhi yake kwa mujibu wa taarifa husika.Kwa Watanzania siku hizi kiongozi anaweza kuwa kwenye harusi au kitchen party ya shoga yake toka uko vyombo vyetu vya habari umekaa kwenye runinga unasikia tamko la taarifa ya Serikali waziri au kiongozi anatoa tamko rasmi la Serikali pembeni yake ni chupa za bia na sahani za ubwabwa na sio kwenye kiambaza maalumu [podium] cha taarifa za Serikali kwa Umma.

  Wenzetu ama mataifa ya wenzetu wanavyo vyumba maalumu vya kutolea taarifa
  1: Taarifa za Ikulu
  2: Taarifa za Serikali
  3: Matamko au Kusanyiko la Jamii

  Nakumbuka nikiwa mdogo enzi hizo shule ya msingi kulikuwa na Radio moja RTD, kulikuwa na sauti ambazo ulikuwa ukiisikia tu kwenye taarifa ya habari basi watu wazima wanajua kuna tamko rasmi la Serikali sauti hiyo na nyinginezo ila nakumbuka mtu huyu DAVID WAKATI.Na hakika zama zile serikali ingekuwa na TV, nina hakika kukengekuwa na sehemu maalumu ambayo sio studio ambako waandishi wanakwenda kupokea taarifa za Serikali na matamko yake, na sehemu nyingine ni maalumu kwa hadhi ya taarifa ya za Ikulu kwa umma.

  Naomba wana JF mnisaidie kujua sehemu zinazotumiwa kutoa taarifa za Serikali na Ikulu ni wapi?
  Manake tukiwa na sehemu hizo zitawapa nafasi mawaziri na viongozi kutokwepa kujibu majibu ya taarifa muhimu au za Ikulu ama za Serikali zinazotaka majibu.Manake kama taarifa ya Membe kuhusu Gadhafi ni taarifa muhimu lakini ilivyotolewa na sehemu ilipotolewa du imekuwa bomu linalomtafuna polepole.

  Tunataka kuona vyumba maalumu vya hadhi ya Serikali na Ikulu na Matamko mengine ya Jamii,ili tunapoziona TV zetu kisha tukaona chumba [Press Conference Room] tunajua hii hapa leo ni taarifa ya Ikulu toka chumba maalum cha taarifa za ikulu kwa umma hata kama kitakuwa nje ya ikulu lakini kina hadhi ya ikulu ambacho daima chumba kinabaki intact na hadhi ileile. Kesho tukiona taarifa tena tunajua hii hapa ni taarifa ya Serikali toka nayo kwenye chumba cha Serikali, ama Mtondogoo tukiona tunajua hii ni taarifa ya wanajamii yoyote ile nao wanachumba kilichojengwa na Serikali kwa ajili ya Umma kutoa taarifa zake.

  WanaJF naomba kujua vyumba hivyo vipo au ndio hivi tunapewa taarifa zenye utata.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama ile iliyotolewa clouds na TBC ni taarifa ya serikali, sidhani.

  Kuna njia rasmi ya kutoa taarifa za serikali. Yale yalikuwa ni maoni yake binafsi ambayo kama raia mwingine yoyote anaweza kuyatoa mahali popote na saa yoyote kama ambavyo alikwisha sema hapo awali kuwa nchi haiwezi kuchukuliwa na wahuni wanaondesha Pick up etc
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwa maandishi then yanawekwa geti la kuingilia ikulu waandishi wanapitia pale au ni wapi ?Nijuzeni .
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndiio maana tunataka kujua manake naona wanakurupuka tu wako kwenye sherehe tunasikia hilo ndilo tamko la serikali.Tukijua kuwa zipo taarifa maalumu zipatikane huko na watoa taarifa wapate nafasi ya kujibu maswali ya wadu wa habari ili yakidhi taarifa zao.
   
Loading...