Hivi jamani kwenye kutafuta kazi ni kwel GPA inazingatiwa?

Wakuu nimemaliza bachelors degree kwa overall gpa ya 2.5,nltaka kujua je itaniathiri katika kupata ajira endapo ntahitaj kuajiriwa,maana kwa sasa nipo naendesha biashara yang kwanza
Mkuu swali ni je Kichwani mwako una GPA ya ngapi?Unaweza kuwa GPA ya 4. lakini ubongo ukawa na GPA 1. na ukawa na paper GPA ya 1. na ubongo ukawa na GPA ya 5.

Kitu cha muhimu unapoomba kazi hakikisha unatengenzea CV inayoshawishi,Unaandika barua inayoshawishi na kama ukiitwa kwa interview una hahakikisha Unajiuza kadiri au zaidi ya uwezo wako.Hata hvyo GPA nzuri inaweza ongeza uwezekano wa wewe kupata au kukosa kazi kwa kutegemea fani,kampuni etc.

Nakutakia kila heri ila kwa GPA yako ya 2.5 mimi naweza kukuajiri kama unaweza kunishawishi kwama utaweza ku add value kwenye biashara yangu.Next time uliza hili swali kabla ya kuhitimu na sio baada ya kuhitimu kwani unakuwa umechelewa
 
mkuu umemaliza na GPA ya afya tu sio yakujitesa kibigwa tu.
kubwa ukipata nafasi waonyeshe uweze kwenye content tu ya degree yako.
kuna watu wanayo kubwa ila ya rushwa ya ngono content zero.
work hard ukipata nafasi kila mtu ananafasi yake tu.
 
Baadhi ya sehemu -- nasikia -- wanazingatia GPA kwa kuhakikisha hawaajiri mwenye GPA fulani au ya kuizidi hiyo. ;)
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom