Hivi jamani, hamuoni aibu kila kitu ubalozi wa Marekani, kikitokea kitu mnakimbilia kusema tutashtaki Marekani? Ni ushamba

daza steven

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
359
357
Zamani wakati wa ujinga wengi tulikuwa hatujui kuhusu hiyo Marekani tulimezeshwa kila kitu cha upande 1 wa shilingi. lakini inatia aibu kijana ambaye wazazi wake wamempeleka shule lakini leo bado yupo katika zama za ujinga bado anaona kama Marekani ndiyo kimbilio wakati ni nchi hatari hasa kwa bara la Afrika, jamani tujikwamue kutoka utumwa wa kiakili

Mimi huko nyuma nilikuwa nikiamini kuwa Marekani ndiyo taifa ambalo linaongoza kwa kuwa na democrasia kubwa na pana kuliko nchi yoyote hile Duniani kumbe siyo, ukifika Amerika unaweza shangaa jinsi watu wanavyoishi kwa hofu na mashaka. Lakini likitokea jambo dogo tu hapa Bongo utasikia wanalikimbiza ubalozi wa Marekani hivi vijana mnakwama wapi? Mnalijua vizuri taifa hili?

Watu wamekuwa wakilalamikia polisi wa Tanzania kuwa hawatendi haki mimi sibishi, sasa nenda kaangalie polisi wa Marekani utarudi spidi mwenyewe bongo

Marekani ndiyo nchi pekee iliyobaki ambapo inawaumiza sana nduguzetu weusi kwa kuwabagua katika kila jambo si elimu, afya na haki zingine za mtu na utu lakini mimi nashangaaga kuona mtu anakimbilia kujisalimisha kwa Marekani ni dhambi inayokutosha kukufikisha motoni, Marekani inaua, inapiga, inafunga, inanyanyasa, inatesa, sheria kandamizi wenyewe mmeshuhudia maandamano makubwa ambayo hayajawai tokea Huko Marekani tangia kuanzishwa kwa taifa hilo kwa kuuliwa Geoge Floyd. Hari ni mbaya nduguzangu huko Marekani mnakoona kimbilio

Angalia Marekani ilichokifanya Libya hadi leo hakuna taifa kama lile la Gadafi ambalo alikuwa hata na ombaomba 1, elimu bure, maji bure, umeme bure, afya bure lakini Marekani kuna omba omba fatilieni mambo. Leo hii Libya haina uchumi, haina chakula cha kutosha, hakuna huduma nzuri za afya tena, miundombinu imebomolewa wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyochochewa na Marekani, Libya ni vita asubuhi mpaka asubuhi

Libya leo inatoa wakimbizi haya yote ni matokeo ya Marekani tena kwa kigezo cha kuwa eti Libya haikuwa na democrasia jamani tumswalie Mtume, huko marekani kuna democrasia? wana nchi wa Libya wanajuta mwaka jana walikuwa wanatimiza mika kama 8 hivi tangia kupinduliwa kwa gadafi wengi walikusanyika juu ya kaburi la Kanal Muhal Gadafi kuomba dua ya msamaha lakini majuto ni mjukuu.

Iraq leo hari ni mbaya kuliko wakati wowote hata juzi wananchi walipokuwa wanaambiwa kuwa kuna Korona hawakuiogopa kwani wao wanamajanga makubwa mara 10 ya Korona, haya yote yamesababiswa na Marekani. Baada ya Marekani kumuondoa Sadam Hussen leo hakuna ile Iraq ya Sadam ni vilio na kusaga meno kasome utaona mambo ya ajabu sana.

Nchi ya Liberia ambayo ni koloni la Marekani wamekuwa na hari mbaya tangia kurudishwa kwa manegro kutoka Marekani hari yao ni mbaya sana na hata leo nchi hiyo ambayo imepita katika vipindi vigumu vigumu ni chini maskini ya chini kutoka chini lakini bado ukiangalia bendera yao iko kopilaiti na ya Marekani. Ni taifa ambalo Marekani ilihakikisha inaligawa kwa maslai yake binafsi ndiyo maana katika Afrika Liberia ndiyo taifa linaloongoza kwa ukabila Afriaka na Duniani ni balaa nenda ukasome utaona vitu vya ajabu Marekani wamevijenga.

Tulishuhudia Geoge W Bush alipokuja Bongo alitoa zawadi ya vyandarua, Kweli. Yaani taifa kubwa kama hilo linatupa sisi vyandarua vya mbu wakati lilikuwa na uwezo wa kumdhibiti mbu kabla hajafika ndani, mbona Baba wa taifa Nyerere aliweza kudhibiti mbu, sisi tukiwa wadogo hakukuwa na vyandarua kama sasa nakumbuka kulikuwa na utaratibu wa kumwaga dawa katika manyumba yetu kila sehemu yenye maji maji kama choo, bafu, mitaro na kadhalika tena ilikuwa bure sasa Bush anatuletea chandarua chenye dawa, kumbe dawa ya kumuua mbu ipo ila yeye anachanganya hapo hapo, hiyo ndiyo Marekani mnayo itukuza.

Angalia jinsi walivyo mmisilidi Mzee Mkapa wakati wauongozi wake maana vuvuzela lilipigwa na nakumbuka wote tuliaminishwa kuwa huwezi kuwa na viwana au nchi ya viwanda kama unafuata siasa za ujamaa na kujitegemea au ukomunist. Hayo yalikuwa mafundisho kutoka Marekani na Mzee Mkapa akaingia mkenge bila kujua na zile kelele zilimchanganya akaviuza viwanda vyote na vikafa yaani ubinafsi-shaji hiyo ndiyo Marekani.

Kuwa na viwanda haijalishi uko katika mfumo gani wa siasa viwanda ni maisha na maisha ni viwanda, hata Adam na Eva Mungu alipowaacha katika busta ya Edeni walianzisha viwanda, hata kabla ya mwarabu au mzungu kuja Afriaka tayari tulikuwa na viwanda. Ndugu zangu wametudanganya vya kutosha, wametudharau vya kutosha na wameturudisha nyuma vya kutosha sasa tuanze kuachana na fikra za Marekani vijana tunapotea tutalipeleka wapi taifa hili.

Nampongea Dkt Magufuli hata kuwakatila njia wanazotumia wazungu kupambana na Korona Marekani na wazungu wanaamini katika loludouni lakini sisi hatuamini kufungia watu na njia zetu zimezaa matunda si kila kitu kufuata Marekani, Marekani leo Korona imenywea yenyewe hakuna mtu anaeamini.

Nchi ya Namibia nduguzangu imepita katika nyakati ngumu sana nendeni mkasome mtaona yote yaliyotokea yalikuwa na mkono wa Marekani, angalia Savimbi njinsi alivyotumika na Marekani na Kaburu Bota utaona vitu vya ajabu sana na kusikitisha, Utajiri wa Almasi Namibia ulikuwa laana kwao, angalia leo jinsi inavyotengeneza mashirika ya kiterolist na kujitoa muhanga hadi wasilamu wenyewe wanashangaa hii ni Marekani.

Tuanze kubadilika vijana. Maana pia nimesikia kunamtu anataka uraisi yeye anasema Marekani wanataka yeye ndiyo awe raisi wa Tanzania.
 
Tatizo hata mfumo wetu wa elimu umetawaliwa na mambo ya kigeni. Ndiyo sababu wanaohangaika na hizo balozi za makaburu kutafuta huruma zao si wananchi wa kawaida (common citizens) bali "wasomi" ambao kwa sehemu kubwa elimu zao ni za bandia. Akili zao zimetawaliwa na utumwa wa kifikra. Tarajia kuoga mvua ya matusi kutoka kwao wasomi hawa.
 
Yani ndio template rahisi ku-edit.

Ndio maana habari za ubalozi huo haziishi hapa.
 
Nakazia ni wakati wa mapinduzi ya kweli,tuna wasomi wengi na walete innovative ideas za kulikwamua taifa hili hoja za kipumbavu za demokrasia peleka jalalani.

Kwa mtazamo wangu demokrasia imewekwa na waasisi wake wakiwa na lengo la kupata ukweli wa taarifa nyeti za ndani mfano nchi kama China na urusi taarifa zake mbwa mkubwa anazipata kwa shida sana sasa mabwege Fulani kidogo wameshafikisha umbea.

Ni muda wa mabadiliko tuwekeze akili zetu kwenye mfumo wetu wa elimu kama Japan walivyofanya kwenye Meiji revolution, tunazo taasisi za elimu nzuri tu Arusha technical college,
UDSM,UDOM,MUHAS n.k hazihitaji msaada wa watu wa marekani zinahitaji update ndogo ndogo zilizo ndani ya uwezo wetu.
Tuwekeze kwenye sayansi na teknolojia na kwa kufanya hivi ndani ya miaka kumi ijayo hutaamini kama ni ile tz unayoijua.
Korea kaskaz anamsumbua mmarekani kwa sababu anajua kwenda na wakati.
It's not the strongest species that survive but the flexible one.
-Darwin

Don't ask what mother Tanzania can do for you,it has done a lot providing you with education, free health services, it's time to ask yourself what are you going to reward this beautiful mother
 
Umeishia kulalamika tu, unataka tukionewa tushtaki wapi?

Hao wamarekan mnaosema wabaya ndo wanatuletea ARV na misaada mbalimbali, kama hamuwaamin kwa nn mnapokea misaada yao nyie mbogamboga?
Ndio wakati wa mabadiliko, ndio Mkuu magu anaondoa hiyo dhana potofu lakini watu hawamwelewi coz wamesha adapt mfumo wa kishoga wa kusubiri kupewa tu.
 
Tatizo hata mfumo wetu wa elimu umetawaliwa na mambo ya kigeni. Ndiyo sababu wanaohangaika na hizo balozi za makaburu kutafuta huruma zao si wananchi wa kawaida (common citizens) bali "wasomi" ambao kwa sehemu kubwa elimu zao ni za bandia. Akili zao zimetawaliwa na utumwa wa kifikra. Tarajia kuoga mvua ya matusi kutoka kwao wasomi hawa.
download.jpg
 
Yaani kuishi na watu km ww ni balaa tupu hv unaijua Marekan au unaisomaga tu kwenye vitabu na magazet kisha unachanganya bra bra zako plus stor za mtaan kisha unapost ujinga hapa
Sasa nakupa siri kuhusu Marekan
1.Political stability
2.Strongest nation

Nilitaka nikufafanulie ila nimeona napotexa mda tu kula 7000 zako vzr
 
Nakazia ni wakati wa mapinduzi ya kweli,tuna wasomi wengi na walete innovative ideas za kulikwamua taifa hili hoja za kipumbavu za demokrasia peleka jalalani.

Kwa mtazamo wangu demokrasia imewekwa na waasisi wake wakiwa na lengo la kupata ukweli wa taarifa nyeti za ndani mfano nchi kama China na urusi taarifa zake mbwa mkubwa anazipata kwa shida sana sasa mabwege Fulani kidogo wameshafikisha umbea.

Ni muda wa mabadiliko tuwekeze akili zetu kwenye mfumo wetu wa elimu kama Japan walivyofanya kwenye Meiji revolution, tunazo taasisi za elimu nzuri tu Arusha technical college,
UDSM,UDOM,MUHAS n.k hazihitaji msaada wa watu wa marekani zinahitaji update ndogo ndogo zilizo ndani ya uwezo wetu.
Tuwekeze kwenye sayansi na teknolojia na kwa kufanya hivi ndani ya miaka kumi ijayo hutaamini kama ni ile tz unayoijua.
Korea kaskaz anamsumbua mmarekani kwa sababu anajua kwenda na wakati.
It's not the strongest species that survive but the flexible one.
-Darwin

Don't ask what mother Tanzania can do for you,it has done a lot providing you with education, free health services, it's time to ask yourself what are you going to reward this beautiful mother
Free health services? be serious.
 
Back
Top Bottom