Hivi Jakaya Mrisho Kikwete ni kweli alikuwa Tumaini lililorejea 2005?

Bright

Member
Apr 9, 2010
67
0
Bwana Prince M. Bagenda aliandika kitabu chenye kichwa cha habari "Jakaya Mrisho Kikwete: Tumaini Lililorejea" na kuchapishwa Machi 2006. Nafikiri mwaka 2011 inabidi tena aandike kingine sasa sijui kichwa cha habari kitakuwaje. Tumaini kama huyu JK tuliwahi kuwa nalo kweli baada ya uhuru?
 
Tatizo la wanaharakati walioishiwa!!! Bagenda .......that was too cheap braa!
 
Umesema aliandika kitabu ? Hapana yalikua ni maombi ya kazi kwani msanii hutunzwa kwa wimbo mzuri
 
bwana prince m. Bagenda aliandika kitabu chenye kichwa cha habari "jakaya mrisho kikwete: Tumaini lililorejea" na kuchapishwa machi 2006. Nafikiri mwaka 2011 inabidi tena aandike kingine sasa sijui kichwa cha habari kitakuwaje. Tumaini kama huyu jk tuliwahi kuwa nalo kweli baada ya uhuru?
watu wote waliodhani kuna jipya kwa kikwete sasa wanaona haya.
Mimi nilijua hakuna jipya kwa bwana huyu na hasa nilipogundua anatafuta urahisi (urais) kwa udi na uvumba.
Nilibaini uongo na ujanja ujanja usiosemekana.
Nilijua tumeliwa na wote niliowaasa wasitoe kura zao kwa huyu mbabaishaji leo wananiona kama nabii.
Swali langu kwao ilikuwa ni je, huyu bwana alikuwa amefanya nini kiasi kwamba tuweke tumaini kwake? Tulibaini hakuna labda ahadi zisizowezekana nyingiiiiii........... Sasa wote kila mmoja naona analia kama mimi.
Kikwete hana jipya na hataleta jipya zaidi ya kuvuruga uchumi wetu na siasa zetu.
 
Bwana Prince M. Bagenda aliandika kitabu chenye kichwa cha habari "Jakaya Mrisho Kikwete: Tumaini Lililorejea" na kuchapishwa Machi 2006. Nafikiri mwaka 2011 inabidi tena aandike kingine sasa sijui kichwa cha habari kitakuwaje. Tumaini kama huyu JK tuliwahi kuwa nalo kweli baada ya uhuru?

hivi unaweza kuona kuna watu kabisa wanatupa hela zao kununua kitabu alichotunga huyu jamaaa, nani hamjui kuwa ni kibaraka na silaha ya sisiemu(ccm)?
 
Huyo Bagenda naye alitaka kujipendekeza tu. Hamna kitu!

baada ya kujipendekeza, hakupata kitu, aibu eheee, alitaka amuige Mkandara wa udsm pale alipotoa ile riport wakati wa kampeni za kikwete, jamaa alivyochukua urais tu, kampa cheo udsm kifuta machozi. pole bagenda, aibu lakiniiiii,
 
Back
Top Bottom