Hivi itakuja kutokea duniani muimbaji bora wa kike kama Whitney Houston?!

Wadau kwa muda wa miaka mingi nimesikiliza muziki wa RnB, Soul na Pop hasa wa wasanii wa kike ila mpaka sasa sijapata wa kumfikia WH! Huyu katika wasanii hakika alikuwa msanii na sidhani kama kuna msanii wa kufikia records alizoweka!
Mpaka anafariki alikuwa kashapata tuzo, 640+ huku akiwa nominated zaidi ya mara 781!!
Mbali na Whitney Houston Wasanii wanaomfatia kwa ubora ni pamoja na

2. Mariah Carey

3. Celine Dion

4. Christina Aguilera

5. Beyonce

6462db0a37784bd65ea396f5799f8e22.jpg


36eecb7c6ffaa7c9e4dd1cc8063d4643.jpg
Huo ni mtazamo.
Kwa upande wangu hakuna kama Miriama Makeba.
 
Sijui kama kweli but niliwahi sikia nyimbo za Whitney zilikuwa zikitumika kuwaamsha wagonjwa walio kwenye coma
na zimewahi kutumiwa na NASA huko kwenye space....


Really?...Wow!
I will always love her.
 
Uongo ni kwamba BB ndiye kamfundisha WH kubwia unga. BB yeye alikuwa mtu wa jani hadi alipokutana na WH ndiyo akaanza kuwa nyoka mla unga.

Nimekuwekea huo wimbo ili uone tofauti yao kuwa mwaka 1985 wakati WH anatoa hicho kibao, Bobby Brown alikuwa na Mtoto wa miaka 16. Ukiangalia mwili wa WH unaona kuwa unga wa Columbia ulishaanza kumchonga.

Wote walibugia na siyo siri. WH akakafundisha hata katoto kake nakenyewe kakaanza kubugia na mwisho na kenyewe kakafa maji kwenye bafu la kuogea.....maajabu matupu mtu kufa kwenye bafu

Anyw, unaweza ukabaki na ufahamu wako kuwa ni BB kamfundisha WH kubugia unga. Yaani Katoto kadogo kanamfundisha Shangingi la kimataifa kubugia unga.
Sasa uongo uko wapi hapo bwashee? Kwamba Whitney alikuwa abwii unga? Kwamba hakuwa anabwia unga na BB? Haya mambo wote tunasoma tu kutoka source mbalimbali na usilete ujuwaji...

Nikikuuliza tu mmatumbi mwenzio Ray C ni nani kamfundisha kubwia unga unaweza kutowa maelezo?
 
Sasa uongo uko wapi hapo bwashee? Kwamba Whitney alikuwa abwii unga? Kwamba hakuwa anabwia unga na BB? Haya mambo wote tunasoma tu kutoka source mbalimbali na usilete ujuwaji...

Nikikuuliza tu mmatumbi mwenzio Ray C ni nani kamfundisha kubwia unga unaweza kutowa maelezo?
Atakuambia lord eyez
 
Huyu Mama na kumzidi umri BB bado BB ndiye amfundishe HW kutumia unga? Acheni uongo kama hamfahamu historia ya watu.

Whitney alikuwa mtumia unga kwa miaka mingi tu ila sema familia walificha au hawakutaka kuliona hilo na wakaja wakapata jalala la kutupia lawama.

Wee mtu alishatoka na akina Eddy Murphy, Jermain Jackson, Scott Pippen nk ndiyo kuja kuokotwa na kitoto BB by the time.

Mama ndiyo maana alikuwa amekauka mwili kwa miaka mingi kwa sababu Cocca inakausha mwili na mtu anakuwa hana Maziwa wala Makalio.

Hebu angalia huu wimbo ambao aliimba wakati hajawa bado na BB jinsi alivyochonga na kubaki mifupa. Cocca inachongesha watu si kawaida.


Huu wimbo ni kati ya nyimbo zake za mwanzo kabisa katika tasnia ya muziki, nyingine kama 'I wanna dance with somebody etc, hiyo ni miaka ya mwanzo ya 80's na ndo lilikuwa umbo lake na sio kwamba alishaabza kubwia madawa
 
Jamani tusimsahau Celine Dion huyoo ndo no.Moja anafata Whitney sio lazima uwe Na Tuzo nyingi ndo unaweza wengine Nyota tu..Mfano Barnabas Na Diamond
 
Mkuu,
Kama umeshawaona wala Unga wa Cocaine, wengi huwa wanachongeka kama wanywa Gongo. Angalia hata Video walivyomjaza Makeup kibao ili kuficha uso ulivyoharibika. Siyo umbo lake hilo ila effect za Unga.

Matola hebu someni hii habari kama MLIPITIWA na hamkusoma:

'I feel responsible': Whitney's brother Michael reveals HE was the one who introduced her to drugs

Read more: 'I feel responsible': Whitney's brother Michael reveals HE was the one who introduced her to drugs

Michael Houston Did Crack Cocaine With Whitney Houston Before Bobby Brown, He Confesses To Oprah
Read more: Michael Houston Did Crack Cocaine With Whitney Houston Before Bobby Brown, He Confesses To Oprah

Huu wimbo ni kati ya nyimbo zake za mwanzo kabisa katika tasnia ya muziki, nyingine kama 'I wanna dance with somebody etc, hiyo ni miaka ya mwanzo ya 80's na ndo lilikuwa umbo lake na sio kwamba alishaabza kubwia madawa
 
Umenikumbusha mwimbaji wa Pakistan wa kitambo aitwaye Nazia Hassan ambaye ni Marehemu sasa. Wimbo wake ulipendwa sana hata Tz ingawa kwa bahati film yake hadi leo sijaiona.


Lata Mangeshkar wa India ana umri wa miaka 86, ameanza kuimba 1942.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom