Hivi ingekuwaje 2015 kama tusingempata Hayati Magufuli kwa nchi ilipokuwa imefikia?

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
983
2,053
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa.

Nani hakumbuki hata viongozi wa upinzani waliwahi sema tunahitaji Rais dikiteta? Na kweli walikuwa sahihi kabisa manake tulikuwa pabaya mno.

Fikirieni nchi hadi tukawa hatuna Tena ndege, shirika la reli limekufa, huduma za jamii zimezolota kabisa. Kwa ufupi tufika pabaya mno kama nchi na suluhisho ilikua ni lazima apatikane mtawala kama JPM ili aweke nchi sawa kwanza ili baadaye ndo tuje tupate kiongozi.
Tatizo la JPM Naona alifanya kazi hadi akapitiliza.

Kwangu Mimi JPM alichoharibu ni suala la uchumi na democracy tu lakini kwa vitu vingine huyu jamaa alikuwa kichwa sana tukichukulia na nchi ilipokuwa imefikia.

Nawakumbusha Tena kwa tulipokuwa tumefika ilikuwa ni lazima tumpate JPM ili kuiweka nchi kwenye mstari.

Kwa hiyo tumpe sifa zake na yale mabaya aliyofanya tuchukue kama Somo ili tusonge mbele ndugu zangu.
 
"Kwangu Mimi JPM alichohalibu ni swala la uchumi na democracy tu lakini kwa vitu vingine huyu jamaa alikua kichwa Sana tukichukulia na nchi ilipokua imefkia."

Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani, mengine ni kuendekeza sana kupata sifa binafsi mpaka kufikia kusema vitu kama hakuna corona ambayo ilichangia vifo vya wengi. Lakini kuna vitu lazima tukubali amejitahidi especially miundombinu.
 
Magufuli hakuheshimu katiba, aliminya haki za wananchi, Alileta siasa za biashara za kununua watu, Aliiba chaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kiwango cha Kutisha, Aliua watu Zanzibar, Akaunda magenge ya wasiojulikana, wakateka, wakaua watu hivihivi bila hofu, Akatumia pesa za nchi bila due process, Alikuwa mkanda, Akanajisi bunge, vyombo vya habari na mahakama, Alikuwa katili alivunja nyumba za wananchi wakati kuna zuio la Mahakama, Akateua na kulinda viongozi washenzi kama akina Sabaya na Makonda, Alikuwa muongo, msanii asiye na lugha za staha.

Kiufupi huyo Magufuli wako alikuwa tje worst president, hatuwezi kumuweka katika kundi la marais wazuri wa nchi hii
 
Nawasalimu ndugu zangu ,natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa...
Kwann mnafungua nyuzi kumuongelea huyu jambazi, mkabila, mkanda, muuwaji, mtekaji, mwenye roho mbaya, mbaguzi, mwnye kauli chafu, mtukanaji mbele ya hadhara, n.k?

Huyu ni chukizo mbele za Mungu na wanadamu.
 
1625127511848.png
 
Magufuli hakuheshimu katiba, aliminya haki za wananchi, Alileta siasa za biashara za kununua watu, Aliiba chaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kiwango cha Kutisha, Aliua watu Zanzibar...
Hayo yote yameangukia kwenye swala la Uchumi na Democracy.Upo sahihi kwa mtazamo wako Wala sikupingi lakini nazani yote ni kwa Sababu kipindi anachukua nchi presure ilikua kubwa ukiizingatia upinzani ulikua mkubwa Sana .Kuitoa nchi kwenye mazoea na kuiweka sawa ilifkia kipindi akawa anajihami na Katika kujihami ikapelekea kuumiza watu.

Hata na Mimi nikili kaniumiza kiuchumi pakubwa Sana lakini nshamsamehe na bado nakili Kuna vitu kafanya kwa faida ya Nchi
 
Kikwete angeendelea walau kwa miaka mitano mbele tungekuwa tumeshaondoka kwenye kundi la nchi maskini na uchumi ungepata kwa mwendo wa swala kama sio mwendo wa duma.

Nchi mbalimbali za Afrika wangekuja kwetu kujifunza jinsi ya kukuza uchumi kwa kasi. Tatizo la Watanzania wengi ni sadists hivyo hatupendi mafanikio ya wengi na tunapenda kuona watu wakiwa na maisha ya chini kuliko sisi ili watunyenyekee.

Pia hata sisi wenyewe pia tukifanikiwa hujiona miunguwatu na kuwa limbukeni.
 
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa...
JPM alikuwa ni kiongozi mwenye kufanana sana na mahitaji ya nchi yetu. Uonevu ulikuwa umezidi na watu wakijiona ni miungu watu.

Kulikuwa na umafia wa hali ya juu, mitandao ya unyanganyi wa mali za watu ukiongozwa na wafanyakazi wa serikali, hatukuogopana kiasi cha kuoneana huku tukijua yule anayeonewa hana uwezo wa kumfanya chochote muoneaji.

Reli mara ya mwisho kufika Moshi ilikuwa 1995 JPM mwaka jana kaifufua hiyo safari Wachagga wameenda krismasi wakitandika pombe kwenye mabehewa. Hivi sasa kuna wataalam wa masuala ya masuala ya reli 120 wamesomeshwa pale NIT ili wakati SGR ikianza kazi tuwe tayari na wataalam wazalendo.

Ndege hizi kama sio uwezo wa kufuatilia aliokuwa nao RIP zisingenunuliwa. Twiga asingeonekana angani, Mama Samia asingesafiri kwenda Kenya na Uganda akijinafasi.

Hayati alikuwa na udhaifu wake wa hasira na maamuzi yenye kuumiza wengi. Ukitaka tajiri aishi kama shetani maana yake unamuua na njaa mfanyakazi wake. Manji alienda zake Canada, Mo Dewji anaweza kwenda zake South Africa, Bakhresa anaweza kuishi Dubai au New York, tatizo ni yule dereva wake, tatizo ni yule mfanyakazi wa kampuni yake anayesomesha na kulea familia.

Hayati alikuwa na matatizo ya kiafya ambayo ni makubwa, ilikuwa ni vigumu kwake kuwa na amani ya kiakili ikiwa ndani ya moyo kumewekwa kitu cha kumsaidia kupumua. Alikuwa ni mkiwa anayeishi miongoni mwa watu wengi kwa wakati mmoja.

Mungu natumaini amemsamehe madhambi yake kwa kuweza kupata sakramenti ya mwisho siku aliyoaga dunia.
 
Magufuli hakuheshimu katiba, aliminya haki za wananchi, Alileta siasa za biashara za kununua watu, Aliiba chaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kiwango cha Kutisha, Aliua watu Zanzibar, Akaunda magenge ya wasiojulikana, wakateka, wakaua watu hivihivi bila hofu, Akatumia pesa za nchi bila due process, Alikuwa mkanda, Akanajisi bunge, vyombo vya habari na mahakama, Alikuwa katili alivunja nyumba za wananchi wakati kuna zuio la Mahakama, Akateua na kulinda viongozi washenzi kama akina Sabaya na Makonda, Alikuwa muongo, msanii asiye na lugha za staha.

Kiufupi huyo Magufuli wako alikuwa tje worst president, hatuwezi kumuweka katika kundi la marais wazuri wa nchi hii
Marais wazuri wa nchi hii ni akina nani hao?
 
"Kwangu Mimi JPM alichohalibu ni swala la uchumi na democracy tu lakini kwa vitu vingine huyu jamaa alikua kichwa Sana tukichukulia na nchi ilipokua imefkia."

Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani, mengine ni kuendekeza sana kupata sifa binafsi mpaka kufikia kusema vitu kama hakuna corona ambayo ilichangia vifo vya wengi. Lakini kuna vitu lazima tukubali amejitahidi especially miundombinu.

Mmh vifo vya wengi?’ Hapa Tz au huko ulaya kulikokua na lockdown?!
 
Kikwete angeendelea walau kwa miaka mitano mbele tungekuwa tumeshaondoka kwenye kundi la nchi maskini na uchumi ungepata kwa mwendo wa swala kama sio mwendo wa duma. Nchi mbalimbali za Afrika wangekuja kwetu kujifunza jinsi ya kukuza uchumi kwa kasi. Tatizo la Watanzania wengi ni sadists hivyo hatupendi mafanikio ya wengi na tunapenda kuona watu wakiwa na maisha ya chini kuliko sisi ili watunyenyekee.. pia hata sisi wenyewe pia tukifanikiwa hujiona miunguwatu na kuwa limbukeni

Uchumi wa mission town au uchumi wawizi watu hawafanyi kazi ila wqnapesa
 
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa...
Uchumi na democracy ndo sifaa kuu ya maendeleo. Kwa hiyo jpm aliharibu kila kitu maana iriharibu inner core ya maendeleo akabaki anapapasa tu au anapuyanga kama zitto kabwe
 
Kwak
Kwann mnafungua nyuzi kumuongelea huyu jambazi, mkabila, mkanda, muuwaji, mtekaji, mwenye roho mbaya, mbaguzi, mwnye kauli chafu, mtukanaji mbele ya hadhara, n.k?

Huyu ni chukizo mbele za Mungu na wanadamu.
Kila binadamu ni chukizo
 
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa...
Pole. JPM alitutoa kwenye mwanga na kutuweka gizani. Kumbuka; mazuri aliyofanya binadamu huzikwa nayo mifupani mwake na mabaya hushamiri na kukumbukwa daima.
 
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa...
Katika viongozi ambao wamerudisha nyuma maendeleo ya nchi hii, kuleta ubaguzi na mifarakano katika jamii ni Magufuli! Afadhali alivyopotea kwa sababu angeipeleka nchi kubaya sana na hata kusababisha vita vya sisi wenyewe!
 
Nawasalimu ndugu zangu, natumai hamjambo wote.

Ndugu zangu sote tunakumbuka ni wapi nchi yetu ilipokuwa imefkia kwa ufupi ilikuwa inaenda shimoni kwa maana kila kitu kiliharibika na alihitajika kiongozi mwenye kaliba ya JPM kuitoa nchi Mahali ilipokuwa.

Nani hakumbuki hata viongozi wa upinzani waliwahi sema tunahitaji Rais dikiteta? Na kweli walikuwa sahihi kabisa manake tulikuwa pabaya mno.

Fikirieni nchi hadi tukawa hatuna Tena ndege, shirika la reli limekufa, huduma za jamii zimezolota kabisa. Kwa ufupi tufika pabaya mno kama nchi na suluhisho ilikua ni lazima apatikane mtawala kama JPM ili aweke nchi sawa kwanza ili baadaye ndo tuje tupate kiongozi.
Tatizo la JPM Naona alifanya kazi hadi akapitiliza.

Kwangu Mimi JPM alichoharibu ni suala la uchumi na democracy tu lakini kwa vitu vingine huyu jamaa alikuwa kichwa sana tukichukulia na nchi ilipokuwa imefikia.

Nawakumbusha Tena kwa tulipokuwa tumefika ilikuwa ni lazima tumpate JPM ili kuiweka nchi kwenye mstari.

Kwa hiyo tumpe sifa zake na yale mabaya aliyofanya tuchukue kama Somo ili tusonge mbele ndugu zangu.
Kama aliharibu uchumi na demokrasia then atakuwa alipatia nini Mkuu ..... maana hivyo ndiyo vitu muhimu!!
 
Magufuli hakuheshimu katiba, aliminya haki za wananchi, Alileta siasa za biashara za kununua watu, Aliiba chaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kiwango cha Kutisha, Aliua watu Zanzibar, Akaunda magenge ya wasiojulikana, wakateka, wakaua watu hivihivi bila hofu, Akatumia pesa za nchi bila due process, Alikuwa mkanda, Akanajisi bunge, vyombo vya habari na mahakama, Alikuwa katili alivunja nyumba za wananchi wakati kuna zuio la Mahakama, Akateua na kulinda viongozi washenzi kama akina Sabaya na Makonda, Alikuwa muongo, msanii asiye na lugha za staha.

Kiufupi huyo Magufuli wako alikuwa tje worst president, hatuwezi kumuweka katika kundi la marais wazuri wa nchi hii
Kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom