Hivi inamaana tanzania itapata viongozi kutoka chadema na ccm pekee ?

siriusblack

Senior Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
165
Points
250

siriusblack

Senior Member
Joined Apr 30, 2013
165 250
Nadhani sasa inabidi Watanzania tubadili fikra na tuone Tanzania yetu ni zaidI ya U-CHADEMA na U-CCM , Siamini kwamba vyama pekee vyenye viongozi bora ni CHADEMA na CCM pekee.

Watanzania hatupati majibu ya kero dhahiri zilizopo kwenye nchi yetu badala yake tunapelekwa pelekwa tu na habari za siasa huku nchi za wenzetu wakipiga hatua mbali kutuacha na sisi kubaki kufarakana na kuwekeana nongwa tena kwa maslahi ya watu wachache.

Ifike mahali Watanzania tusikubali kugawanywa kwa misingi ya udini na ukabila na badala yake si tu kudai bali tuhakikishe watoto wetu wanapata elimu bora kwakuwa elimu itatusaidia sisi na watoto wetu kuona mmgawanyo wa rasilimali hauko sawa na kasi ya serikali katika kujibu na kutatua kero za wananchi hairidhishi na hivyo tutumie busara tutakapo pata nafasi ya kupiga kura tena mbeleni huko kwakuwa baada ya miaka kumi tunaweza kuona kama tunaelekea tunakokutaka au la.

Kama ni upinzani basi tupime na kuangalia , ukiacha kupambana majukwaani na movements wamelifanyia nini jimbo na tukipata majibu basi ndipo tuamue kupiga kura

Lakini kingine Watanzania tukatae rushwa, suluhisho la matatizo mengi litaanza na sisi na hatua mojawapo ya kuelekea tunapokutaka ni kwa kuanza kukataa rushwa

Hivyo basi ndugu zangu wa Tanzania tusikubali kupoteza muda kwenda kusikiliza mtu akituambia maneno matupu tu majukwaani tutumie historia, mafanikio ya jimbo na mafanikio ya nchi kwa ujumla kuamua ni wapi tutakaa masaa hata zaidi ya sita ya kumsikiliza mtu ambaye atakuwa ana nia ya dhati na sera nzuri , tusikubali kupoteza muda bure bure tu.
 

Forum statistics

Threads 1,391,023
Members 528,344
Posts 34,070,642
Top