Hivi inakuwaje unamtengenezea mpenzi wako fumanizi feki na kumkodia watu wamlawiti?

Spa Africa

Member
Mar 8, 2018
24
57
Juzi kati nilikuwa kituo kimoja cha Polisi(jina nalihifadhi),nilienda kufuatilia kesi ya ugomvi kati ya binamu yangu na mkewe,huyu binamu yangu alikuwa amempiga mkewe kwa kuchelewa kurudi nyumbani,lakini utetezi wa mkewe ni kwamba alichelewa sababu ya foleni,na kwa kweli shemeji yangu alikuwa amekula kichapo cha maana sana,kiasi mjumbe wa mtaa ilibidi aipeleke ile kesi polisi ili na yeye ajivue lawama.Sasa katika kfika pale polisi,huyu shemeji yangu alitaka mambo yaishe tu,maana "wamesameheana",ila hawa polisi wakawa wanakomaa na mwanaume(binamu yangu).

Pale polisi kumbe sijui kuna dawati la Wanawake,sasa wale polisi wa kike wanakomaa na jamaa,kuwa hata kama kasemehewa,lakini wao lazima wamshikishe adabu.

Sasa tukiwa hapo polisi,ikaja kesi nyingine,hii ni ya mdada mmoja kaletwa na ndugu zake,amepigwa sana na mumewe na wanadai mumewe kamtengenezea fumanizi feki halafu kamkodia mabaunsa wamempiga na kumlawiti.Na kweli yule dada kapigwa haswaa,anaonekana ni binti mdogo hivi around 25-30.

Katika kusikiliza maongezi ya polisi,inaonekana huyo mwanamke kapigwa sana na mumewe na kwa maelezo ya mwanamke ni kuwa jamaa alikuwa kamchoka,anamfanyia vitimbi lakini haondoki,akaamua kutengeneza kama fumanini,halafu akakodisha mijamaa ikamka tigo mdada huku akirekodiwa.

Sasa hebu wanasaikolojia wa mambo ya mapenzi watujuze,hivi kama mwanamke humpendi kwanini usimfukuze?Huyu mtu inakuwaje anatengeneza fumanizi feki na kufikia kumlawiti mkewe?Halafu sheria imekaaje kwa mume kukodi watu wamlawiti mkewe?Sikubahatika kumuona huyo jamaa mwenye kutenda huo unyama,ingawa jambo hili limenishangaza sana.

Sisi tuliozesha watoto wetu wa kike,ukisikia mtoto wako katendewa hivi na mumewe utafanya nini?Nimestaajabu sana sana.
 
Umasikini ndio kitu kinachofanya mambo ya ajabu kutokea kwenye ndoa,,,ila ukiangalia wanawake wanaojiweza wakiona mwanaume anaanza kubadilika wanajiweka pembeni haraka sana kwasababu anajua anauwezo wakuendesha maisha yake
Nakubaliana na wewe 99%
 
Hata kama ni umasikini, lakini mwanamke ana kwao. Ni nafuu sana kuishi katika hali ya umasikini kuliko kuishi kwa mateso.

Pamoja na kuwa hakuna uthibitisho wa kuwa ni mke wa ndoa, ila wakati wawili hao wanakutana, Hugo jamaa si alikubaliana na hali halisi ya familia? Msichana amekutwa kwenye hali ya umasikini, anaweza kuendelea kuishi maisha hayo ambayo amekuwa akiyaishi kwa furaha kuliko udhalilishaji wa namna hii.

Mwanaume unaoa ili iweje? Sikh moja nawe ukizaa mtoto wa like halafu akateswa hivi, utakuwa kwenye nafasi ya kumtetea?

Ninakerwa mno na unyanyasaji huu. Ni muhimu sana kumheshimu mtu aliyejitolea kutumia maisha yake yaliyosalia kuishi nawe. Ni heshima kubwa mno na isiyo na kipimo. Wanaume tumezidi kwa unyanyasaji.

Kuna uwezekano mkubwa mwanaume ukitulia, mke wako,naye akatulia. Na mnajipa nafasi nzuri zaidi ya kujenga maisha.

Mwanaume tuna nafasi kubwa sana ya kumfanya mwanamke/ mke / mchumba na familia kwa ujumla ikawa ya furaha sana. Tutimize wajibu wetu.
 
Hakika maneno yako yameniingia sana moyoni ukizingatia nina mabinti watatu wakubwa mmoja ana 23 mwingine ana 18 na mwingine ana 15 nimeumia sana kwakweli
Hongera sana mkuu ujumbe wako umeni impress sana
 
Hata kama ni umasikini, lakini mwanamke ana kwao. Ni nafuu sana kuishi katika hali ya umasikini kuliko kuishi kwa mateso.

Pamoja na kuwa hakuna uthibitisho wa kuwa ni mke wa ndoa, ila wakati wawili hao wanakutana, Hugo jamaa si alikubaliana na hali halisi ya familia? Msichana amekutwa kwenye hali ya umasikini, anaweza kuendelea kuishi maisha hayo ambayo amekuwa akiyaishi kwa furaha kuliko udhalilishaji wa namna hii.

Mwanaume unaoa ili iweje? Sikh moja nawe ukizaa mtoto wa like halafu akateswa hivi, utakuwa kwenye nafasi ya kumtetea?

Ninakerwa mno na unyanyasaji huu. Ni muhimu sana kumheshimu mtu aliyejitolea kutumia maisha yake yaliyosalia kuishi nawe. Ni heshima kubwa mno na isiyo na kipimo. Wanaume tumezidi kwa unyanyasaji.

Kuna uwezekano mkubwa mwanaume ukitulia, mke wako,naye akatulia. Na mnajipa nafasi nzuri zaidi ya kujenga maisha.

Mwanaume tuna nafasi kubwa sana ya kumfanya mwanamke/ mke / mchumba na familia kwa ujumla ikawa ya furaha sana. Tutimize wajibu wetu.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Back
Top Bottom