Hivi inakuwaje mwezi uandame Kenya halafu Tanzania usiandame?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,381
Bila jazba Wala povu, nauliza?

Nimeona Matangazo wenzetu Kenya wanasema wameuona Mwezi na Leo ni Idd ElFitri!

Huku kwetu tunaambiwa mwezi haujaandama?

Hii huwa inatokeaje, kijigrafia mbona tupo Ukanda mmoja, hili linawezekanaje?

Na wala si mara ya kwanza utata huu kuwepo?

Tatizo ni Nini!
Ni suala la kiamani, kisayansi au ni nini?
Wengine utawasikia wakilalama BAKWATA ni CCM kama ndivyo suala la kuandama mwezi liwe ni Siasa!

Kuna nini kimejificha?
 
Bila jazba Wala povu , nauliza ?
Nimeona Matangazo wenzetu Kenya wanasema wameuona Mwezi na Leo ni Idd ElFitri!
Huku kwetu tunaambiwa mwezi haujaandama?!
Hii huwa inatokeaje,Kijigrafia mbona tupo Ukanda mmoja ,hili linawezekanaje?
Na Wala Si mara ya kwanza utata huu kuwepo ?
Tatizo ni Nini!
Ni suala la kiamani,kisayansi au ni Nini?
Wengine utawasikia wakilalama BAKWATA,ni CCM kama ndivyo suala.
la kuandama mwezi liwe ni Siasa!
Kuna Nini kimejificha?

Acheni kulaumu mnataka kuharibu nguzo yenu hii ya uislamu.Siku moja tuu inawasumbua akili? hebu malizieni salama.Leo mwezi utaonekana, jana kulukuwa na mawingu
 
Bakwata hawajui kutofautisha kuandama na kuona mwezi wao hawajaona sio haujaandama. Hawa Bakwata ni wakati wa waislamu kupinga kwa nguvu serikali katika kuwatambua hawa liundwe baraza la kujitegemea kutangaza mwezi sio kikundi fulani wanatia watu dhambi na baya zaidi wanagawa waislamu kila kukicha.
 
Acheni kulaumu mnataka kuharibu nguzo yenu hii ya uislamu.Siku moja tuu inawasumbua akili? hebu malizie salama.Leo mwezi utainekana jana kulukuwa na mawingu
Shida sio siku moja hapana tumeambiwa ni haramu kufunga siku ya Eid na baya zaidi hili linawagawa waislamu sana kwanza tukasema sawa tusifuate Saudi Arabia sasa tunaigawa hata na E. Africa kwa faida ya nani? tukubaliane mwezi ukiandama E.Africa tufuate Bakwata wasijifanye wamekuwa Saudia sasa wanazuoni wa Kenya wanajulikana kuna elmu kubwa kule na watu wa Lamu wanajulikana katika mambo haya ya dini. Itafika siku Mwanza watasema tumeona mwezi na Dar watasema hatujaona. Kuna tofauti mwezi kuandama na kuona mwezi. Bakwata hawajaona sio haujaandama.
 
Kwanza huyu Mufti kwa elimu gani hasa ya kuongoza waislamu? Ni wakati sasa waislamu kuweka tofauti zao pembeni na kuwaambia serikali imefika mwisho kutambua Bakwata kama chombo kikuu cha waislamu wafanye mambo yao lakini kuwe na chombo na sio Tanzania tu kiwe E.Africa watakaokuwa wanatangaza hii hali kwa umakini na uhuru kwa mujibu wa dini lakini hatuwezi kufika huku. wamefanya kazi kubwa kutengenisha waislamu wa Tanzania na wamefanikiwa sasa wanatenganisha waislamu wa E.Africa sijui mwisho tutatengana kwa mikoa kama Dar na Moro.
 
Bila jazba Wala povu , nauliza ?
Nimeona Matangazo wenzetu Kenya wanasema wameuona Mwezi na Leo ni Idd ElFitri!
Huku kwetu tunaambiwa mwezi haujaandama?!
Hii huwa inatokeaje,Kijigrafia mbona tupo Ukanda mmoja ,hili linawezekanaje?
Na Wala Si mara ya kwanza utata huu kuwepo ?
Tatizo ni Nini!
Ni suala la kiamani,kisayansi au ni Nini?
Wengine utawasikia wakilalama BAKWATA,ni CCM kama ndivyo suala.
la kuandama mwezi liwe ni Siasa!
Kuna Nini kimejificha?
Mnashangaa nini mbona Rais wa Zanzibar aliwahi kutangaza muandamo wa mwezi.
 
255717649082_status_5eef8922c313406895d7e24fda5416b7.jpg
 
Back
Top Bottom