Hivi inakuwaje mtu mzima na akili timamu anaenda kwa mganga wa kienyeji

Alagwa

Member
May 30, 2012
95
84
Katika Maisha haya nimewahi kuwa na marafiki wengi ila kwa vipindi tofauti tofauti ila huyu wa sasa sijamuelewa kabisa. Yani mshikaji wangu huyu kila kitu kikitokea yeye Huwaza ni ushirikina.

Basi juzi aliniaga anaenda mahali ila hakuniambia ni wapi jana katika kupiga piga stori mara akaniambia alienda kwa mganga eti Kuna mtu anachezea nyota yake daaaaaa nilimsikitikia maana sikutegemea kama msomi na kijana kama yeye bado atakuwa gizania kiasi hiki.

Mi naelewa kuwa mafanikio nimatokeo ya namna unavyojituma ila sio ndumba wala ushirikina. Je wewe unaamini mambo ya waganga au kuloga
 
Kwani Biblia au Quran inasemaje kuhusu ushirikina, uchawi upo na unafanya kazi, Jamaa yupo sahihi, mana hata mimi nawazaga kwenda kwa mganga ila Biblia inasema amelaaniwa mtu Yule amtegemea mwanadamu kuwa Kinga yake na moyoni mwake amemuacha bwana,
Wazungu wametubrain wash.
Muhimu kuutafuta ukweli na ukweli utakuweka huru.
 
Katika Maisha haya nimewahi kuwa na marafiki wengi ila kwa vipindi tofauti tofauti ila huyu wa sasa sijamuelewa kabisa. Yani mshikaji wangu huyu kila kitu kikitokea yeye Huwaza ni ushirikina. Basi juzi aliniaga anaenda mahali ila hakuniambia ni wapi jana katika kupiga piga stori mara akaniambia alienda kwa mganga eti Kuna mtu anachezea nyota yake daaaaaa nilimsikitikia maana sikutegemea kama msomi na kijana kama yeye bado atakuwa gizania kiasi hiki. Mi naelewa kuwa mafanikio nimatokeo ya namna unavyojituma ila sio ndumba wala ushirikina. Je wewe unaamini mambo ya waganga au kuloga
Mkuu nauwezo wa kukufanya uumwe kichwa kwa masaa 4

Mahitaji;nitumie majina yako matatu pamoja na picha yako WhatsApp

Utaleta mrejesho mwenyewe
 
Dunia inaweza kuwa Pana zaidi ya unavyoijua wewe huwezi jua watu wanakumbwa na vitu gani katika maisha yao.Usitegemee kila binadamu aishi kama wewe kila mtu yuko huru kuamini anachokitaka usomi hauwezi kuwa kinga ya watu kutokwenda kwa waganga.Kuna dunia nyingine togauti na hii unayoijua wewe kuna siku unaweza kuwa kwenye point ambayo utakuwa desperate and you will be happy to visit A witch doctor.
 
Back
Top Bottom