Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya. A business administrate?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya a business administrate?

Genge la kuuza nyanya mtaji elfu 20

Hizo skili zake za business administration anataka akazionyeshee wapi?
 
Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya a business adminstrate?

Genge la kuuza nyanya mtaji elfu 20

Hizo skili zake za business administration anataka akazionyeshee wapi?
Inashangaza kwakweli ila usishangae sana, alisoma ili aje kuajiriwa na benki au kampuni flani, na akiajiriwa hapo basi ndoto yake imetimia na atakomesha watu mtaani hasa wasio na ajira.

Ndivyo elimu na mazingira halisi ya kibongo yalivyo.

Pia utashangaa zaidi huyuhuyo ukimkuta anawasifia sana entrepreneurs wa nchi zingine hasa Marekani kuwa yule jamaa alianza chini sana leo ni bilionea mkubwa anamiliki kampuni flani.
 
Business Administration siyo somo la biashara japo marketing imo Ila watu wengi wasichoelewa kinachofundishwa ni utawala ile department ya utawala yaani managerial ya kusimamia decision making, ndio maana wanasomea BA Wana perform vizuri wanapokuwa kwenye position za management Kama finance manager, HRM, Marketing Manager na nyingine za management, ni Kama mtu aliyesomea chuo cha CBE Kuna course tofauti na siyo kwamba unasomea jinsi ya kufungua biashara Kama wengi wanavyodhani.
 
Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya a business adminstrate?

Genge la kuuza nyanya mtaji elfu 20

Hizo skili zake za business administration anataka akazionyeshee wapi?
Tuwekee mtaala wa hiyo diploma, ili tuweze kutoa maoni yaliyo sahihi.
 
Jenga hoja mkuu, kila mtu hapa anasoma unachochangia. Msingi wa swali lake utamkuta mtu kasoma hiyo kozi ya BA lakini anashindwa hata kufanya biashara ndogo huku yupo mtaani amepigika akisubiri labda ajira.
Business Administration siyo somo la biashara japo marketing imo Ila watu wengi wasichoelewa kinachofundishwa ni utawala ile department ya utawala yaani managerial ya kusimamia decision making, ndo maana wanasomea BA Wana perform vizuri wanapokuwa kwenye position za management Kama finance manager, HRM, Marketing Manager na nyingine za management, ni Kama mtu aliyesomea chuo cha CBE Kuna course tofauti na siyo kwamba unasomea jinsi ya kufungua biashara Kama wengi wanavyodhani.
 
Kwanza sema ni business administrator na si BUSINESS ADMINISTRATE. Pili pesa za mtaji za kuanzisha biashara hazihusiani na elimu ya mtu, ndio utajiuliza mbona ulipokuwa chuo kikuu ulikuwa na boom na hukuwahi fikiria kuanzisha hata genge la kuuza nyanya yenye mtaji wa elfu 20?
 
Huu mfumo wetu wa kusoma ufaulu mitihani, ukariri ufaulu mitihani ni wa hovyo. Tunasema mara nyingi huu mfumo umepitwa na wakati lakini kwa kua unawafaidisha wanasiasa sio rahisi kueleweka.

Huu mfumo uko kisiasa, utasikia wamepata divisheni one elfu 10, ufaulu umeongezeka kwa asilimia tano, sijui utumbo gani, sasa divisheni hizo na ufaulu unawasaidia nini watoto?

Mwisho wa siku hao wenye divisheni one ama two wanafika chuo kikuu wanasomea business administration halafu wanasubiri waajiriwe, anamiliki simu ya milioni 2 halafu akakaa kijiweni kungoja ajira.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom