Hivi inakuwaje msomi wa mambo ya fedha hajui shilingi Elfu 10 ina mnyama gani? Anashindwa kujibu kwenye interview

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Nimechoka, nilienda kusimamia interview watu wana degree za finance za kwanza na za pili na CPA wameshindwa kujibu swali la written interview lililohoji Noti ya Elfu kumi ina mnyama gani? Nimechoka. Sasa mtu anasomea mambo ya fedha ya kitu gani wakati hajui hata hela noti ya elfu 10 ina mnyama gani.

Hopeless kabisa wasomi wetu wajiongeze waache kukariri notisi vyuoni kufaulu tu. Hizo bachelor na masters za finance na CPA walipataje? Wana JamiiForums naomba ufafanuzi. Nimechoka leo nimeamini wasomi wetu wengi wako below standard.

Wote wameshindwa kujibu hilo swali na sifa za midigrii yao na CPA zao very sad.
 
Ila nae alietunga maswali dah. Okay, ndio Tanzania.

Mimi imebidi nigoogle maana nilidhania Simba (ndio maana jina wekundu wa msimbazi).

images - 2021-03-07T173731.738.jpeg
images - 2021-03-07T173736.540.jpeg
images - 2021-03-07T173747.942.jpeg
 
Aisee imeniuma walikuja wamelamba masuti na mitai shingoni, viatu vinang'aa sikuamini kwao kushindwa kujibu swali dogo kama hilo. Kuna tatizo sio kwenye elimu yetu lakini nadhani wasomi wetu wanakariri tu masomo na hawajui hasa wanasoma nini? Nimepata shock serious .Sijawahi maisha yangu yote kuwa shocked kiasi hiki.
 
Consultant aliyetoa hilo swali tulimbeza kuwa haliwezi saidia chuja waomba kazi lakini akasema take from me hilo swali litawabwaga, baada ya mjadala mrefu tukakubali libebe asilimia 70 baada ya ku conconvince. Na kweli consultant ka prove kuwa yuko right, Candidates 75 walioomba hakuna aliyepita kwa swali dogo tu hilo.
 
Hicho si kigezo mtu wangu cha maana sana kwanza unaijua vizuri hiyo course unayotamka? Acha ujinga
konda pamoja na kuzishika mia tano kila siku kuna siku nilimuuliza mia tano ina alama gani kwa nyuma akakosa. Je nichukue hicho ni kigezo hafai kuwa kondakta wa daladala?
 
Back
Top Bottom