Hivi inakuwaje gari ya rais inachomoka tairi?

Wameshapata gea ya kununua magari mengine...sasa hivi waagize VOGUE kabisa!
 
Hapo ndio inabidi Mr. JK aamke na kutafakari kwamba kazi alizotoa kwa kujuana katrika idara nyeti za ikulu na usalama wa taifa kwa watu ambao hawako qualified ndio itakula kwake mwenyewe mwishowe.

Tujuavyo kwa mtu nyeti na muhimu kama yeye, swala kama hili haliwezi tokea kamwe. Je wangekuwa speed 180 na tatizo litokee kama hilo ingekuwaje ati ? ?
 
hOGO

Tanzania imeshuhudia vituko vingi mwezi huu wa Mei,kutoka Rais Kikwete kutetea takrima hadi mtumishi wa Bwana Askofu Kilaini kudai kuwa Kikwete bado ni chaguo la Mungu,kutoka sakata la Masauni kufoji umri (oh Mungu, inawezekanaje?) hadi kifungo cha Liyumba (wengine wanadai alistahili kunyongwa kabisa).Na kutoka kauli ya Waziri Kombani kuwa daraja la mto Kilombero litajengwa katika awamu ya pili ya Kikwete (as if JK ameshashinda uchaguzi) hadi ajali ya gari la msafara wa JK.Makala hii inajaribu kuibua maswali kuhusu hili la mwisho,yaani ajali hiyo.Isome hapa Ajali Msafara wa JK: Ajali tu,Hujuma au Uzembe? | KULIKONI UGHAIBUNI
 
Nakumbuka 1987 ilitokea kwa Rais wa Nigeria.....hitirafu katika gari iliyombeba mkuu wa nchi!!

Nasisitiza binafsi naona ni hitirafu za kawaida, wengine mna uhuru wa kufikiri tofauti.

...B, kutoka 1987 had leo 2010 ni miaka mingapi?? zaidi ya miaka 24! Jambo linalotokea mara mbili tu katika Nusu karne haliwezi kuwa ni jambo la kawaida tu, Ndugu yangu. Na linapohusu usalama wa raisi aliye madarakani, ndio kabisaa halipaswi kuwa la kawaida! naunga mkono wote wanaosema tupunguze kurahisisha mambo jamani!!
Ingekuwa nchi za watu wanaojua kuwajibika, saa hizi kuna watu ambao vibarua vyao vingekuwa vimeishaota nyasi zamani lakini kwa kuwa hii ni nchi ambayo wafanyabiashara wanne wa madini wanaweza KUJIPIGA RISASI WENYEWE WAKAFA na hivyo kutokuwepo mtu wa kushitakiwa, anything can happen!
 
Kikwete chupuchupu

na Juma Kasesa (Tanzania Daima)


Aidha, akiwa hapo, Rais Kikwete alimnyanyua Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi na kumtaka aeleze kwa nini jiji linakabiliwa na uchafu, ambapo alizitupia mpira halmashauri kuwa ndizo zenye dhamana ya kuondoa uchafu na yeye hana mamlaka ya kuziagiza kusimamia.

Kauli hiyo ilionekana kumuudhi Rais Kikwete na kumuuliza Kingobi anataka apewe mamlaka gani ili aweze kuzisimamia halmashauri hizo na kumfanya mkurugenzi huyo kubakia kimya pasipo na majibu.

Sasa kwanini Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi hakufukuzwa kazi hapa?Napata mambo mawili hapa,it's either JK hajui majukumu ya mkurugenzi wa jiji na amemuuliza swali lisilomuhusu kabisa or Bakari Kingobi ndiye ambaye hajui kuwa moja ya jukumu lake ni kusimamia huo usafi wa jiji.Kazi kweli kweli!
 
Hapo ndio inabidi Mr. JK aamke na kutafakari kwamba kazi alizotoa kwa kujuana katrika idara nyeti za ikulu na usalama wa taifa kwa watu ambao hawako qualified ndio itakula kwake mwenyewe mwishowe.

Tujuavyo kwa mtu nyeti na muhimu kama yeye, swala kama hili haliwezi tokea kamwe. Je wangekuwa speed 180 na tatizo litokee kama hilo ingekuwaje ati ? ?

Sheikh speed 180 una maana 180km/hr ama?Maana najaribu kupata picha barabara ipi hiyo ya kuendesha kwa speed ya 180km/hr hiyo hapa D'salaam au hata nje ya D'salaam!Labda kama ndo mpango wa kumtoa maisha president!
 
Halafu kuwa gari la rais ambaye anaongoza vita ya ufisadi (at least ndivyo wanavyodai) linatumia gari ambalo tairi lake hadi uje na pampu inanifanya nijiulize kama bado tunazo kichwani au vipi? Sasa kama kungekuwa na mtu anataka kufanya kitu mbaya pale ingekuwaje?
 
NINAVYOSIKIA mimi ni kwamba idara ya magari ya Ikulu haiendeshwi na wataalamu wa fani husika bali mashushu wasiojua chochote kuhusu transport management.
Imefikia kiasi kwamba eti wanaenda kukodisha magari kwa matumizi ya Ikulu kwa watu binafsi. Maajabu haya jamani.
Tunawalaani na kuwalaumu wakoloni lakini baba wala babu hajawahi kunisimulia jambo hili kiutokea kwa magavana wakati wakitumia Ma-Ford na Morris Minor za miaka ile.
Kwa kweli ukizungukwa na watu wanaonuka kinyesi na wewe pia unaweza kutuhumiwa ni mchafu!! Maana kama utawala unaogusa mahala pa juu namna hii uko hivyo utawala huko wilayani na vijijini utakuwaje jamani?

Mheshimiwa ukirudi madarakani una kazi kubwa ya kupangua timu ya wasaidizi wasiokusaidia ili upat e wasaidizi watakaokusaidia.
 
NINAVYOSIKIA mimi ni kwamba idara ya magari ya Ikulu haiendeshwi na wataalamu wa fani husika bali mashushu wasiojua chochote kuhusu transport management.
Imefikia kiasi kwamba eti wanaenda kukodisha magari kwa matumizi ya Ikulu kwa watu binafsi. Maajabu haya jamani.
Tunawalaani na kuwalaumu wakoloni lakini baba wala babu hajawahi kunisimulia jambo hili kiutokea kwa magavana wakati wakitumia Ma-Ford na Morris Minor za miaka ile.
Kwa kweli ukizungukwa na watu wanaonuka kinyesi na wewe pia unaweza kutuhumiwa ni mchafu!! Maana kama utawala unaogusa mahala pa juu namna hii uko hivyo utawala huko wilayani na vijijini utakuwaje jamani?

Mheshimiw aukirudi madarakani tena basi una kazi kubwa ya kupangua wasaidizi wako ili kuwaondoa wasaidizi wasiokusaidia upate wasaidizi wanaokusaidia kikweli kweli na sio tu kutafuta hela za kirahisi kupitia bajeti ya Ikulu na masurufu ya safari.

Wasaidizi wazuri = rais mzuri vinginevyo no way!!!
 
Nimekua nikifuatilia kuhusu mushkeli katika magari ya msafara wa Rais.Ingawa mwanzo ilionekana au nililichukulia kwa mtazamo kamakichekesho au utani lakini baada ya kusoma uchambuzi wa rai mwema hapo chini naanza kujiuliza maswali lukuki.Kweli ajari zipo na zinatokea kwa sababu mbalimbali.Kudra ya mungu,uzembe,mjama na hujuma.ili la gari la Rais kama ingelikua mara moja na Ikulu kutoa ufafanuzi bila kuficha wala kujikanyaga tungeliamini.Lakini kwa nchi yetu hayo niliyoyataja juu inawezekana.Uzembe kwanaohusika akiwemo JK mwenyewe ni jambo la kawaida,ufisadi imekua ni jambo la kawaida kwa viongozi kwa kupokea rushwa kunua mitambo au vifaa au kusahini mikataba usiyo na kichwa wala miguu na kusababisha hasara na kupoteza maisha ya watu wakati mwingine hili sio siri.Kwa vile rushwa katika nchi yetu imekua ni mtaji kuanzi kwa JK mwenyewe sioni kama kutakua na ugumu kwa watu kutoa kitu kidogo kwa wahusika na kuyahujumu magari ya Mh.Rais.Au watu hata wafanyakazi wanaomzunguka Mh.Rais wamechoka na maamuzi yake au kutokua na maamuzi ya kutatua matatizo ya wananchi na makali na machungu ya maisha kwa walalahoi na hivyo kuamua kumuhujumu na kumuumbua.Kama uzembe,rushwa,UFISAADI kuzunguka maisha yake KATIKA Ikulu itakuaje katika serikali na nchi kwa ujumla MUNGU IBARIKI TANZANIA
Usalama magari ya Rais utata mtupu


Mwandishi Wetu
Mei 26, 2010
Mawili yapata mushkeli kwenye msafara
Mwandishi wa Kikwete asema dereva alisahau kuondoa gia
Adai tairi halikuchomoka, lilipata pancha
UTATA umeibuka kuhusu usalama wa magari anayotumia Rais Kikwete kufuatia tukio linalohusisha magari aliyotumia wakati wa ziara yake ya jiji la Dar es Salaam ya Jumatatu wiki hii ambapo moja lilipata matatizo ya tairi na jingine kuzima ghafla.

Wakati wa ziara hiyo, gari alilopakia Rais Kikwete lilizimika katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mavurunza, wilayani Kinondoni, eneo la Kimara Mwisho, saa 7:30 mchana, na hivyo kusababisha msafara wake kusimama kwa dakika tatu.

Kwa mujibu wa watu waliokuwa kwenye msafara huo, gari hilo lilizimika tena baada ya mwendo mfupi kutoka katika makutano hayo na kulazimu Rais Kikwete kuhamishiwa kwenye gari jingine la akiba kwenye msafara huo. Lakini gari hilo la akiba nalo lilipata tatizo la tairi maeneo ya BP barabara ya Kilwa, na Rais Kikwete, kwa mara nyingine, akahamishiwa kwenye gari jingine.

Akizungumza na Raia Mwema, Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga alisema kuwa katika tukio la kwanza dereva alishindwa kuondoa gia ya four wheel drive (4WD) mahsusi kwa ajili ya kuendesha kwenye barabara ya matope. Hata hivyo, Raia Mwema halikufanikiwa kumpata dereva huyo kuthibitisha hilo.

Premi alisema msafara wa Rais ulipita eneo lenye matope wilayani Temeke na kwamba ilimlazimu dereva kutumia gia ya 4WD lakini baada ya kutoka eneo hilo na kuingia katika barabara nzuri, dereva alighafilika katika kuondoa gia hiyo na gari kuwa zito.

“Dereva nadhani alighafilika na kushindwa kuondoa gia ya 4WD ili kuweka gia ya kawaida na kwa hiyo gari lilikuwa zito na ratiba ya Rais ilikuwa ndefu kwa hiyo ilibidi tu kubadilisha gari ili ratiba iendelee na ikamilike.”

Kuhusu tukio la Barabara ya Kilwa, Premi alisema kuwa gari la Rais lilipata pancha lakini baadhi ya watu wengine waliokuwepo katika msafara huo walidai kwamba kulikuwa na mushkeli mwingine na si pancha.

“Tulipokuwa sehemu nyingine gari ya Rais ilipata pancha na hilo ni tukio la kawaida kabisa”, alisema Premi
lakini alipoelezwa kuwa picha za gari hilo katka baadhi ya magazeti zinaashiria kuwa haikuwa pancha bali gurudumu liling’oka, alisema: “Pamoja na hayo, gari kupata matatizo kama hayo ya matairi si jambo geni na haina maana kwamba gari husika ni mbovu. Mimi nashangaa waandishi wanaandika masuala haya na kusahau mengine muhimu zaidi kwa wananchi….unaandika matatizo ya magari na kuacha masuala ya msingi kwa wananchi kama suala la maji?”, alihoji Premi.

Inaelezwa kuwa katika tukio hilo la msafara wa Rais kusimama ghafla eneo la Kimara, takriban dakika mbili zilitumika kwa maofisa wa usalama wa taifa kupata suluhu ya namna msafara huo utakavyoendelea kutokana na mkanganyiko wa gari ipi kati ya mbili zilizokuwa zinafanana aitumie Rais. Inaelezwa kuwa gari hilo la Rais lililoharibika eneo la Kimara lilisukumwa na watu waliokuwa pembezoni mwa barabara. Hata hivyo, baada ya dakika nane gari hilo aina ya Toyota Landcruiser VX V8 lenye rangi nyeusi, liliweza kuwaka.

Hata hivyo, Raia Mwema halikufanikiwa kumpata ofisa yeyote wa Ikulu kuzungumzia uimara wa magari hayo anayotumia Rais Kikwete, na kama yalifanyiwa ukaguzi wa kina kabla ya safari kama inavyopaswa kufanywa na mafundi wa Ikulu.

“Tairi kuchomoka na hata pancha kwa gari la msafara ama hata la mtu muhimu ni suala la kuangaliwa kwa makini sana maana kuchomoka tairi kunatokana na ama ubovu wa kitu katika mfumo wa tairi ama kutofungwa vyema, mambo yote hayo hayapaswi kutokea kwa gari la kiongozi yeyote si rais pekee,” anasema fundi magari aliyejitambulisha kwa jina la Hemedi.

Habari za ziara hiyo ya Rais Kikwete, jijini Dar es Salaam, kuingia dosari kutokana na mushkeli wa magari aliyoyatumia ambazo zilipamba kurasa za mbele za magazeti kadhaa, Jumatatu, zimeibua gumzo kubwa miongoni mwa wakazi wa Jiji. Jana Jumanne baadhi ya wakazi wa jiji walipiga simu Raia Mwema au kutuma ujumbe wa sms au e-mails kueleza hofu yao kuhusu usalama wa rais iwapo ataendelea kutumia magari hayo.

Magari hayo yanayotumika na Ikulu pamoja na viongozi wengine wa serikali ni ya gharama kubwa inayokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 150 pamoja na kuwa huwa na kawaida ya kufanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara na wakala wa magari ya Toyota Tanzania.
 
VX hizi sijui kama ni guard lakini kwa ninavyo fahamu mimi magari yake yale mengine yakijerumani huwa yana weight kubwa sana kwasababu ni armour plated na hata shock up zake ni nzito kama za ma-lorry. About the VX sina uhakika lakini the tires za zile benz na beemer huwa usalama wanaorder from Germany.. Sasa sijui lakini chances of 2 tyres going messy ni ndogo sana unless kama yalibandilishwa na hayakukazwa vizuri (and this happens quite a lot...japokuwa kwa Rais ni kitu ambacho ni uzembe wa ajabu)..
 
Gari ya Rais kuchomoka tairi halafu hakuna responce ya uwajibikaji? kweli laana imetukumba watanzania!!!!

Salva ameonesha dharau kubwa kwa mpigiwa kura wetu
 
Ninachompendea muungwana
hana tatizo ktk hili na hatochukua hatua labisaaaa maana analichukulia kama ajali tu.

Luhanjo anasemaje hapo?
 
Back
Top Bottom