Hivi inakuwaje gari ya rais inachomoka tairi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi inakuwaje gari ya rais inachomoka tairi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hassani, May 25, 2010.

 1. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hivi hazifanyiwi ukaguzi,au kulikuwa na mkono wa mtu?,jana rais JK ziarani dar,alibadilishiwa gari mara mbili,baada ya gari ya pili kubadilishwa ilitembea kidogo na kuchomoka tairi
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mbona uchumi wa nchi haufanyiwi ukaguzi kuna mkono wa mtu hapo?
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inakuwaje rais kupata kikohozi, hivi hana daktari wa kumchunguza? Hilo swali limekaa kiuchokozi, ingawa unataka kujua sababu zilizopelekea gari kuchomoka gurudumu. Hapo inabidi iundwe tume kuchunguza tukio hilo.

  Nadhani ni swala linalowezekana kama gari limetembea sana kwenye rough roads. Sio rahisi kuwa kila nut kuwa imepitiwa kukazwa sawa sawa. Hata hivyo kuna uwezekano wa manufacturer error.

  Hili swala la manufacturer error nimewahi kushuhudia gari jipya kabisa likiwa na piston moja haina mkono. Kweli kila mtu alistaajabu pale hiyo piston ilipopasua block.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  [​IMG][​IMG]:mad2::mad2:[​IMG][​IMG]
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Watumishi wa Ikulu na usalama wa taifa sio makini kabisa kwani ni matukio mengi tu ya uzembe yamekwishatokea kwa JK. Kwa sababu gari kwanza limezimika pili kuchomoka tairi. Sasa atarajie kula nyoka au kenge! Kama liliwekewa 'studs' za Taiwan ni rahisi kuchomoka kwani gari ikienda mwendo mrefu zinachemka na kuyeyuka.

  Basi weekend hii lazima utaona msafara wake ukienda Bagamoyo aidha kwa kupitia Morogoro road au Old Bagamoyo road.
   
 6. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mkuu anatumia Toyota Vx siku hizi Toyota wanavurunda magari yao wamesha zua matatizo makubwa kwenye magari yao
   
 7. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Mh Mkaa Mweupe! Ina maana kwa kidistance cha kutoka IKULU to KIMARA,tena lami tupu inaweza kuwa sababu?,kama ilishatembea huko siku za nyuma sawa,basi nna shaka kama hizo gari zinafanyiwa service kabla ya ziara yoyote ya rais.Rais ni kiongozi wa nchi ambaye kutokana na sababu za kiusalama gari yake inatakiwa ihakikishwe kabla haijaipanda.
   
 8. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2010
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  du hii kweli kali, yani mara mbili!! aaaa bana mkono wa m2 nini? lakini wale usalama vp, the way walivyo serious kumbe...! mwe..
   
 9. Mgoneke

  Mgoneke Member

  #9
  May 25, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini ni ajali kama ajali nyingine zinavyotokea,ile ni gari anytime anything can happen
   
 10. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani gari ya Rais ina tofauti gani na Toyota Nadia ya my wife wangu mpaka isichomoke tairi??

  Gari ya Rais kama gari lingine lolote lile linaweza kupata hitirafu.......so to me hii sio issue kabisa!!!
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  this is so awkward. someone has to be responsible.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi huyo JK si yuko ziarani hapo Darisalama? Nilitegemea mambo kama haya kutokea huko madongokwinama ambako barabara za lami zitakuja in 2099.
   
 13. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  I suppose ur wife is not a president of United Republic of Tanzania
   
 14. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na hapo barabara zilichongwa usiku kucha, je kama wasingechonga ingekuaje? Magari ya kichina nini?
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Thanx for informing us that your wife has a car -- whoever you are! But it becomes all different if the Prez's car gets a miushap -- worse if it's two mishaps in a row. Presidents' cars are carefully looked after than your wife's car. You know -- conspiracy theories etc...!

  Mwanamayu: Do you mean he will go to Bagamoyo to enforce the charms? Could be that they are weakening up -- or someone's are becoming stronger! - kwi... kwi... kwi...
   
 16. M

  MJM JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  sure
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kikwete chupuchupu

  na Juma Kasesa (Tanzania Daima)

  RAIS Jakaya Kikwete amenusurika kupata ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kulegea gurudumu na kisha kung'oka muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kuteremka katika gari hilo kwa dharura wakati akiwa ziarani jijini Dar es Salaam.

  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9:15 katika Barabara ya Kilwa maeneo ya karibu na zilipo ofisi za makao makuu ya kampuni ya mafuta ya BP.

  Kabla ya tukio hilo, msafara wa Rais Kikwete ulisimama ghafla na rais akahamishwa kutoka katika gari hilo aina ya Land Cruiser VX na kwenda katika gari jingine.

  Watu walioshuhudia tukio hilo walilieleza Tanzania Daima kuwa, muda mfupi baada ya msafara wa rais kuendelea na safari, dereva wa gari alilohama rais alijaribu kulisogeza pembeni ya barabara, hatua iliyosababisha gurudumu la gari hilo kung'oka na kusababisha ligote chini upande wa mbele kulia.

  Tukio hilo liliwashtua watu waliokuwa katika eneo hilo, ambao walianza kujadili ni nini kingetokea iwapo gurudumu hilo lingeng'oka wakati rais akiwa ndani ya gari hilo.

  Mwandishi wa gazeti hili aliyekuwapo eneo la tukio alieleza hatua hiyo ilisababisha kuwasili katika eneo hilo kwa gari maalum la kubeba magari mabovu maarufu kwa jina la ‘breakdown'.

  Tukio hilo la rais kulazimika kuhama kutoka katika gari alilokuwa amepanda lilikuwa ni la pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza akiwa katika maeneo ya Kimara Mavurunza.

  Kikwete alikuwa katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi ya maji jijini Dar es Salaam.

  Msafara huo ukiwa unaondoka Kimara ulisimama ghafla na kuzua taharuki kwa maofisa usalama na wananchi baada ya kuona Rais Kikwete akishushwa ndani ya gari alilokuwa amepanda na kuingia katika gari jingine baada kupata hitilafu huku mvua kubwa ikinyesha.

  Tukio hilo la rais kushushwa katikati ya barabara ya Morogoro katika eneo hilo, lilichukua dakika nane na kusababisha msongamano wa magari kabla ya msafara huo kuruhusiwa kuendelea kuelekea Chang'ombe Toroli ambako alikuwa akienda kukagua mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na mashirika ya maji Dar es Salaam.

  Tanzania Daima ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, alikiri kutokea kwa matukio mawili tofauti yaliyosababisha rais alazimike kuhamishwa kutoka katika magari aliyokuwa amepanda.

  "Ni kweli matukio hayo yalitokea, katika tukio la kwanza gari alilopanda lilipata hitilafu baada ya gea kugoma kubadilika wakati katika tukio la pili, gari alilopanda lilipata pancha," alisema Rweyemamu.

  Alipoulizwa kuhusu taarifa za gari la pili kung'oka gurudumu hata kusababisha kuitwa kwa gari la kubeba magari mabovu, Rweyemamu alikanusha habari hizo na akasema hazikuwa sahihi.

  "Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyopata rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika Jiji la Dar es Salaam?" alihoji Rweyemamu.

  Mwandishi wa habari hizi alimweleza Rweyemamu kuwa, gazeti hili liliona umuhimu wa suala hili kwa kuwa lilikuwa likigusa usalama wa kiongozi mkuu wa nchi moja kwa moja.

  Jibu hilo lilisababisha Rweyemamu amuombe mwandishi afuatilie kuhusu ukweli wa taarifa hizo na ndipo baada ya muda usiozidi dakika 30 alipiga simu chumba cha habari na kulihakikishia Tanzania Daima kuwa hitilifu za magari alizokabiliana nazo Rais Kikwete zilikuwa ni za kawaida.

  Akiwa katika ziara hiyo jana, Kikwete alishuhudia wananchi wakiwabana kwa malalamiko na wakati mwingine kuwazomea maofisa watendaji wa Shirikika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) na Mamlaka ya Maji Safi jijini Dar es Salaam (DAWASA).

  Kufuatia hali hiyo ya kuzomewa katika eneo la Kimara, Rais Kikwete na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya kwa nyakati tofauti walilazimika kuingilia kati na kutoa ufafanuzi kwa wananchi waliokuwa wakiwabana kwa maswali maofisa hao wa Dawasa na Dawasco.

  Ofisa Mtendaji wa Dawasco, Alex Kaaya na Archad Mutalemwa wa Dawasa walikumbana zahama hizo baada ya diwani wa kata hiyo kuanika kero ya upatikanaji wa maji inayowakabili kwa muda mrefu na hivyo kumlazimu Rais Kikwete kuwataka watoe majibu.

  Ziara hiyo ilianzia kwa Kikwete kutembelea Makao Makuu ya Dawasco ambapo alipata fursa ya kupata maelezo ya utendaji wa mashirika hayo kuhusu kero ya upatikanaji maji jijini Dar es Salaam.

  Akiwa hapo alielezwa na maofisa hao hatua zilizochokuliwa na mashirika hayo katika kuondoa kero hiyo kwa kuanzisha miradi wa uchimbaji visima, ikiwamo kuhakikisha wanavikarabati vyanzo vya maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuondoa tatizo hilo.

  Kaaya alisema tatizo linalosababisha kero ya maji jijini ni uchakavu wa miundombinu, upotevu wa asilimia 50 ya maji, njiani na miundombinu iliyokuwapo sasa kutoendana na ongezeko la idadi ya watu.

  Alisema miundombinu iliyopo ilijengwa mwaka 1976 na ilikuwa inatosheleza kwa wakati huo tofauti na sasa ambapo Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wanaofikia milioni saba.

  Naye Mutalemwa akitoa ufumbuzi wa tatizo la maji jijini, alisema wanatarajia kuanzisha mradi wa uchimbaji visima Julai mwaka huu, na kubainisha kuwa wamejipanga ifikapo mwaka 2013 tatizo la maji liwe limekwisha jijini.

  Aidha, akiwa hapo, Rais Kikwete alimnyanyua Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi na kumtaka aeleze kwa nini jiji linakabiliwa na uchafu, ambapo alizitupia mpira halmashauri kuwa ndizo zenye dhamana ya kuondoa uchafu na yeye hana mamlaka ya kuziagiza kusimamia.

  Kauli hiyo ilionekana kumuudhi Rais Kikwete na kumuuliza Kingobi anataka apewe mamlaka gani ili aweze kuzisimamia halmashauri hizo na kumfanya mkurugenzi huyo kubakia kimya pasipo na majibu.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliagiza kujengwa kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Mavurunza hadi Segerea ili kupunguza kero ya usafiri.

  Baada ya ziara hiyo, Rais Kikwete alikutana na viongozi wa Jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee na kuwataka kusimamia ipasavyo majukumu waliyopewa.
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hakiyamungu huyu bwana nilishasema siku nyingi ameingiza wahuni ikulu,pale kuna watoto wa kijiweni watamtoa roho.kwanza ratiba hazina mpangilio,hotuba za kubumba,sasa kwenye tairi wakifika kwenye msosi mi sipo.2010 tutafute presdaa mwingine.
   
 19. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hayo ni majibu ya maombi ya wafanyakazi na familia zao. Kisasi ni juu ya Mungu na yeye atalipa kwa wakati wake.
   
 20. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  kaka karibu,jukwaani
   
Loading...