Hivi inakuajekuaje kati ya mamilioni ya watu, unaibuka kupata bahati ya kuwa Rais wa Nchi?

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Bado najiuliza ni bahati iliyoje kati ya mamilioni ya watu MTU mmoja tuu unapata bahati ya kuwa rais wa Nchi,cheo ambacho unaweza kuwataka watu wote wasitoke majumbani,ukiagiza ghorofa lijengwe linajengwa japo litachelewa,

Mliosoma history za viongozi mtujuze makuzi ya watu hawa huwa yakoje mpaka kupata bahati hii kubwa.
 
Kuna kujichanganya na watu, na pia kujipambanua miongoni mwa watu.
Kujichanganya, kunasaidia hasa hatua za mwanzo au za chini, mfano ubunge n.k.
Kujipambanua ni pale uko miongoni mwa wengi ambao mnajichanganya na jamii, ila wewe ukaonesha utofauti, juu ya mtazamo, utendaji n.k. ukawavutia wanaoteua au wanaopendekeza, hivyo ukawazidi wengine.
Vya ziada ni bahati, kuyasoma mazingira na kuyatumia ili kukuinua.
 
Bado najiuliza ni bahati iliyoje kati ya mamilioni ya watu MTU mmoja tuu unapata bahati ya kuwa rais wa Nchi,cheo ambacho unaweza kuwataka watu wote wasitoke majumbani,ukiagiza ghorofa lijengwe linajengwa japo litachelewa,

Mliosoma history za viongozi mtujuze makuzi ya watu hawa huwa yakoje mpaka kupata bahati hii kubwa.
Wengi huwa hawajui kama siku moja watakuja kuwa marais, ila jinsi maisha, siasa na kazi zinavyoenda ndio mtu anakuja kuona, kumbe na mimi naweza kujaribu hii kazi.

Right place, right time, right people na bahati muhimu.
 
Mkuu umejiuliza swali ambalo nimewahi kujiuliza mara nyingi sana, katika kutafakari nilihitimisha kwamba lazima kunakuwa na nguvu ya ziada (extra ordinary power) ambayo kibinadamu unaweza kosa namna ya kuielezea. Taifa kama la Tanzania lina watu zaidi ya mil 55 na ndani ya watu hao kuna kuna wenye akili nyingi sana, wasomi wakubwa sana, wajanja wengi kadhalika na kadhalika. Kwa nini iwe huyo na si yule?
 
Pamoja na yoote lakini BAHATI inahusika. Mataifa yaliyoendelea wanataratibu ngumu na michujo mikali sana hadi mtu kupenya na kua kiongozi wa nchi ili wampate the best in all angles. Unapimwa uzalendo wake, usafi wake kwenye utendaji na hata maisha binafsi, uelewa wake kwenye nyanja za kisiasa, uchumi hata kimataifa, haiba yake na hata uwezo wa kuongea na kuwasiliana na umma

Kuna vigezo vingine havijaandikwa wala havisemwi bali ni kama utamaduni. Kwa mfano US wanataka Rais awe na urefu wa kuanzia kimo fulani. Hawataki Rais wao awe mfupi, na vigezo vingine kibao
 
Mathayo sura ya 2
1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Nukuu hiyo hapo juu, si inajielezea, au niongeze sauti(nifafanue)?
 
Sio kweli Mkuu Marekani imewahi kuwa na marais wafupi, Lakini Kuwa active katika siasa haikupi guarantee ya ku ukwaa URAIS Msome trump hajawahi kuwa hata governor wala Senator kiufupi jamaa hana Background ya kuwa active politician ila Still ameukwaa URAIS, Hilary Clinton ambaye amekuwa FLOTUS na Secretary of states mbona aliangushwa na mtu ambae hajawahi kuwa Hata senator
 
Hiyo ni mipango yake Mola Maulana

Ukitafakari Mzee Mwinyi alipataje Urais wa Znz na Tanzania utashangaa sana tena mbele ya Magwiji

1977 anajiuzulu uwaziri,

1983 anarudishwa Nyumbani toka Ubalozini Misri anakuwa 'Baba wa Nyumbani' kwa miezi 11 hadi anatokea Mlemavu wa macho a.k.a Kawawa wa Znz (Sheikh Thabit Kombo) Katibu mstaaf wa ASP anaombwa ushaurh na MWL Nyerere nani amrithi Jumbe …nae anamtaja Ally

MWINYI KATOKEA BENCHI
 
Mathayo sura ya 2
1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Nukuu hiyo hapo juu, si inajielezea, au niongeze sauti(nifafanue)?
Due upo deep
 
Hii kitu ni kweli kabisa
Akawa pia Mkuu wa Udsm ile ya wabishi kina Prof Chachage

Jitihada haishindi Qadar

Watu kama Seif Sharif,Malecela,Gharib Bilal,Lowasa bado hawaamini kama wangezeeka bila ya ving'ora
Tunatakiwa kuweka juhudi na maarifa kweny kila jambo

Ila kudra nyota (bahati) tumepishana ila kila ana time yke ni kama Jamaa mmoja wa marekani ali hastle kuupata urais ila time ilivo fika akafanikiwa.
 
Mathayo sura ya 2
1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Nukuu hiyo hapo juu, si inajielezea, au niongeze sauti(nifafanue)?
Ndio mkuu, Ifafanue vizuri
 
Wakati mwingine ni BAHATI MBAYA tu! Mfano mzuri ni huyu wa kwetu. Aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa ajili tu ya kujaribu!
Hakuwa na uhakika wa kushinda, kutokana na ukweli kwamba ushindani ulikuwa ni mkubwa, na waliojiandaa mapema mfano Lowassa na Membe walijadhatiti zaidi kuliko yeye!

Lakini ghafla akajikuta AMESUKUMIZWA ndani na kuwa Rais.
 
Moja ya swali la kufikirisha sana. Wala sio tu urais.. Mamlaka yoyote yale ya uongozi, hata viongozi wakubwa ma CEO wa makampuni makubwa.

Ukitafakari sana, unakuta ni watu wa kawaida sana, lakini wameweza vipi kupata madaraka.

Kuna wadau hapo juu wamesema ni Nyota na Bahati na mimi nakubaliana nao mia kwa mia.

Ila pia Nyota na Bahati haitoshi, kuna ile ambition ndani ya moyo wa mtu lazima iwepo.

Ambition ndio inavuta bahati na nyota.
 
Bado najiuliza ni bahati iliyoje kati ya mamilioni ya watu MTU mmoja tuu unapata bahati ya kuwa rais wa Nchi,cheo ambacho unaweza kuwataka watu wote wasitoke majumbani,ukiagiza ghorofa lijengwe linajengwa japo litachelewa,

Mliosoma history za viongozi mtujuze makuzi ya watu hawa huwa yakoje mpaka kupata bahati hii kubwa.
Wengi hasa Afrika wanatumia njia zile chafu za kienyeji na kuna mambo mabaya mno nyuma ya pazia usiombe.
 
Back
Top Bottom