Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Si kwa viongozi tu bali hata kwa wafuasi wa upinzani hususani Chadema wengi muda wote wamekuwa ni wenye hasira na jazba kwa jambo lolote. Wao wamejipa hatimiliki ya 'akili' , yaani 'wanajitambua'. Mara kwa mara majibu au michango ya walio wengi hutoa kwa jazba na hasira kali, hata bungeni wabunge wengi wa upinzani mfano akina Msigwa nk wakianza kuongea lazima wakaze shingo huku wakirusha mikono hewani, je hii inasaidia kueleweka? au inaongeza maana?
Nilikuwa nauliza tu wajameni, nini haswa mantiki ya hasira na jazba kutoka viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani?
Nilikuwa nauliza tu wajameni, nini haswa mantiki ya hasira na jazba kutoka viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani?