Hivi ili kiwango cha elimu nchini kiongezeke tunahitaji matamko?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
809
Wajuzi nisaidieni kunipambanulia hili la elimu yetu ya Tanzania na uelekeo wake.

Mwanzoni mwa utawala wa Magufuli baada ya uteuzi wa baraza la mawaziri na kuona limesheheni pHDs na maprof nilifikiria sasa mambo yanaenda kuwa sawia nchini mwetu maana baraza limejaa wasomi kama Spika wetu anavyojidai na bunge lake.

Wizara ya elimu ikapata profesa, sasa nimekuwa nikifuatilia sana utendaji wa profesa huyu kwa kuinua elimu au kuweka sawa wizara hii.
Kumekuwepo vitu vingi vingi ambavyo binafsi nashindwa kuelewa ni katika kuinua elimu au ndo matamko ambayo yamekithiri katika awamu hii....Kuna wakati tuliambiwa kuwa elimu ya msingi itaishia darasa la sita na vitabu vikachapishwa na kupelekwa mashuleni, mara ghafla likapotelea hewani, mpaka leo hatujawahi kuambiwa officially kama lilifutwa au lipo laja,japo tulisikia lilifutwa na vitabu kutolewa mashuleni.

Majuzi imetolewa tena kali ya mwaka, hii ni kuhusu msomi anaesoma Diploma kutotambulika tena....Nasema kutotambulika sababu huwezi kujiunga na digrii kama umepitia diploma kwanza, yaani ukimaliza kidato cha nne uanze na certificate,diploma na kujiunga na digrii kama zamani. Au kama ufaulu wako hauruhusu digrii moja kwa moja umalizapo kidato cha sita ukianza na diploma ndo basi hapo ni mwisho wako.
Nilivyosikia hii ni kwa sababu ya kuinua kiwango cha elimu,yaani ilionekana digrii holders kiwango kinakuwa chini.

Sasa nikafikiria sana, sijui wamefanya research wapi na lini ili kuja na huo mpango wao. Nikafikiria tu kwa haraka haraka digrii holders ninaowafahamu,waliopitia cert,dipl,digrii hadi pHD na waliopata credit za kuwaruhusu baada ya kidato cha sita.

Kuna Prof mmoja namfahamu tena yuko vizuri sana na alianza na diploma,na leo niandikavyo ni prof na tena ni msaidizi wa mkuu wa chuo kikuu kimojawapo hapa nchini, na yuko vizuri mno. na kuna hao waliopata ufaulu wa kuwaruhusu kujiunga na digrii moja kwa moja lakini hata ukijaribu kufanya nao usaili,wako hoi mnooo.
Binafsi sijaelewa hili nalo linahusiana vipi na kuinua elimu yetu/
imefikia wakati mtu mpaka unajiuliza, hivi hawa maprofesa ni kweli wanafaa kupewa wizara au ni kwamba wanafaa sana kuwa vyuoni ili waendelee kufanya research, hata tukiangalia mawaziri wote ambao ni maprof hawachapi kazi sawa na wenye digrii moja au masters.
ni wazo langu naruhusu kukosolewa.
 
Wajuzi nisaidieni kunipambanulia hili la elimu yetu ya Tanzania na uelekeo wake.
Mwanzoni mwa utawala wa Mh JPM baada ya uteuzi wa baraza la mawaziri na kuona limesheheni pHDs na maprof nilifikiria sasa mambo yanaenda kuwa sawia nchini mwetu maana baraza limejaa wasomi kama Spika wetu anavyojidai na bunge lake.
Wizara ya elimu ikapata profesa, sasa nimekuwa nikifuatilia sana utendaji wa profesa huyu kwa kuinua elimu au kuweka sawa wizara hii.
Kumekuwepo vitu vingi vingi ambavyo binafsi nashindwa kuelewa ni katika kuinua elimu au ndo matamko ambayo yamekithiri katika awamu hii....Kuna wakati tuliambiwa kuwa elimu ya msingi itaishia darasa la sita na vitabu vikachapishwa na kupelekwa mashuleni, mara ghafla likapotelea hewani, mpaka leo hatujawahi kuambiwa officially kama lilifutwa au lipo laja,japo tulisikia lilifutwa na vitabu kutolewa mashuleni.
Majuzi imetolewa tena kali ya mwaka, hii ni kuhusu msomi anaesoma Diploma kutotambulika tena....Nasema kutotambulika sababu huwezi kujiunga na digrii kama umepitia diploma kwanza, yaani ukimaliza kidato cha nne uanze na certificate,diploma na kujiunga na digrii kama zamani. Au kama ufaulu wako hauruhusu digrii moja kwa moja umalizapo kidato cha sita ukianza na diploma ndo basi hapo ni mwisho wako.
Nilivyosikia hii ni kwa sababu ya kuinua kiwango cha elimu,yaani ilionekana digrii holders kiwango kinakuwa chini.
sasa nikafikiria sana, sijui wamefanya research wapi na lini ili kuja na huo mpango wao. Nikafikiria tu kwa haraka haraka digrii holders ninaowafahamu,waliopitia cert,dipl,digrii hadi pHD na waliopata credit za kuwaruhusu baada ya kidato cha sita.
Kuna Prof mmoja namfahamu tena yuko vizuri sana na alianza na diploma,na leo niandikavyo ni prof na tena ni msaidizi wa mkuu wa chuo kikuu kimojawapo hapa nchini, na yuko vizuri mno. na kuna hao waliopata ufaulu wa kuwaruhusu kujiunga na digrii moja kwa moja lakini hata ukijaribu kufanya nao usaili,wako hoi mnooo.
Binafsi sijaelewa hili nalo linahusiana vipi na kuinua elimu yetu/
imefikia wakati mtu mpaka unajiuliza, hivi hawa maprofesa ni kweli wanafaa kupewa wizara au ni kwamba wanafaa sana kuwa vyuoni ili waendelee kufanya research, hata tukiangalia mawaziri wote ambao ni maprof hawachapi kazi sawa na wenye digrii moja au masters.
ni wazo langu naruhusu kukosolewa.
Nchi ya matamko, mtu akilala akiamka tamko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom