Hivi ikiwa mdaiwa ameshindwa kulipa deni baada ya muda uliopangwa na mahakama nini kinafuata na ikiwa mdaiwa hana mali yoyote.

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
668
1,000
Mnaojua sheria maomba msaada katika hili. Nilikuwa na kesi ya wizi na kukabwa mtaani, kesi iliisha kwa mtuhumiwa kufungwa miezi sita kwa kila kosa, kwa makosa mawili au kila kosa fine ya Tsh. 150,000/= ambayo mkosaji alilipiwa. Vilevile alitakiwa kulipa fedha alizochukua wakati wa tukio na simu aliyochukua jumla ikiwa 2,750,000/=.

Tangu ipite hukumu huu ni mwezi wa 5 na sioni dalili kama atalipa ndani ya miezi 6 aliyotakiwa na mkosaji hana mali za thamani ya fedha anazopaswa kulipa. Swali langu kwenu wanasheria, ikiwa muda umeisha na hajalipa ni nini kitatokea kwa mkosaji au napaswa nifanye nn ili niipate haki zangu?Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheremaya

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
2,871
2,000
Huyo aliekukaba hakuwa na wadhamini?

Kesi ilifunguliwa ni madai au jinai?

Makubaliano ya kulipana ilikuaje kwamba atakua anapeleka pesa mahakamani au atakulipa wewe mwenyewe..

Kama ni madai amini ukimfunga,akiwa gerezani itakupasa uwe unampelekea chakula,

Ikipita muda hajakulipa hata kidogo nenda mahakamani kakaze hukumu...

Mimi sio mwanasheria nawachokoza tu wenye fani yao waje kujibu kisomi zaidi
 
Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,595
2,000
Kinachotakiwa kufuata ni kufuta deni, kifupi unasamehe na kusahau kama kuna unaemdai. Samehe saba mara sabini.
 
Shukrani
Kesi ilifunguliwa ya Jinai.
Makubaliano ni kwamba hela atalipa mahakamani.
Nashukuru kwa ushauri, jana nimefika na nilipatiwa barua ya kumwita mahakamani. Tarehe 1/2 nitakupa mrejesho.
 
Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
668
1,000
Kinachotakiwa kufuata ni kufuta deni, kifupi unasamehe na kusahau kama kuna unaemdai. Samehe saba mara sabini.
Ni kweli mkuu ila nimeshavua nguo acha tu maji nioge, niliumia sana na kila nikikumbuka manyuzi niliyo shonwa nakosa kabisa usamehefu. Labda mungu aniongoze upya.
 
lendanai

JF-Expert Member
Oct 19, 2014
296
250
Huyo aliekukaba hakuwa na wadhamini?

Kesi ilifunguliwa ni madai au jinai?

Makubaliano ya kulipana ilikuaje kwamba atakua anapeleka pesa mahakamani au atakulipa wewe mwenyewe..

Kama ni madai amini ukimfunga,akiwa gerezani itakupasa uwe unampelekea chakula,

Ikipita muda hajakulipa hata kidogo nenda mahakamani kakaze hukumu...

Mimi sio mwanasheria nawachokoza tu wenye fani yao waje kujibu kisomi zaidi
Mkuuu hapo unakaza hukumu na watakao beba mzigo ni wadhamini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom