Hivi ICC ni kwa waafrica na ulaya mashariki tuu,mbona G.W.Bush yeye haitwi huko. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ICC ni kwa waafrica na ulaya mashariki tuu,mbona G.W.Bush yeye haitwi huko.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by commonmwananchi, Apr 6, 2011.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Wana JF,naomba niwe wazi.USA imevamia na kuua wairaq wasio na hatia,Israel imewaua walebanon wasio na hatia,Israel imeuwa wapalestina pale gaza ikiwa pamoja na kupiga mahospitali makombora,sijasikia neno ICC au NATO.na sasa wakoloni wameungana kumpiga GHADAFI kutaka mafuta yake kwa uongo wa kuwaonea huruma raia wa libya.haohao walimuua LUMUMBA,Je haki ipo hapooo???.......
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Mbona hauulizi kwa nini nchi chache tu ndio zina kura ya VETO?
   
 3. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo itakapofika zamu yetu kwa ajili ya maliasili zetu we waona poa tu sio?,
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Hicho kinachoitwa UN'o na hiyo ICC ni viini macho tu vya kufunga midomo, mikono na miguu ya wadogo ili WAKUBWA WAENDELEE KUNYONYA NA KUIBA RASILIMALI ZA DUNIA bila kubughudhiwa.

  WAPO WANAODHANI, KWAMBA WAKUBWA WALE WANATUTAKIA MEMA NA WANATUPENDA!

  INGELIKUWA WAKUBWA WALE KWELI WANAPENDA HAKI NA WATU WASIUWAWE MBONA HAWAKUISHAMBULIA CUBA ILI KUMTOA FIDEL CASTRO WASIEMTAKA KWA MIAKA KIBAO?

  INGELIKUWA WAKUBWA WALE WANAJUA KUKEMEA DHIDI YA MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA, LINI MLISIKIA NATO AU BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIKIKEMEA AU KUITISHIA ISRAEL KUWA ITASHAMBULIWA KWA KUKAIDI AMRI AU KUZUIWA ISIWAUWE WAPALESTINA!?

  HAKI ISIPOSIMAMIWA NA SISI WENYEWE HAITOLETWA NA JIRANI ASIYETUPENDA, LAZIMA TUJITAMBUE KWANZA, LAZIMA TUACHE KUNYENYEKEA WEZI NA MAFISADI, LAZIMA TUWE NA UCHUNGU NA VYETU, BILA HVYO TUTATAWALIWA NA VIBARAKA MILELE.

  MAENDELEO YANALETWA NA SISI WENYEWE NA SI VINGINEVYO. HATUTALETEWA MAENDELEO KUTOKA NJE NA KAMA TUNATARAJIA HIVYO BASI TUTEGEMEE KUWA TEGEMEZI MILELE.

  NA ANAETAKA KULETA MAENDELEO AJUE NYUMBA INAJENGWA NA WALIOPO...

  huwa nashangaa sana WAKUBWA WALE WAKISEMA WANATAKA DUNIA IWE MAHALA SALAMA PA KUISHI HUKU MATENDO YAO YAKIASHIRIA DHAHIRI KUWA DUNIA SI MAHALA SALAMA PA KUISHI!!
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,043
  Likes Received: 3,069
  Trophy Points: 280
  Mkuu ungeuliza hvi: kwanini US.A si mwanachama(haikuridhia) mkataba wa ICC kama ilivyo kwa nchi zingine? Jibu la swali ndo linajibu swali lako la kwa nini ICC inaonekana inawajibika kwa baadhi ya maeneo na si duniani kote?
   
 6. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Duniani hakuna haki absolutely, HAKI IKO MBINGUNI!
  Hapa duniani haki yako utaipigania mwenyewe na ukitegemea wengine wakusaidie hutaipata.
  Mara nyingi wanaojidai kutetea haki za wengine wanaangalia maslahi yao kwanza.
  Tatizo kubwa la Afrika hasa weusi ni utegemezi kwa nchi tajiri kwa sababu tu ya utumwa wa fikra ambalo Gadafi ameonekana kupinga na ili Afrika inyonywe vizuri lazima watu kama Gadafi waondolewe madarakani.
   
Loading...