Hivi huyu vc wa university of dsm ana watoto kweli....................?

Kwenye moja yakauliza profesa alisema madai ya wanafunzi niya msingi.! Sasa iweje leo aje kuwageuka nakuwafukuza chuo.? Maana mgomo umesaidia watoto wawakulima na wawindaji waliokuwa wamekosa mkopo kupata.! Ww unaesema maamuzi ya profesa ni sawa dhambi hii pia na ww itakutafuna.!
 
Yule amesoma politiko sayansi!
So anajua porojo,ukimckiliza lazima umuamin
Kwenye moja yakauliza profesa alisema madai ya wanafunzi niya msingi.! Sasa iweje leo aje kuwageuka nakuwafukuza chuo.? Maana mgomo umesaidia watoto wawakulima na wawindaji waliokuwa wamekosa mkopo kupata.! Ww unaesema maamuzi ya profesa ni sawa dhambi hii pia na ww itakutafuna.!
 
Jamani tusidanganyane hapa, ukweli ni huu:-

1. Katika matatizo yote uongozi wa DARUSO ya Mh. Kilawa ulijitahidi sana kutatua matatizo kwa diplomasia ambayo kwa namna moja ama nyingine ilifanikiwa kwani waliokua lupango waliachiwa kwa udhamini wa chuo chini ya sahihi za uongozi huo, pili wale waliosimamishwa masomo kwa muda walipewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, wale walikutwa na makosa na BARAZA la chuo liliagiza 8 wasimamishwe kwa miezi tisa na wengine 35 wasimamishwe hadi kesi zao zitakapofungwa lakini ni Kina Kilawa na wenzie walioshinikiza Utawala kuridhia hao 35 waendelee na masomo huku DARUSO ikifanya juhudi za kufuta kesi hizo mahakamani wakisaidiwa na Mwanasheria wa Chuo nalo lilifanikiwa baada ya kikao cha takribani masaa 6 kati ya Kilawa (Rais), Mustafa (Waziri Mkuu) na mwenyekiti wa DARUSO Board. Katiak Kiako hicho kinasa sauti changu kilifanikiwa kumnasa Mh. Kilawa akaiomba hata hao 8 wawekwe kwenye kundi hilo lakini Prof. Mukandala akasema ni rahisi ili tuanze na ho 35 kwanza ili tusionekane kunaenda kinyume na maamuzi ya BARAZA na kamati ya nidhamu.

2. Siku ya jumatatu 12/12/2011 jopo ya wajanja saba tu (nawaita wajanja maana waliingia Yombo 4 kukiwa na wanafunzi zaidi ya 700 lakini wote walitimua mbio) lilianzia revolution square na kupita likiwachapa wenzao kulazimisha waungane nao wakitumia kigezo cha boom ili wapate wafuasi wa kutosha. In a mean time kundi lilikua kubwa na kwa ushawishi wa alshabab (mabirika mawazo) wahandisi nao walijiunga kwa nia ya kupata boom na siyo nia ya wenzao kurudi kama ajenda ya alshabab na wenzie Mesaya (UDBS) na Laizer (SoL) ilivyokua. Ikumbukwe kuwa kundi hili liliondoa matangazo yote yaliyowekwa jumamosi na jumapili na uongozi wa DARUSO na Utawala ili kufunika ajenda yao binafsi ambayo kwangu naona ndicho kilichowapeleka hapa tulipo. Baada ya kukusanyika utawala mabirika, laizer na mesaya kwa ujanja ili baadae wapate kutimiza azma yao waliomba ridhaa ya kuonana na uongozi ambapo bila ajizi ofisi ya VC ilikubali kuonana nao na baada ya maongezi ya kama dakika 25 walirudi na majibu yaleyale yaliyokwishatolewa na DARUSO ila walitoa uongo wa kuwa utawala unaaalika wale 8 waende kwa mazungumzo ambako hakukua na makubaliano hayo. Pia Mabirika mawazo na wenzie pale kwa vc wlitaja majina ya uongo.

3. Wale wote 8 waliosimamishwa masomo kwa miezi tisa walikubaliwa kwa moyo mmoja kusikilizwa na Prof. Muakndala (ambaye mnafiki mmoja hapo juu aliyesema atamlisha sumu, chuki binafsi) aliwajulisha hawa vijana kuwa hawaijui vyema sheria zao na kuwaelekeza namna ya kujidefend kwa kuandika barua za appeals huku wakiendelea na masomo, kiukweli ni kwamba hii ni kama unamwibia mtu alafu huyohuyo anakufundisha namna ya kumshinda mahakamani!!!!!!!!!!!!! wote walivyorudi chini kama muda wa saa 1.00 jioni walwaeleza wenzao matokeo na kwamba mpaka muda huo madai yao yote yameshatekelezwa. Lakini cha kushangaza bwana mmoja anayeitwa Kashaija wa CASS alihimiza madai yao bado moja la kuing'oa DARUSO ya Kilawa maana haijasaidia kitu. (monance baraka aka Kijicho na Hatari chacha fred wakaunga mkono huku evarist silayo akipinga swala hilo akisema wahubiri amani kwa siku 30 baada ya hapo rufaa zao zisiposikilizwa basi walianzishe na wakati huo waing'oe DARUSO - wote hawa ni mojawapo wa wale nane) Evaristi alikua ni chembe tu kati ya waliokuwa wamegubikwa na ghadhabu ya kuipindua serikali.

4. Mjanja Mabirika mawazo aka alshabab alipanda jukwaani aka kiti cha plastiki na kuhimiza kuing'oa serikali ya Kilawa maana yeye ndiyo ameshatangazwa rais (muda huo wengi walikua wametawanyika maana ajenda yao ilikua ni pesa za kujikimu tu nazo wameshapata kingingine ilikuwa ni wenzao kuruhusiwa kusoma nalo tayari limeshatatuliwa. Mabirika, kashaija, kijicho, chacha, mesaya, laizer na ronaldi waliendeleza kuaminisha watu kuwa bila kuing'oa serikali ya kilawa usiku huohuo wangekua hawajasolve z wakati x na y tayari ziko solved. Hapo ndipo shughuli ya kuvunja magari yaliyokua yamewabeba wanafunzi na raia wengine kwa mawe marungu na kucharaza viboko waliokuwemo ndani na hapa mabirika mawazo aka alshababu ametajwa na afisa usalama wa taifa, madereva wawili na wanafunzi kumi kuwa ndiye alivunja kioo cha mojawapo ya shuttles; walifunga barabara ya chuo kuelekea mwenge; wakaenda yombo kucharaza viboko wale waliokua na kipindi cha saa moja; wakaenda cafteria ambapo ndipo alshabab ilifanya kazi yake ya kulipua cafteria ya mazese na sheraton watu walipewa kichapo cha ukweli hasa yule mama mjamzito nilimuonea huruma lakini ndiyo hivyo tena nilichoweza kumsaidia ni kumpeleaka kituo cha afya kwa uangalizi zaidi, hapa cafeteria anayetajwa ni monance baraka aka kijicho alimchapa viboko mmoja wa wahudumu na kuvunja chombo maalumu cha kuwekea juice na cha kuhifadhia vitafunwa vyote vikiwa vimejaa, namahadharisha kijicho akae macho maana aliyemchapa anamfahamu na ameazimia kulipiza kisasi inga Prof. mgaya nilisikia akimsihi asilipize kisasi. Baada ya cfeteria walielekea vyumba wanapolala viongozi wa DARUSO mabirika mawazo akagonga chumba cha raisi akimtaka kuachia ngazi na kumkabidhi chumba na ofisi mara moja usiku uleule maana ameshatawazwa kuwa rais (ikumbukwe kuwa hiiyo ilikua azma yake na wenzie mesaya na laizer na ikumbukwe kuwa mawazo alikua campaign manager wa mgombea urais aliyeshindwa baada ya yeye kuenguliwa kwenye search) huku ronald wa UDBS ndiye aliyevunja mlango wa waziri wa fedha(jina sikulipata vyema) ambaye ndiye alimuwekea dhamana ndipo akatoka segerea.


Mwisho nawasihi wanafunzi kuwa makini hasa wanapopanga kugoma au kushinikiza jambo fulani lazima wawe na objective zinazowezekana na zenye mashiko na shukrani ziwaendee Mukandala na Kilwa maana kwa uchunguzi nilioufanya asilimia 98 ya wajumbe wa BARAZA walita chuo kifungwe kwa mwaka mzima finalist warudi kufanya mitihani isipokua wale wahuni na hapo kutapatikana nafasi mwaka wa kwanza waanze upya na hivyo kupoteza mwaka wa kwanza na wapili wa sasa kama ilivyokua enzi za kina mbatia. Mfano kina monance watamlaumu nani kwa kumpiga mjamzito na muuza chips na juisi? mabirika atamlaumu nani kwa kuvunja vioo vya magari ya watu kwa uchu wa madaraka ya kuwa Raisi? kumbuka ukiwa nnje ya madaraka unapendwa sana ukizama ndani unakua doko mifano mingi tu ipo. Nawasihi Prof. Mukandala na BARAZA la chuo kuwa na msimamo dhabiti juu ya vikundi vya kihuni vinavyotumia matatizo ya wanafunzi kujipatia umaarufu na kujitafutia mwelekeo wa maisha ya siasa. mfano emeka na chacha wanajulikana anataka kugombea ubunge wapi na kwa tiketi ya chama gani mwaka 2015 na pia waangalie namna ya kuwasaidia wale wasio na hatia ambao walilazimishwa kujiunga wakakumbana na rungu la polisi maana kimsingi siyo wote waliokamatwa walikuwa wanajua hata kinachoendelea na ushahidi upo. Video clips nilizopiga kwa siri kwa kutumia miwani yangu ipo kama wataenda mahakamani nitawatetea.

Tuwe makini na solidarity itukombea kifikra, kivitendo na siyo kusukumwa na hisia pekee
 
Hao ambao wao walikuwa wanapiga kwa uchu wa madaraka ni watoto wa mawe? usirukie mada madai yao yaliishia wapi likaja hilo?
 
Dah.! siamini kama anawezatokea binadamu mwenye roho mbaya, kibaraka wa wakubwa, msaliti. Mchawi, na muuaji kama huyo jamaa hapo juu aliyejipinda kutuandikia utumbo, ujinga na uongo ulio pitiliza.! Repoti zakinafiki kama hizi yeye zinamsaidia nini.! Nanamuapia kwamba milele yote utaendelea kuwa kibaraka, umbwa na mtumwa na ww unaweza hata kumsaliti mama yako nafamilia yako.! Uombe 2ckutambue ndani ya udsm maana 2takufanyia tambiko kama dawa nafundisho kwa wasaliti wote.!
 
Dah.! siamini kama anawezatokea binadamu mwenye roho mbaya, kibaraka wa wakubwa, msaliti. Mchawi, na muuaji kama huyo jamaa hapo juu aliyejipinda kutuandikia utumbo, ujinga na uongo ulio pitiliza.! Repoti zakinafiki kama hizi yeye zinamsaidia nini.! Nanamuapia kwamba milele yote utaendelea kuwa kibaraka, umbwa na mtumwa na ww unaweza hata kumsaliti mama yako nafamilia yako.! Uombe 2ckutambue ndani ya udsm maana 2takufanyia tambiko kama dawa nafundisho kwa wasaliti wote.!

wewe ndio msomi tunayemtegemea siku moja atuongoze ambao hatukupata bahati ya kufika chuo kikuu?
 
mi nahisi siyo tu akili timam ya profesa mukandala bali kuna 'kolabo' ya ukweli na huyu 'baba riz' maana kama mnakumbuka aliwahi kuzomewa na wasomi hawa wa mlimani. katika uhalisia hii mambo haijakaa katika 'humanitarian grounds' badala yake ni kulipizana visasi. haya hii ndiyo tanzania yenye amani na utulivu, na hii ndiyo udsm a.k.a. chuo cha mwalimu.
 
Back
Top Bottom