Hivi huyu Vandernbroeck anatutafuta nini Wanamsimbazi?

The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,245
2,000
Jana ameiangamiza timu yetu, jana ametuumiza Wanasimba. Na hii si mara yake ya kwanza kutufanyia hivi.

Wale Platinum FC kwa jinsi nilivyowaona si wakali sana wa kututisha (najua game ijayo tutapindua matokeo) ila game plan ya Mwalimu wetu na zile sub zake za hovyo ndo zilizotugharimu. Kulikuwa kuna haja gani ya kumtoa Meddie Kagere badala ya kumwongezea nguvu? Kuna watu watasema "usimwingilie Kocha,yeye ni mtaalamu anajua zaidi kuliko wewe shabiki", acheni ujinga! Mmeambiwa wataalamu huwa hawakosei na sometimes kuzidiwa na amateurs?

Nauliza; kocha una chuki gani dhidi ya Kagere ambaye alikuwa anaisumbua Platinum kuliko yule mchovu Mugalu aliyeingia? Halafu unampendea nini Mzamiru Yassin na kiwango chake kile kibovu? Huyu Miraji Athumani ni mzuri, lakini kwakuwa umekuwa humpi nafasi, unadhani angefanya nini cha ajabu jana?

Nakuambia anza kupanga nguo zako kwenye begi. Kwanza ulikuja ukiwa kimbaumbau,una koromeo refu na macho kama una utitiri wa kuku. Sasa tumekulisha ukanawiri na ukajua kuvaa halafu unaanza kutuzingua. Get prepared!
 
The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,233
2,000
Mwanzo wa mwisho wana Simba

Ile peak ya mafanikio kwa kikosi husika ilishapita zamani ikifika pale Simba ilivyotinga robo fainali CAF

BAADA YA pale curve ikaanza kubend

Na Sasa wananchi Ni zamu curve inaaanza kupanda

Kutesa kwa zamu
 
dendaboy

JF-Expert Member
Sep 15, 2016
1,008
2,000
Hakuna sababu ya mpaka sasa kuwepo simba dadadeki zake

yaani sasa hivi simba ikikutana na timu ya kupaki basi tu mchezo umekwisha hakuna plani mbadala

swala la kipindua meza babu ni simba ile ya uchebe sio hii ya kishingo yaani wale wanakuja kupaki basi tu hapa game inakwenda suluhu na safari inaishia hapo kama huamini tusubiri utaona

na ubingwa mwaka huu simba tusahau
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,860
2,000
Tatizo sio kocha tatizo uongozi ndio maana Nkwabi alipoombwa agombee tena akasema hawezi kuwa mwenyekiti bila mamlaka mpaka Uchebe anaondoka Simba haikuwahi kucheza mchezo mbovu namna hii, wachezaji viwango vinazidi kushuka, sasa hivi wakina Rashid Juma wangekuwa wanacheza mpira kiwango cha juu ila kocha alikuwa anamuua kwa kumweka benchi.
Washabiki tuna haki ya kulalamika lakini viongozi watakuja kukurupuka wakati madhara yameshatokea hivi unawezaje kumwacha beki kijana kama Julko unabaki na beki mzee Wawa
 
The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,245
2,000
Hakuna sababu ya mpaka sasa kuwepo simba dadadeki zake

yaani sasa hivi simba ikikutana na timu ya kupaki basi tu mchezo umekwisha hakuna plani mbadala

swala la kipindua meza babu ni simba ile ya uchebe sio hii ya kishingo yaani wale wanakuja kupaki basi tu hapa game inakwenda suluhu na safari inaishia hapo kama huamini tusubiri utaona

na ubingwa mwaka huu simba tusahau
Hakuna sababu ya mpaka sasa kuwepo simba dadadeki zake

yaani sasa hivi simba ikikutana na timu ya kupaki basi tu mchezo umekwisha hakuna plani mbadala

swala la kipindua meza babu ni simba ile ya uchebe sio hii ya kishingo yaani wale wanakuja kupaki basi tu hapa game inakwenda suluhu na safari inaishia hapo kama huamini tusubiri utaona

na ubingwa mwaka huu simba tusahau
Na ubaya ndo huo, Simba ikishakutana na timu inayojua kupack vizuri haiwezi kupata ushindi. Na kama Platinum watafanya hivyo basi safari yetu itakuwa imefikia tamati.
 
Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
1,054
2,000
Simba pia wachezaji wame knock...Game ya jana ingeweza kuamuliwa na individuals tu kama wangecheza kwenye kiwango chao...Luis...Chama...Kagere hawajacheza kitu jana...
Game tumepoteza tuangalie game ijayo...maana hatukuzidiwa kwa lolote zaidi ya wao kukaba sana na kujituma ila si uwezo.
 
Diplomat Son

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,998
2,000
Jana ameiangamiza timu yetu, jana ametuumiza Wanasimba. Na hii si mara yake ya kwanza kutufanyia hivi.

Wale Platinum FC kwa jinsi nilivyowaona si wakali sana wa kututisha (najua game ijayo tutapindua matokeo) ila game plan ya Mwalimu wetu na zile sub zake za hovyo ndo zilizotugharimu. Kulikuwa kuna haja gani ya kumtoa Meddie Kagere badala ya kumwongezea nguvu? Kuna watu watasema "usimwingilie Kocha,yeye ni mtaalamu anajua zaidi kuliko wewe shabiki", acheni ujinga! Mmeambiwa wataalamu huwa hawakosei na sometimes kuzidiwa na amateurs?

Nauliza; kocha una chuki gani dhidi ya Kagere ambaye alikuwa anaisumbua Platinum kuliko yule mchovu Mugalu aliyeingia? Halafu unampendea nini Mzamiru Yassin na kiwango chake kile kibovu? Huyu Miraji Athumani ni mzuri, lakini kwakuwa umekuwa humpi nafasi, unadhani angefanya nini cha ajabu jana?

Nakuambia anza kupanga nguo zako kwenye begi. Kwanza ulikuja ukiwa kimbaumbau,una koromeo refu na macho kama una utitiri wa kuku. Sasa tumekulisha ukanawiri na ukajua kuvaa halafu unaanza kutuzingua. Get prepared!
Na Sisi Mashabiki tujifunze kuwa Wavumilivu na hata analysis zetu nazo ziwe ni zile za Kiufundi mno na siyo hizi za Kimihemuko ambazo nimeanza kuziona tokea jana baada ya Mchezo. Kwanza Simba SC Kufungwa lile Goli 1 wanatakiwa Kushukuru kwani Klabu yenye uwezo zaidi yao hapo Harare ilichezea Kichapo kizuri tu.

Sina tatizo na Kocha ila nina tatizo na Unafiki wa Sisi Mashabiki. Kocha huyu huyu alipokuwa akimpanga Mshambuliaji Mmoja tulilalamika akawarudisha Wawili hakukuwa na jipya bado tena tukalalamika. Kocha huyu huyu amekuwa akimuweka benchi Larry Bwalya kwakuwa bado hajaingia vyema katika Mfumo wa Timu tena tukalalamika na kuna Mechi kadhaa za Ligi alivurunda sana tu.

Tatizo Kubwa la Mashabiki wa Soka Tanzania tunapenda Vilabu na siyo Kuupenda Mpira husika na Kujifunza pia mbinu zake. Na kama kuna Watu ambao nawalaumu mno ni Vyombo vya Habari na Wachambuzi wa Soka nchini ambao ukiwasikiliza tu 99% ya Chambuzi zao zimeegemea Ushabiki ( Unazi ) zaidi, Unafiki na wengine kwakuwa ni Wakala wa Wachezaji basi wanatumia hizo Redio kama Platforms za Kuwanadi zaidi.

Binafsi sina shaka na nina uhakika tena wa 100% kuwa Simba SC inaenda Kunadili Matokeo hiyo tarehe 5 January 2021. Kiufundi kama Simba SC ikicheza hapa Dar es Salaam ule mpira walioucheza Kipindi cha Pili na Kocha akahimiza tu Umakini katika Kukaba ( Kujilinda ) na Kapombe pamoja na akina Chama na Miquissone wakiwa vizuri FC Platinum anakufa goli zaidi ya 3 Benjamin Mkapa Stadium.

Anaglizo tu kwa Simba SC na hili lazima niliweke ( liwekwe ) wazi na tusifichane ni kwamba hawa FC Platinum ni wazuri na nguvu yao Kubwa iko katika Flanks ( Winga ) hasa ile ya Kulia halafu wana Mapafu ( Pumzi ) mno huku wakiwa na Viungo ambao ni attacked minded, Wepesi na wana Msaada mkubwa wa Nguvu ambazo pia wanajua Kuzitumia vyema. Wiki mbili zinatosha Kujipanga Kimkakati ili Kuwakabili na Kuwatoa.
 
Uphill

JF-Expert Member
Sep 23, 2018
500
1,000
Hapa wamejaa utopolo....! Kwa Mkapa hatotoka mtu...! 'Hata aje Barcelona kama hutaki meza sumu..!
Hata Plateau hakutoka kwa Mkapa si ndiyo? Kocha na wachezaji waje na plan ya kulazimisha matokeo kwa Mkapa. Na tunatakiwa kuwambia ukweli ili wapambane timu ipate ushindi. Hawa tukilegezea tutatolewa hapo hapo kwa Mkapa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom