Hivi huyu NDODI wa starTV huwa mnamwelewa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huyu NDODI wa starTV huwa mnamwelewa??

Discussion in 'JF Doctor' started by Van pierre, Mar 27, 2011.

 1. V

  Van pierre Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa me cmwelewi kabisa!kuna siku nilimsikia anasema TUSILE CHIPS,MAYAI,NYAMA,UGALI,WALI,SAMAKI,MAHARAGE,DAGAA and TUSINYWE JUICE,SODA ZOTE,BIAAAA huyu jamaa anataka tu starve to death nini!!anataka tuwe na jamii ya watu vikonde?2tafanye kazi?? Kuna siku aliniua kabisa,nikamsikia laivu kwenye hiyo tv anakataza watu kunywa cocacola,pepsi... And kutumia blueband,halafu anazitaja hizo bidhaa kwa majina yake KABISAAAA!jamaa si anaharibu biashara za watu huyu???au me ndo nipo wrong???!
   
 2. I

  Isekuu Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kampuni yao ipoipo tu dialo mwenyewe hata kiswahili tabu.
   
 3. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  :embarassed2:
   
 4. S

  Smoke Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo, yupo ok bt maybe hukumsikia vizuri, ugali uliokobolewa ndio alisema tusile kwa sababu unakua hauna madini ya kutosha ya iodine ambayo yana speed up kusafiri kwa kasi kwa umeme wa meridian mwilini, pili blueband ni mbaya huo ni ukweli coz ukisoma kwenye cancer ya matiti na hypertension yenyewe inachangia kusababisha hayo magonjwa. Kuhusu vinywaji vya coca na pepsi vile ni depresants na kwa utafiti zaidi kachunguze kemikali zinazowekwa kwenye soda halafu kawaulize wataalam kama zina faida mwilini. Mayai alisema tusile kwa wingi kupita kiasi kwa sababu kiini chake kina cholesterol nyingi. Buddy i think you should pay attention well next time and judge well instead of partial perceiving.
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  umenena vyema mkuu.
   
 6. V

  Van pierre Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma mkuu!sasa na hii ya kuzitaja hizi bidhaa kwa majina kwenye tv inakuwaje??si anaharibu busines za watu?me nafikiri ktna mambo anatakiwa kuyatamka akiwa na mteja mmoja mmoja
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Hivi jamani katika watanzania wanaoshi mijini wangapi hawatumii unga wa kukobolewa yaani sembe? lini tumeanza kutumia sembe?
   
 8. S

  Smoke Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sidhani kama ni vizuri, watanzania wako wangapi na atawafikia wangapi na kwa mda gani kama akienda kwa mmoja mmoja? Nadhani ni vema anachofanya ili mradi havunji sheria! Utaogopa kuelimisha watu wakati unaona watu wanakufa na kuugua, utaogopa kuwapa ukweli eti kwa sababu unaogopa kampuni? Na zaidi hajalazimisha watu kutumia au kutotumia, amewapa watu ushauri wa kidaktari kamaliza, kinachobaki ni juu ya mtu mwenyewe kuamua afanye nini. Au sio mkubwa?!
   
 9. N

  Nsagali Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Doctor akikushauri kitu kazi inabaki kwako kufuata au kuacha kwa hiyo na ndodi yupo sawa.
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ukweli wa mambo ni kwamba watu wengi tunakulakula mno. Tunajiletea janga la kiafya kwa kutokuchagua aina na uwingi wa chakula
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Unapotoa comment just think 100 times....kitu kikiwa na madhara kwako hakina shida kwasababu umeanza kula muda mrefu? Just look on effects even if ni matokeo ya muda mrefu....................
   
 12. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Dona ndiyo ugali, achana na sembe wewe.
   
 13. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Amini usiamini ukifuata lishe anayoshauri kula dr ndodi kwa 100% hautakuwa mteja wa hosptal, presha ,kisukari ,magoti kuuma, unene wa kizembe,na hasa kitambi ya ugonjwa hautakuwa navyo kabisa,,
  wewe na family yako utaishi mwenye afya njema, furaha na amani na mwenye maendeleo yataongezeka ksb gharama za hosp zitakuwa hazipo.
  .
  Ningekuwa kiongozi wa nchi hii hakika dr ndodi ningempa kazi ya kuelimisha jamii nchi nzima ili kuokoa watu na magonjwa mengi ya kujitakia...% kubwa ya wagonjwa wote wanaumwa magonjwa ya ulaji mbaya wa kula.

  Dr ndodi ni mshauri mzuri sana upande wa lishe,,,,haijalishi umekula sembe miaka mingapi, lakin tujaribu kubadilika na kuanza kula vyakula vya afya ili tuwe na afya bora na siyo bora afya....

  Mungu amzidishie uzima na afya njema ili tuendelee kupata elimu anayoitoa,,,pia anapoongea jitahidi kumsikiliza kwa utulivu na umakini naamini utamwelewa vizuri sana ,pia anaweza kuwa msaada mzuri sana kwa afya yako.
   
Loading...