Hivi huyu mwanaume anatumia akili au makamasi kufikiri?

Tegelezeni kwa niaba ya wote tulioko kwenye thread hii nakuomba ushirik kikamilifu kumsaidia huyo jirani yako kwa kumpa ushauri nasaha jirani yako huwez kumuacha. YOU CAN CHOOSE FRIEND BUT YOU CAN'T CHOOSE NEIGHBOR. So do the needful. Plz update us.

Huyo anahitaji tiba mbadala ya ushauri nasaha kwa kweli...............
 
An idle mind is devil's workshop.....................devil at work!!
Ni jirani yangu na wakati nahamia katika nyumba ninayoishi nilimkuta akiwa na mwanamke ambaye nilijua ni mkewe Baadae yule mwanamke akamwambia mke wangu kuwa yule mwanaume anaye mkewe ambaye walioana na kuzaa naye watoto wawili, na walidumu katika ndoa kwa miaka saba na kutengana hivyo akarudi Mkoani na ndipo akachukuliwa yeye na kuja kupangishiwa nyumba hapa jirani na tunapoishi. (wameishi bila ndoa miaka 3 na wala hawajapata mtoto).

Huyu bwana ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hivyo sina mazoea naye. Siku za hivi karibuni huyu bwana alinijia akitaka nimweleze kama huyu mwanamke wake (ngoja nimuite hawara yake) ni Malaya? Nilimwambia sijui lolote kwa kuwa mimi sishindi hapa nyumbani. Ilipofika usiku nikasikia ugomvi wakipigana na huyo hawara yake, na ilipofika asubuhi nikamuona huyo mwanamke anafungasha na kuondoka. Siku huyu jamaa alipokuwa anasafiri alinijulisha kwamba nisije shangaa maana mkewe wa ndoa anakuja kutoka mkoani na ni yeye atakayekuwa akiishi hapo.

Ni kweli mke alikuja na kujitambulisha kwetu kama jirani. Lakini jana huyo mkewe kaja na kumweleza mke wangu kuwa mumewe kampigia simu kuwa yule hawara atakuja na kufikia hapo na kulala kwa siku moja kisha ataondoka na kuendelea na safari yake kwenda Arusha, hivyo amruhusu kulala hapo nyumbani lakini haruhusuwi kuchukua chochote. Yule hawara alifika kwa mbwembwe jana jioni na ilipofika usiku hatukulala, kwani alikuwa anamfanyia vurugu mke wa jamaa kwa kuvunja vyombo eti kwa madai kuwa walinunua wote na huyo mwanaume.

Huyu mwanamke wa ndoa mpaka sasa yuko kimya na anamwangalia tu jinsi huyo hawara anavyofanya vurugu na kuvunja vyombo na makabati, na hivi ninavyoandika hapa ninashuhudia vituko mbwembwe na tambo za huyo hawara akimfanyia mwenzake, lakini mwenzake kapiga kimya kama hakuna kitu.

Najiuliza:

1.Hivi huyu mwanaume ana akili kweli?

2. Je wakiuana humo ndani ya nyumba ni nani atakuwa responsible na hivyo vifo?

3. Hivi kweli unawezaje kuruhusu hawara aje afikie kwako wakati mkeo wa ndoa yupo na watoto, Je akiwadhuru watoto?

Mimi ni mwanaume lakini anavyofanya huyu mwenzangu simuelewi kabisa, au ndivyo wanaume wa kanda ya ziwa walivyo?

Hebu wale wadada na wakaka watetezi wa haki za ndoa hapa JF mkuje kutoa ushauri: gfsonwin, snowhite, King'asti, jouneGwalu, Mwita Maranya, Jiwe Linaloishi, nivea, FirstLady, sweetlady MwanajamiiOne, SnowBall, The Boss, Neylu, BADILI TABIA, nyumba kubwa, Dark City, Arushaone, Mungi, Preta, lara 1, giLESi, charminglady, cacico, Remmy, Bujibuji, Scofied, KakaKiiza, Kaizer na wengineo niliowasahau lakini wana michango yenye kujenga hapa MMU
 
Ndoa ndoana!! Miaka 7 mume kakutelekeza na watoto!!! Anakuita baada ya kutibuana na hawara!! Unakubali kurudi!! Anakuletea hawara ili aje akumalize!!! Akili za huyo mwanaume ni za konokono!!!
 
Mwashangaaaa Nini!!!!!!!!!!!? Kazi kungaa sharubu tu!!!!!!!!! Toka lini Fahari wawili wakakaa zizi moja!!!!! Ofcourse huyo bwana ana makosa sana kucheat na huyo Hawara.

Ila hawara pia ana HAKI ZAKE ZA MSINGI TU hapo! We utumike 3 F. Years afu uachwe kizembe zembe hivi hvivi eti kisa mwenzio anarudi!!!!!! Bull shit!!!!!!

Vunja bibi wewe vunja hapo kila kitu!!!!!!!!! Usibakishe hata kikombe!!!!!! Wanaume wana masihara sana na maisha ya wanawake!!!!!!!! Yaani ujisikie tu UNIFURUMUSHE!!!!!! Kirahisi rahisi tu!!!!!!! Mmmmmmmh!

Angekuwa mtu mwepesi mwepsei huyo hawara angeondoka kimya kimya maskini ya Mungu, with her broken heart, akaenda kufia mbele ya safari kimya kimya huku hili Fisadi la Mapenzi Limepoziiiii!!!!!!!!! Halina stress kabisaaa linajinafasi na mkewe!!!!!!! Thubutuuuuuu yao!!!! Vunja hadi mlango hapo shostito!!!!!!!!!!!
Inaonekana hata wewe ni.mwizi wa waume za watu ndo mana unamtete huyo hawara.
ndio mana kila wakati naomba Mungu yasinikute maana huyo hawara angejuta kukatisha mbele ya upeo wa macho yangu. Kama angekuwa baunsa nikamshindwa ningekuwa radhi kumkodishia wanaume.
 
madawa ya kienyeji nayo yanafanya kazi vizuri tu. so msimlaumu. Mimi nawalaumu wanawake wanao endekeza ushirikina. mia
 
Huyo Mwanaume adhabu atakayokuja kuipata katika maisha yake ni ya 'kukata' na 'shoka' maana atalipia na zaidi matendo yake ya hovyo. Wanawake ni wavumilivu wa kupindukia na inawachukua muda mfefu kulipizia kisasi. Kuna wanaume wengi wanaolipa matendo yao ya mwaka arobaini na saba leo hii ninapoandika hapa.
 
Inaonekana hata wewe ni.mwizi wa waume za watu ndo mana unamtete huyo hawara.
ndio mana kila wakati naomba Mungu yasinikute maana huyo hawara angejuta kukatisha mbele ya upeo wa macho yangu. Kama angekuwa baunsa nikamshindwa ningekuwa radhi kumkodishia wanaume.

Hahahaaaaaaaa! Wewe mtu mzima hatishiwi nyau!!!!!! Kama una hasira sana mfunge mumeo speed governer!!!!!! LOL! Mi waume za watu WANICHOSHA tuuuu, pesa zao za mawazo, bugdha tupu! Heri vitoto hivi single vyenye URITHI mzito ndo navovitakaga!!!!!!!! Hao waume zenu nimewaachia wanaotoka mkoa jana na leo!!!!!!!
 
Hahahaaaaaaaa! Wewe mtu mzima hatishiwi nyau!!!!!! Kama una hasira sana mfunge mumeo speed governer!!!!!! LOL! Mi waume za watu WANICHOSHA tuuuu, pesa zao za mawazo, bugdha tupu! Heri vitoto hivi single vyenye URITHI mzito ndo navovitakaga!!!!!!!! Hao waume zenu nimewaachia wanaotoka mkoa jana na leo!!!!!!!

Haya chacha mutoto ya mujini hiyo, wenye visima vya mkwanjwa ndo una wasaka kwa usongo
 
Haya chacha mutoto ya mujini hiyo, wenye visima vya mkwanjwa ndo una wasaka kwa usongo

As long as he doesnt have a ring on his fingures it means HE IS SINGLE AND AVAILABLE FOR TAKING!!!!!!!!1 Hapo chacha tunmavotoana roho, wenyewe kwa wenyewe!
 
Mhhhhhhh!!!!! BIG UP AISEEEEE!!!!!! Ila mimi hiyo chai nayowapikia ningeweka Potassium kidogo au hata Conco Hydrochloric Acidi, au hata H2SO4 nikishindwa kabisaa Maji ya Betri kumaliza kazi!!!!!!!! Baaaaaaaaasss!!!!!!! Ndoa hiziii!!!!!!!!! Mi siwezi aiseeeee!

Ha ha ha, nilikuwa na mpango wa kukutongoza but navyojijua drama zangu ukija kuzijibu kwa style hizo tunaweza sababisha bendera zipepee nusu mlingoti as ni msiba wa kitaifa mapumziko 3 days... Maana hawa warembo mjini wasivyojua kukataaa kutulia na mke wa ndoa ni kazi sana kwa dot com generations zaidi ya kujikaza kisabuni wasiwe wengi
 
Uanaume nao una gharama zake,huwezi kuitwa mwanaume mpaka kitu kikuume.Nadhani mtu wa kwanza kumshauri alitakiwa awe wewe kama kweli ungependa awe mwanaume unaemfikiria hasa kuwa.Na iwapo angeenda kinyume na ulivyofikiri hapo ndipo ungepata uhalali wa kujiuliza kama kweli anafikri kwa kichwa ama ulivyosema.NAAM nyumba zetu zimeficha matatizo mengi na hayo yanayoonekana kwa nje ni kama uchi wa ndoa.WEWE kama jirani mwanaume msaidie kumvalisha vazi asitirike huwezi jua hata wewe kuna yanayofanyika usipokuwepo na wengine wanajiuliza we una akili au?
 
Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume... People treat you the way you want them to treat you... Hapo wakushangaliwa na hao wanawake pia. Ni mambo mengi wanaume wanatufanyia na kutuchezea ambavyo wasinge thubutu kama tusingeruhusu. Upole, ustaarabu, na husuda ina mpaka wake. Matatizo yapo kwa wote...

Tatizo la Mke

Kwa kukubali kudharauliwa hadi kiwango hicho. Mume kamtelekeza kwa miaka mitatu na kumtuma mkoani yeye pamoja na watoto wake. Kamrudisha hapo nyumbani huku mke akijua fika kuwa kuna hawara alikuwa akiishi hapo na mbaya zaidi ni kuwa huyo hawara karuhusiwa kufikia hapo akiwa en route kuelekea Arusha. Kakubali Mumewe amchezee... But hata hivo sio rahisi kujudge maana ukute naye kaelewa maumivu ya moyo wa huyo mwanamke akijua fika vitu vya humo ndani sio vyake ni halali ya huyo dada. Tena WARNING; Huyo mwanaume anaonekana ni mshenzi ukute hata huyo mwanamke mpya sio mke bali ni mwanamke mpya ila kaja kujisafisha kwenu... (Labda kama kweli na hao watoto wameletwa hapo).

Tatizo la Hawara

Ok, ni kawaida kuwa mtu unaweza toka na mme wa mtu, BUT hivi kuna sababu yoyote ya kwenda mletea vituko mke wake na vujo tele hata kama ana hasira juu ya mahusiano yao kuvujika? Nashangaa... Hiyo confidence ya kulala humo ndani anaitoa wapi (mchawi??); kuwa unajua kuwa mke wake pia anajua wewe ndiye uliyekuwa mbadala na unarudi kulala humo ndani?

Kwa upande namuelewa... Kapoteza miaka mitatu kwa ajili ya huyo mwanaume. Wapo wote (ki mantiki kwa halali kabisa maana alitengana na wife); then kamfanyia visa na kumtoa humo ndani bila kitu chochote. Hasira zake ni halali ila tu nashangaa hiyo roho yake ya paka asiee... Duh!

Kwa mtazamo wangu naweza sema haya mambo magumu sana kuja na justification za hasa yupi anatakiwa lawama. Mwanaume ana makosa pia, ila hao wanawake nao sio watoto wadogo waangaliwe tu kuwa wao ndiyo wameonewa na hali wao ndio wamechangia kwa ukubwa hali kuwa ilivo. Kitu nakuhakikishia ni kuwa mwanaume angejua kuwa mke wake kichaa na hakubaliani na upuuzi usio kuwa na tija asinge thubutu, hata huyo hawara asinge thubutu...

Ila niongezee kuwa watu wa sampuli kama hiyo ya huyo mke hatari saana. Hulimbikiza mambo rohoni, siku aki react unakuta kama sio mume ama hawara ama wote maiti tu, na wala hajutii...
nipe fursa ya kukutoa dinner one of this days please!
 
Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume...

kinacholazimisha kumjudge huyo jamaa yetu ni kuwa, busara ya vitabu vya dini ilitutaka wanaume "kuishi kwa akili" na wake zetu, hapa ndio maana huyu mwanababa anakuwa centre of attention sababu katika mazingira yetu na mienendo ya wanaume, ye ndio ameonyesha upungufu zaidi wa kiakili.
Hata stadi za kuhandle nyumba ndogo, darasa la The Boss limempita pembeni....
Hii ndio sababu ya kumng'ang'ania huyu mwanaume inapoanzia.
 
ndoa ndoano ,naleta mashtaka baba paroko nanyimwa haki yangu ya ndoa,siku zinavyozidi kwenda wanaume wanaisha wanabaki wavulana tunaelekea wapi thatha.
 
Hahahaahaha Babu Mwanamalundi inakuhusu nini??? Maana umewaka!

Ha ha ha ha ha ha!! No no no no!!! Watu wengine wanakera sana kufuatilia maisha ya watu wengine. Wanachotakiwa kufahamu ni kuwa hakuna "formula" or "blue print" ya maisha. As long as hawakulishi, hawakufulii nguo, hawakulipii nauli ya dalaladala, hawakukogeshi, etc etc, so what??Wanachotakiwa kuelewa ni kuwa---There is nothing good or bad; only thinking makes it so. Mkome kufuatilia maisha ya watu. Natoa onyo kali.
 
Hahahaaaaaaaa! Wewe mtu mzima hatishiwi nyau!!!!!! Kama una hasira sana mfunge mumeo speed governer!!!!!! LOL! Mi waume za watu WANICHOSHA tuuuu, pesa zao za mawazo, bugdha tupu! Heri vitoto hivi single vyenye URITHI mzito ndo navovitakaga!!!!!!!! Hao waume zenu nimewaachia wanaotoka mkoa jana na leo!!!!!!!
Ooooh.......! Maama
 
Mheshimiwa siri ya ndoa na uhalisia wa matukio wanajua wanandoa labda kidogo na huyo hawara, ni vigumu kwa sisi kujua hasa kiini cha tabia za huyo mwanaume, ukimya wa huyo mwanamke wa ndoa na pia vurugu za hawara. ingekuwa rahisi kujadili hili endapo wote watatu wangefunguka ila kwa ukimya wao unapaswa kuuheshimu. Ndoa ina siri nyingi sana wadau oeni au oleweni ndio mtajua lakini mkiwa third parties tunaweza kuzungumza mengi sana juu ya ndoa za wengine kuliko hata za kwetu. Samahaaaaani lakini................
 
Back
Top Bottom