Hivi huyu mwanaume anatumia akili au makamasi kufikiri?

Bado haiondoi hadhi yake kama mke halali kwa mujibu wa sheria unless kama alipodundwa alikabidhiwa na talaka yake otherwise mume huyo anao wake wawili mpaka sasa. Kuishi na mwanamke miaka 7 kama mke ni mkewe halali. Hayo ya kutokuwa mwaminifu, sijui kicheche hayaondoi title ya mke au mume ndoani unless talaka imehusika.

Kwa taarifa hii ninaanza kupata picha mpya kabisa ya tukio hili. Inawezekana sasa mume amelitambua kosa lake la kumtelekeza mke mkubwa sasa ametaka kumrudisha lakini akajisahau kuwa ALIOA mke wa pili (hata kama hakufunga nae ndoa) so mke wa pili nae anayo haki ya kumclaim yeye kama mumewe. Ila swali ni kwamba alikuwa akiwaza nini kuwaweka mahali pamoja?

Na huyo mama wa ndoa mwambie aache ujinga anasafisha nyumba ya nini aache mumewe aje ashuhudie ukuchaa wa bi mdogo wake, ye anatupa vidhibit?

Ninavyofahamu mimi hata dini inayoruhuru kuoa wake wengi mojawapo ya masharti ni kutowaweka katika nyumba moja. lakini hata kama unasema wote ni wake zake mimi sioni logic, maana jamaa alioa Kiislamu huyu mke wa ndoa, lakini huyu hawara ni M-Lutheran na ndio hapo najiuliza itakuwa ni ndoa ya aina gani hapo?
 
Arushaone inapendeza kuwa umelitazama kwa mtazamo huo... Inatia moyo kuwa kuna baadhi ya wanaume wanawashawishi wanaume zao ku treat wanawake zao vizuri. Ingawa tumetofautiana kim mtazamo kwa mimi kuona wanawake wanalaumiwa pia; na wewe kuona mwanaume ndiye apewe lawama zote - nafurahi kuwa walau twakubaliana kuwa dawa yake ni hao wanawake waungane kutafuta suluhu...

Hata mie ningefurahi kama wangeungana na kumsubiri jamaa arudi wamshikishe adabu.

yaani nikiwaona wanavyopishana mlangoni huyu anatoka na huyu anarudi mwili wangu unanisisimka, maana hapa niko sebuleni kwangu na ninaona kila kinachoendelea nyumba ya pili maana milango inatazamana, balaa gani hili!
 
Kwanza naomba niwatetee wanaume wa kanda ya Ziwa (akiwemo Baba yangu) kwamba hawako hivyo kabisaa..!

Huyo jirani yako ni utaahira alionao tuu yeye kama yeye..!! Mwanaume mwenye akili timamu hawezi kufanya hayo madudu ya kumleta hawara afikie kwa mkewe..!! Ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu.!!

Ashukuru Mungu kwamba ana mke mstaarabu..!!. Huyo Hawara angekutana na mimi hakuna rangi angeacha kuona..!!

Hahahaha Neylu kumbuka huyo si hawara tena bali mke wapili wa mumeo bibi!! Tena si nyumba ndogo ukasema analala na mumeo kwa msimu, weshaishi miaka saba pamoja na wangekuwa na uzao wangekuwa na watoto pamoja pia so hapa ungekutana na mke mwenza na si hawara tena. Na tena ungekutana nyumbani kwake ambapo alikuwa anaishi na mume wenu wewe ndo ungeonekana mchokozi
 
Last edited by a moderator:
Ninavyofahamu mimi hata dini inayoruhuru kuoa wake wengi mojawapo ya masharti ni kutowaweka katika nyumba moja. lakini hata kama unasema wote ni wake zake mimi sioni logic, maana jamaa alioa Kiislamu huyu mke wa ndoa, lakini huyu hawara ni M-Lutheran na ndio hapo najiuliza itakuwa ni ndoa ya aina gani hapo?

Kwa sheria ya ndoa hii ni ndoa ya kiserikali sasa maana ni kwa mujibu wa sheria. Huyo 'hawara' akienda mahakamani kudai haki zake kama mke believe me not, atatetewa na vyombo vyote vya kisheria.
 
Hata mie ningefurahi kama wangeungana na kumsubiri jamaa arudi wamshikishe adabu.

yaani nikiwaona wanavyopishana mlangoni huyu anatoka na huyu anarudi mwili wangu unanisisimka, maana hapa niko sebuleni kwangu na ninaona kila kinachoendelea nyumba ya pili maana milango inatazamana, balaa gani hili!

Sasa na wewe Tegelezi unataka wana Jf tuunde majeshi tukuchape (I kid), toka jana hadi saa nane hii bado tu mwili unasisimuka huchukui maamuzi yoyote? Umewawakilisha hapa tafadhali najua ni ngumu kuingilia ndoa na mambo ya watu but kama jirani ambaye ulikuwa umehusishwa toka awali ni nafasi nzuri ya wewe kuwaendea na kuwapa ushauri kwamba sasa watulie.
 
Namshangaa yaani kama namwona kakaa kibarazani aki'tegheezaa' ngoja niongee na kikwetu kabisa badala ya kuchukua hatua.

We Baba Tegelezeni vipi bana?
 
Dada unaenda mahali ambapo umeitwa, kwa sasa hali ni shwari maana havunji tena vyombo ila kuna vijineno vya uchokozi anazungumza huyu hawara (Sorry mwanangu MwanajamiiOne kasema huyo ni mke wa ndoa kisheria) ambavyo vinakera masikioni kama huyu mke wa ndoa angekuwa ni mkorofi, zingaumana, lakini namuona yuko bize na vijishughuli vyake vya kutengeneza bustani ya maua hapo nje huku mwenzie anaingia na kutoka huku maneno ya kejeli yakimtoka
 
yaani hiyo miaka saba mke wa ndoa alikuwa hajawahi kanyaga nyumbani mjini kwa mme wake?
 
Namshangaa yaani kama namwona kakaa kibarazani aki'tegheezaa' ngoja niongee na kikwetu kabisa badala ya kuchukua hatua.

We Shemeji Tegelezeni vipi bana?

Umeona eeh?

Alafu hapo chini naona Tegelezeni umejitetea kaka... Kweli on a serious note ni kheri mkawashauri. Sio hadi watu wauwane ndio kauli za 'ninge' zina anza. Majuto mjukuu.. Hicho kitendo cha kusema bado wapo wote ndipo hasa penye tatizo. Enways lets hope for the best.
 
Dada unaenda mahali ambapo umeitwa, kwa sasa hali ni shwari maana havunji tena vyombo ila kuna vijineno vya uchokozi anazungumza huyu hawara (Sorry Mwanangu MwanajamiiOne kasema huyo ni mke wa ndoa kisheria) ambavyo vinakera masikioni kama huyu mke wa ndoa angekuwa ni mkorofi, zingaumana, lakini namuona yuko bize na vijishughuli vyake vya kutengeneza bustani ya maua hapo nje huku mwenzie anaingia na kutoka huku maneno ya kejeli yakimtoka

Hahahha haya Baba kwa kujitetea nimekuelewa. Hapo sasa nadhani Mke mdogo ni hacra za kujeruhiwa ndo mana anatoa kejeli kwa asiyehusika. Ninadiriki kusema kuwa huyo si mwanamke kamili maana angekuwa mwanamke kamili asingejishughulisha na mke wa mumewe bali angejishughulisha na mumewe tena angekuwa kichaa asingemsubiri arudi ye angemwendea hewani kama yuko nje ya mji akamalizia hasira yake
 
Namshangaa yaani kama namwona kakaa kibarazani aki'tegheezaa' ngoja niongee na kikwetu kabisa badala ya kuchukua hatua.

We Shemeji Tegelezeni vipi bana?

Mie nategheeza ili ili niwahabarishe.
Lakini tuache utani katika maisha yangu sikutarajia kukutana na kitu ya namna hii, na ndio maana siishi kushangaa, kama wakishikana nitakuwa na haki ya kuingilia na kuamulia ugomvi, lakini kwa kuwa mfanya fujo ni mke mdogo na mke mkubwa kapiga kimya, mie yangu macho na masikio.

Nakumbuka miaka mitano iliyopita mke wangu alinipigia simu kuwa mzazi mwenzangu niliyezaa naye ujanani kaja kusalimia akiwa na mtoto. Nafahamu alikuja mjini kwa kaka yake, lakini hakusema kama atakuja kwangu na nilijua hapafahamu.

Si akaenda kwa binamu yangu kumuomba eti aje kwangu kumleta mtoto kwa baba yake, na binamu bila kuwasiliana nami akamleta wakati mie nilikuwa Morogoro kikazi, nakwambia nilirudi mbio yaani kufika jioni niko kwangu, kwa bahati nikakuta wameondoka, nilimuwashia moto binamu yangu hatakuja asahau.

Nilichofanya nikamkomboa mtoto wangu kwa kufuata mila za Wasambaa na kumpeleka boading school hakuna sababu ya kuja kwangu tena na akimtaka mwanaye asubiri likizo.
 
Huyo hawataki wote, anataka kuwapoteza ili alete kitu kipya zaidi
MESTOD huyu mwanaume atakuwa bonge la coward then, ..yaani ameshindwa kuwapa facts live juu ya msimamo wake na kuamua kutumia njia ya kipanya kiasi hiki?? Hafai basi, hata hicho chuma kipya kama kipo tunakionea huruma maana nacho kitaachwa kwa style ya ajabu muda ukifika.
 
Last edited by a moderator:
Hayakuhusu. Chukua time yako. Acha kufuatilia maisha ya watu na kutuletea umbeya hapa kwenye jamvi. Wakitoana roho wewe inakuhusu nini? watu wengine bana!! aaaargggh!!! wanakera kweli kweli. Waache na maisha yao.
 
Hongera sana hayo ni maamuzi ya kiume si unaona wanaume wengine wanavyofanya madudu. Yaani huyu hata hafai Baba.
 
Hayakuhusu. Chukua time yako. Acha kufuatilia maisha ya watu na kutuletea umbeya hapa kwenye jamvi. Wakitoana roho wewe inakuhusu nini? watu wengine bana!! aaaargggh!!! wanakera kweli kweli. Waache na maisha yao.
Hahahaahaha Babu Mwanamalundi inakuhusu nini??? Maana umewaka!
 
MESTOD huyu mwanaume atakuwa bonge la coward then, ..yaani ameshindwa kuwapa facts live juu ya msimamo wake na kuamua kutumia njia ya kipanya kiasi hiki?? Hafai basi, hata hicho chuma kipya kama kipo tunakionea huruma maana nacho kitaachwa kwa style ya ajabu muda ukifika.

Utakuta kajaribu kila njia kashindwa, iliyopo ni kuwapambanisha tu!
 
Tegelezeni kwa niaba ya wote tulioko kwenye thread hii nakuomba ushirik kikamilifu kumsaidia huyo jirani yako kwa kumpa ushauri nasaha jirani yako huwez kumuacha. YOU CAN CHOOSE FRIEND BUT YOU CAN'T CHOOSE NEIGHBOR. So do the needful. Plz update us.
 
Last edited by a moderator:
Naona unapenda ku-generalize sana sasa hapo watu wa kanda ya ziwa inafuata nn? Kila mtu na akili yake haijalishi anatokea wapi ni hayo tu
 
Back
Top Bottom