Hivi huyu mwanaume anatumia akili au makamasi kufikiri?

Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Messages
268
Likes
2
Points
0
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2009
268 2 0
Ni jirani yangu na wakati nahamia katika nyumba ninayoishi nilimkuta akiwa na mwanamke ambaye nilijua ni mkewe Baadae yule mwanamke akamwambia mke wangu kuwa yule mwanaume anaye mkewe ambaye walioana na kuzaa naye watoto wawili, na walidumu katika ndoa kwa miaka saba na kutengana hivyo akarudi Mkoani na ndipo akachukuliwa yeye na kuja kupangishiwa nyumba hapa jirani na tunapoishi. (wameishi bila ndoa miaka 3 na wala hawajapata mtoto).

Huyu bwana ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hivyo sina mazoea naye. Siku za hivi karibuni huyu bwana alinijia akitaka nimweleze kama huyu mwanamke wake (ngoja nimuite hawara yake) ni Malaya? Nilimwambia sijui lolote kwa kuwa mimi sishindi hapa nyumbani. Ilipofika usiku nikasikia ugomvi wakipigana na huyo hawara yake, na ilipofika asubuhi nikamuona huyo mwanamke anafungasha na kuondoka. Siku huyu jamaa alipokuwa anasafiri alinijulisha kwamba nisije shangaa maana mkewe wa ndoa anakuja kutoka mkoani na ni yeye atakayekuwa akiishi hapo.

Ni kweli mke alikuja na kujitambulisha kwetu kama jirani. Lakini jana huyo mkewe kaja na kumweleza mke wangu kuwa mumewe kampigia simu kuwa yule hawara atakuja na kufikia hapo na kulala kwa siku moja kisha ataondoka na kuendelea na safari yake kwenda Arusha, hivyo amruhusu kulala hapo nyumbani lakini haruhusuwi kuchukua chochote. Yule hawara alifika kwa mbwembwe jana jioni na ilipofika usiku hatukulala, kwani alikuwa anamfanyia vurugu mke wa jamaa kwa kuvunja vyombo eti kwa madai kuwa walinunua wote na huyo mwanaume.

Huyu mwanamke wa ndoa mpaka sasa yuko kimya na anamwangalia tu jinsi huyo hawara anavyofanya vurugu na kuvunja vyombo na makabati, na hivi ninavyoandika hapa ninashuhudia vituko mbwembwe na tambo za huyo hawara akimfanyia mwenzake, lakini mwenzake kapiga kimya kama hakuna kitu.

Najiuliza:

1.Hivi huyu mwanaume ana akili kweli?

2. Je wakiuana humo ndani ya nyumba ni nani atakuwa responsible na hivyo vifo?

3. Hivi kweli unawezaje kuruhusu hawara aje afikie kwako wakati mkeo wa ndoa yupo na watoto, Je akiwadhuru watoto?

Mimi ni mwanaume lakini anavyofanya huyu mwenzangu simuelewi kabisa, au ndivyo wanaume wa kanda ya ziwa walivyo?

Hebu wale wadada na wakaka watetezi wa haki za ndoa hapa JF mkuje kutoa ushauri: gfsonwin, snowhite, King'asti, jouneGwalu, Mwita Maranya, Jiwe Linaloishi, nivea, FirstLady, sweetlady MwanajamiiOne, SnowBall, The Boss, Neylu, BADILI TABIA, nyumba kubwa, Dark City, Arushaone, Mungi, Preta, lara 1, giLESi, charminglady, cacico, Remmy, Bujibuji, Scofied, KakaKiiza, Kaizer na wengineo niliowasahau lakini wana michango yenye kujenga hapa MMU
 
Last edited by a moderator:
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Likes
94
Points
145
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 94 145
Unajua huwa tunaambiwa kuwa MUNGU humpatia kila mmoja mwenzi wa kufanana nae. So ni huyu mbaba na hawara yake wote wanafanana akili. Huyo mama wa ndoa ana akili sana! Ila alitakiwa kugoma kufikia nyumbani hapo ambapo yuko mwanamke wa mumewe (Kama alijua lakini maana story yako sijaisoma yote)
 
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Messages
268
Likes
2
Points
0
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2009
268 2 0
Unajua huwa tunaambiwa kuwa MUNGU humpatia kila mmoja mwenzi wa kufanana nae. So ni huyu mbaba na hawara yake wote wanafanana akili. Huyo mama wa ndoa ana akili sana! Ila alitakiwa kugoma kufikia nyumbani hapo ambapo yuko mwanamke wa mumewe (Kama alijua lakini maana story yako sijaisoma yote)
Kusema ukweli hata mimi nilishangaa sana wakati huyu jamaa aliponitamkia hivyo kuwa mkewe wa ndoa atakuja na kufikia hapo kwake baada ya hawara kuondoka, lakini nilishangaa zaidi huyo mkewe alipomwelleza mke wangu kuwa mumewe kampigia simu na kumjulisha kuwa hawara atakuja na kufikia hapo nyumbani...

Hivi sasa niko hapa nje nashuhudia mke wa ndoa akifanya usafi wa kutupa vyombo vliivyovunjwa na vioo vya makabati wakati hawara amekaa sebuleni anajichana kwa breakfasti na mpishi ni mke wa ndoa!

Sijui le litazama salama hapa nyumbani maana huu ukimya wa huyu mke wa ndoa mie unaniogopesha kabisa
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,243
Likes
318
Points
180
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,243 318 180
Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume... People treat you the way you want them to treat you... Hapo wakushangaliwa na hao wanawake pia. Ni mambo mengi wanaume wanatufanyia na kutuchezea ambavyo wasinge thubutu kama tusingeruhusu. Upole, ustaarabu, na husuda ina mpaka wake. Matatizo yapo kwa wote...

Tatizo la Mke

Kwa kukubali kudharauliwa hadi kiwango hicho. Mume kamtelekeza kwa miaka mitatu na kumtuma mkoani yeye pamoja na watoto wake. Kamrudisha hapo nyumbani huku mke akijua fika kuwa kuna hawara alikuwa akiishi hapo na mbaya zaidi ni kuwa huyo hawara karuhusiwa kufikia hapo akiwa en route kuelekea Arusha. Kakubali Mumewe amchezee... But hata hivo sio rahisi kujudge maana ukute naye kaelewa maumivu ya moyo wa huyo mwanamke akijua fika vitu vya humo ndani sio vyake ni halali ya huyo dada. Tena WARNING; Huyo mwanaume anaonekana ni mshenzi ukute hata huyo mwanamke mpya sio mke bali ni mwanamke mpya ila kaja kujisafisha kwenu... (Labda kama kweli na hao watoto wameletwa hapo).

Tatizo la Hawara

Ok, ni kawaida kuwa mtu unaweza toka na mme wa mtu, BUT hivi kuna sababu yoyote ya kwenda mletea vituko mke wake na vujo tele hata kama ana hasira juu ya mahusiano yao kuvujika? Nashangaa... Hiyo confidence ya kulala humo ndani anaitoa wapi (mchawi??); kuwa unajua kuwa mke wake pia anajua wewe ndiye uliyekuwa mbadala na unarudi kulala humo ndani?

Kwa upande namuelewa... Kapoteza miaka mitatu kwa ajili ya huyo mwanaume. Wapo wote (ki mantiki kwa halali kabisa maana alitengana na wife); then kamfanyia visa na kumtoa humo ndani bila kitu chochote. Hasira zake ni halali ila tu nashangaa hiyo roho yake ya paka asiee... Duh!

Kwa mtazamo wangu naweza sema haya mambo magumu sana kuja na justification za hasa yupi anatakiwa lawama. Mwanaume ana makosa pia, ila hao wanawake nao sio watoto wadogo waangaliwe tu kuwa wao ndiyo wameonewa na hali wao ndio wamechangia kwa ukubwa hali kuwa ilivo. Kitu nakuhakikishia ni kuwa mwanaume angejua kuwa mke wake kichaa na hakubaliani na upuuzi usio kuwa na tija asinge thubutu, hata huyo hawara asinge thubutu...

Ila niongezee kuwa watu wa sampuli kama hiyo ya huyo mke hatari saana. Hulimbikiza mambo rohoni, siku aki react unakuta kama sio mume ama hawara ama wote maiti tu, na wala hajutii...
 
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Likes
94
Points
145
MwanajamiiOne

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 94 145
Kusema ukweli hata mimi nilishangaa sana wakati huyu jamaa aliponitamkia hivyo kuwa mkewe wa ndoa atakuja na kufikia hapo kwake baada ya hawara kuondoka, lakini nilishangaa zaidi huyo mkewe alipomwelleza mke wangu kuwa mumewe kampigia simu na kumjulisha kuwa hawara atakuja na kufikia hapo nyumbani...

Hivi sasa niko hapa nje nashuhudia mke wa ndoa akifanya usafi wa kutupa vyombo vliivyovunjwa na vioo vya makabati wakati hawara amekaa sebuleni anajichana kwa breakfasti na mpishi ni mke wa ndoa!

Sijui le litazama salama hapa nyumbani maana huu ukimya wa huyu mke wa ndoa mie unaniogopesha kabisa
Huyo Mama wa ndoa nae inawezekana hamnazo sasa anasafisha nyumba ya nini? Si aache mumewe aje ashuhudie?? na anajipikilisha ili iweje si ajabu ndio maana hawara anamchezea ngoma kichwani. Upole mwingine mzigo
 
N

Neylu

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
2,675
Likes
52
Points
145
N

Neylu

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
2,675 52 145
Kwanza naomba niwatetee wanaume wa kanda ya Ziwa (akiwemo Baba yangu) kwamba hawako hivyo kabisaa..!

Huyo jirani yako ni utaahira alionao tuu yeye kama yeye..!! Mwanaume mwenye akili timamu hawezi kufanya hayo madudu ya kumleta hawara afikie kwa mkewe..!! Ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu.!!

Ashukuru Mungu kwamba ana mke mstaarabu..!!. Huyo Hawara angekutana na mimi hakuna rangi angeacha kuona..!!
 
lara 1

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Messages
15,569
Likes
11,698
Points
280
lara 1

lara 1

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2012
15,569 11,698 280
Mwashangaaaa Nini!!!!!!!!!!!? Kazi kungaa sharubu tu!!!!!!!!! Toka lini Fahari wawili wakakaa zizi moja!!!!! Ofcourse huyo bwana ana makosa sana kucheat na huyo Hawara.

Ila hawara pia ana HAKI ZAKE ZA MSINGI TU hapo! We utumike 3 F. Years afu uachwe kizembe zembe hivi hvivi eti kisa mwenzio anarudi!!!!!! Bull shit!!!!!!

Vunja bibi wewe vunja hapo kila kitu!!!!!!!!! Usibakishe hata kikombe!!!!!! Wanaume wana masihara sana na maisha ya wanawake!!!!!!!! Yaani ujisikie tu UNIFURUMUSHE!!!!!! Kirahisi rahisi tu!!!!!!! Mmmmmmmh!

Angekuwa mtu mwepesi mwepsei huyo hawara angeondoka kimya kimya maskini ya Mungu, with her broken heart, akaenda kufia mbele ya safari kimya kimya huku hili Fisadi la Mapenzi Limepoziiiii!!!!!!!!! Halina stress kabisaaa linajinafasi na mkewe!!!!!!! Thubutuuuuuu yao!!!! Vunja hadi mlango hapo shostito!!!!!!!!!!!
 
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Messages
268
Likes
2
Points
0
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2009
268 2 0
Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume... People treat you the way you want them to treat you... Hapo wakushangaliwa na hao wanawake pia. Ni mambo mengi wanaume wanatufanyia na kutuchezea ambavyo wasinge thubutu kama tusingeruhusu. Upole, ustaarabu, na husuda ina mpaka wake. Matatizo yapo kwa wote...

Tatizo la Mke

Kwa kukubali kudharauliwa hadi kiwango hicho. Mume kamtelekeza kwa miaka mitatu na kumtuma mkoani yeye pamoja na watoto wake. Kamrudisha hapo nyumbani huku mke akijua fika kuwa kuna hawara alikuwa akiishi hapo na mbaya zaidi ni kuwa huyo hawara karuhusiwa kufikia hapo akiwa en route kuelekea Arusha. Kakubali Mumewe amchezee... But hata hivo sio rahisi kujudge maana ukute naye kaelewa maumivu ya moyo wa huyo mwanamke akijua fika vitu vya humo ndani sio vyake ni halali ya huyo dada. Tena WARNING; Huyo mwanaume anaonekana ni mshenzi ukute hata huyo mwanamke mpya sio mke bali ni mwanamke mpya ila kaja kujisafisha kwenu... (Labda kama kweli na hao watoto wameletwa hapo).

Tatizo la Hawara

Ok, ni kawaida kuwa mtu unaweza toka na mme wa mtu, BUT hivi kuna sababu yoyote ya kwenda mletea vituko mke wake na vujo tele hata kama ana hasira juu ya mahusiano yao kuvujika? Nashangaa... Hiyo confidence ya kulala humo ndani anaitoa wapi (mchawi??); kuwa unajua kuwa mke wake pia anajua wewe ndiye uliyekuwa mbadala na unarudi kulala humo ndani?

Kwa upande namuelewa... Kapoteza miaka mitatu kwa ajili ya huyo mwanaume. Wapo wote (ki mantiki kwa halali kabisa maana alitengana na wife); then kamfanyia visa na kumtoa humo ndani bila kitu chochote. Hasira zake ni halali ila tu nashangaa hiyo roho yake ya paka asiee... Duh!

Kwa mtazamo wangu naweza sema haya mambo magumu sana kuja na justification za hasa yupi anatakiwa lawama. Mwanaume ana makosa pia, ila hao wanawake nao sio watoto wadogo waangaliwe tu kuwa wao ndiyo wameonewa na hali wao ndio wamechangia kwa ukubwa hali kuwa ilivo. Kitu nakuhakikishia ni kuwa mwanaume angejua kuwa mke wake kichaa na hakubaliani na upuuzi usio kuwa na tija asinge thubutu, hata huyo hawara asinge thubutu...

Ila niongezee kuwa watu wa sampuli kama hiyo ya huyo mke hatari saana. Hulimbikiza mambo rohoni, siku aki react unakuta kama sio mume ama hawara ama wote maiti tu, na wala hajutii...
Dada AshaDii watoto wapo mmoja miaka 12 na mwingine miaka saba, wote ni wa kiume na wanafanana sana na baba yao.
Hilo la ukimya hata mimi na mke wangu limetutisha sana, na jana wakati huyo mwanamke anavunja vyombo usiku huko ndani tulishika roho maana nilijua asubuhi tutajikuta Polisi kutoa ushahidi naana nilidhani watauana.

Kuhusu kumlaumu mwanaume, acha tu nimlaumu, hivi kweli mtu mmeachana naye kwa vurugu kubwa, halafu unamruhusu aje afikie kwako wakati ndani ya nyumba yupo mkeo wa ndoa na watoto, hapana hilo haliwezekani, huyu mwanaume ana dosari kubwa katika akili yake.

yaani ninachoshuhudia hapa ni vituko visivyo vya kawaida, lakini ukimya wa mke wa ndoa ndahani unasaidia maana nadhani dhamira ya hawara ni kutaka kulianzisha wachapane.

Ngoja nitakuwa nikiwadondoshea kinachojiri, mkiona kimya labda yametokea maafa na niko Polisi kutoa ushahidi
 
Last edited by a moderator:
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2009
Messages
268
Likes
2
Points
0
Tegelezeni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2009
268 2 0
Huyo Mama wa ndoa nae inawezekana hamnazo sasa anasafisha nyumba ya nini? Si aache mumewe aje ashuhudie?? na anajipikilisha ili iweje si ajabu ndio maana hawara anamchezea ngoma kichwani. Upole mwingine mzigo
Mwanangu, mwanaume yuko Rwanda ha haijulikani atarudi lini, sasa aache watoto wakatwe na vioo? Na kuhusu kupika kawapikia wanae, nadhani hawara kajipakulia si kipo jikoni
 
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
10,728
Likes
8,304
Points
280
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
10,728 8,304 280
mimi ningeita mwizi ili aje apewe adabu,yaelekea huyu mama alishaona mengi kupitia huyu mwanaume so hayo ni marudio tu ndo maana yupo kimya
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,678
Likes
3,559
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,678 3,559 280
Tegelezeni kwanza naliona tatizo katika mtazamo wa da ASHA dii lkn pia naliona tatizo katika mtazamo wa mwanaume kuwachoka wote so anataka wauane yeye akiwa safarini ili huko aendelee kula bata.

ngoja nikwambie kitu, mwanamke jasiri sikuzote huitete ndoa yake kwa gharama yyte ile na hata pale busara inapohitajika basi hutumia busara ile ambayo japo itamuumiza lkn bado itampa kuwa mshindi mwisho wa siku.

skiliza mkuu huyu mume ni wazi kwamba anamke mwoingine somewhere na sasa anataka kuwadelete hawa kwenye folder zao ili ale maisha na huyo mpya. sitoshangaa kama hawa wakipigana waumizane kisha waende segerea baba aendelee kula bata.

kwangu mm huyu hawara ni mshamba ingefaa waunge nguvu wamuadhibu huyu baba atakaporudi badala ya kuoigana wao ama kuvunja vyombo. mwanaume yyte yule akisha kutoa nyumban kwake na ukakubali kutoka never come back kila siku utakuwa victim wa manyanyaso ya upole, na upendo wake kwake. to me ili kuepuka hali kama hiyo inapotokea mama umefungasha na kuondoaka do it for good...........na utaona maisha yanaenda.
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,237,586
Members 475,561
Posts 29,294,023