Hivi huyu mtu ameruhusiwa na nani au uongozi umelala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huyu mtu ameruhusiwa na nani au uongozi umelala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kaburunye, Jul 20, 2010.

 1. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa wale watumiaji wa barabara ya old bagamoyo (ile njia ya kuja mjini kupitia kawe, mikocheni, msasani nk) mnaweza kuwa mmemwona yule jamaa aliyeamua kuishi kando ya barabara mbele kidogo ya lile daraja baada ya makao makuu ya JKT kama unakuja mjini. Cha ajabu huyu jamaa ambaye inaonekana kama vile akili yake haiko sawa anapika na kuishi eneo lile bila usumbufu wowote.

  Kila nikipita hiyo njia asubuhi huwa namwona jamaa amelala na wakati mwingine nakuta anapika huku akiwa na chupa ya bia pembeni na mdoni anavuta ama itakuwa sigara ya kusokota au bangi. Mara zote najiuliza huu bwana ana kibali cha kuishi hapo au inakuwaje anaachiwa tu kuendelea kuishi hapo??? Hii njia ndo anayopita waziri wa ulinzi (hussein mwinyi) kila siku na nina hakika naye atakuwa anamwona (labda kama ana matatizo ya macho). Swali... hili jambo limekaa vipi wadau, je ni sawa watu kujiamulia kuishi popote hata sehemu ambazo hazina makazi? Naomba vyombo vya dola viliangalie hili
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ywezekana jamaa yuko kazini. Si unajua tena mambo ya Jamhuri!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Mawazo ya miaka ilee....... mtu akivaa vibaya... nywele tifutifu.... mpweke mpweke... halafu awe tena anajua maneno mawili ya kiingereza...watu wanasema ni usalama wa taifa huyo....
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii staili ilkuwa enzi za mwalimu sidhani kama kuna mtu katika kipindi hiki anayeweza kuja kwa staili hiyo.
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mdharau mwiba mguu huota tende. Nani alikuambia kwamba mbinu za miaka ya 70 za kipelelezi zimeachwa? Soma habari za maspai wa Kirusi walivyokuwa wakitumia mbinu za kizamani kule USA kwa miaka kama 10 hivi mpaka wakaja gundulika. Kila mbinu inatumiwa kama yaweza kuleta mafanikio. Tena hizo za zamani sasa ndo zinatumiwa sana sasa kwani watu wengi hawazitajii tena kwamba leo hii zaweza kutumika kama mkuu unavyowaza pia.
   
 6. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa wale watu walichokuwa wanafanya kuna uzamani upi???
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kadiri ya makachero wa kimarekani, baadhi ya mbinu za kizamani (za miaka ya vita ya kwanza na ya pili ya dunia na cold war) ni (1) ile ya kutumia maandiko yasiyoonekana. Hii wanasema ni mbinu ya siku nyingi sana, yaani kwa lugha nyingine imepitwa na wakati. (2) Ni mbinu ya kutumia lugha ya kificho / ya mafumbo yenye code maalum. Hii waliitumia walipokuwa wakiwasiliana kwa redio. Mbinu hizi 2 wamarekani waliwashangaa sana warusi kwamba ni mbinu za kizamani. Na mtaalamu mstaafu wa KGB ya zamani walipomwuliza kuhusu mbinu hizi alijibu kifupi tu kwamba: katika mbinu za kipelelezi hakuna kupitwa na wakati. Zote za zamani na za kisasa lazima zitumike sambamba alimradi zizae matunda.
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Tu asume ni usalama wa taifa, asa ye anayafaidi vp maisha haya mafupi?
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamna cha usalama wala nini, yule jamaa ni kichaa na niwa mda mrefu pale, ingekuwa usalama wale askari wetu wanao vizia malori yanayo vunja sheria na kupita pale darajani na mzigo na chukua kitu kidogo mbele yake mbona hajawareport? tuache kuogopa kivule enzi za mwalimu hazipo
   
 10. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huyo yupo kazini kama yule aliyekuwa anakaa pale maeneo ya ocen road hospital unamkuta amejipaka udongo mwekundu usoni anaongea mwenyewe saa nyingine ukipita na gari hujapandisha kioo anakuomba shs 100 but ikifika saa4 anaingia ocean road anteen anakula msosi wake wa maana then anapotea ikifika saa 8 mchana anrudi tena barabarani. kwahiyo hizi mbinu bado zinatumika na mifano tunayo mingi tu tunaiona waziwazi. Kwasasa sijamuona tena pale ocena road nathani amemaliza kazi alio pangiwa amekwenda sehemu nyingine
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli yule jamaa yuko kazini basi kuna wakati inabidi mtu umshukuru Mungu sana kwa kazi ulioko nayo hata kama hailipi
   
 12. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mi suala langu ni kwa nini anaachiwa aishi pale? Je vyombo vya dola akiwemo waziri wa ulinzi (Husein) hili jambo kwao wanaona ni sawa tu? Leo asubuhi nilipopita nimekuta bado amelala. Amejifunika shuka lake (lililodariziwa maua maua - sijui kalitoa wapi). Walio na uzoefu kwenye nchi nyingine zilizo makini hebu tusaidieni kama kitu hii ni jambo la kawaida. Sidhani kama unaweza kwenda marekani ukaanza kuishi pembezoni mwa barabara (unapika na kulala hapohapo) na vyombo vya dola vikuachie tu!!!! Au tunasubiri msaada wa wafadhili ku-deal na ishu ndogo kama hizi. AU tunasubiri atolewe kwa hisani ya watu wa Marekani.
   
 13. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kabisa jamaa yuko kwenye UNDERCOVER hawa ndio wale makachero
  manake pale kuna hawa mapolisi wa pikipiki FFU wanategaga lakini nadhani wata
  kuwa wameshapewa maelekezo na wakuu wao wakazi juu ya operation zinafanyika
  maeneo yale
   
 14. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sasa unataka akalale wapi?
   
Loading...