hivi huyu DPP Feleshi ni mtu wa namna gani?anafanya kazi kwa maslahi ya nani TZ?..hatumwamini.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hivi huyu DPP Feleshi ni mtu wa namna gani?anafanya kazi kwa maslahi ya nani TZ?..hatumwamini....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, May 25, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Katika jambo ambalo limekuwa linakatisha tamaa juhudi za kupambana na wezi wa mali za umma TZ (mafisadi)ni utendaji wenye utata mkubwa wa ofisi ya DPP na boss wao Feleshi.....Kuna rejea nyingi zenye kuonyesha utata wa hali ya juu jinsi ofisi hii ya DPP inavyofanya kazi na ilivyoshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa chungu mzima wa wizi wa mali za umma.....mifano ni mingi...ukianza na wezi wa EPA..wachache walifunguliwa kesi za kimagumashi lakini wengi wako mtaani wakitafuna nchi....watuhumiwa wa rada..kina Chenge....wako mtaani wakila nchi...watuhumiwa wa kashfa za kagoda..deep green..etc etc....watuhumiwa waliothibitishwa na kamati za bunge kwenye kashfa za richmond....kashfa ya Jairo na wenzake woote....na hivi majuzi watuhumiwa waliopatikana na ripoti chafu za CAG...ambao wanachunguzwa na TAKUKURU lakini kwa experience zilizopita hatuna uhakika watafikishwa mahakamani....

  My take:
  • TAKUKURU mara nyingi wamekuwa wanamaliza kazi zao na kupeleka majalada kwa DPP lakini kesi zinayeyuka...mara nyingi tumemsikia Dr.Hosea akithibitisha kupeleka majalada kwa DPP ili mafisadi wapelekwe mahakamani lakini mambo yanayeyuka na watanzania wanasahaulishwa....kama vile hakukuwa na matatizo na muda unakwenda na watu wanazidi ku enjoy freedom na hata kuficha ushahidi......
  • Kuna kipindi boss wa TAKUKURU Hosea aliuthibitishia umma wa TZ kuwa kuna kesi kadhaa zilizokuwa tayari zimechunguzwa na alisema amezipeleka kwa DPP ili mambo yapelekwe mahakamani lakini miaka imeshaenda sasa na watanzania wamesahu......huyu DPP ni nani????na anafanya kazi TZ kwa manufaa ya nani???
  • Kwanini baadhi ya mambo, mengine madogo madogo ndo tunaona eti DPP akijifaragua kufungua majalada???....refer DPP alipofungua jalada la mh.Sitta pale aliposema Dr.Mwakyembe kalishwa sumu....au kesi za kimagumashi za kina Mramba...Maranda na Liumba kuongea na simu jela...Mbona hatuoni wezi wengi wakubwa walioliibia taifa hili na viongozi wakifikishwa mahakamani?????????.....Hatumwamini huyu jamaa DPP...............
   
 2. M

  Masabaja Senior Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siku nyingi ahaminiki mbona hao wana mambo yao ni kulinda UFISADI, kwani kazi ya TAKUKKURU ni nini?
   
 3. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni mtu aliyepewa mamlaka ili kulinda na kusafisha wana Ccm pale wanapofanya makosa.
   
 4. N

  Ngahekapahi JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Jibu rahisi ni kwamba na yeye anahusika maana kama kesi haziendi maana yake nini?
   
Loading...