Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hawa wanawake wengine ni shida, ya ndani analeta hapa mtandaoni kweli dah. somenihapo chini (instagram)

View attachment 688048

  • joycekiriasuperwoman
    Kilewo baba Watoto wangu, yaliyotokea ilibidi yatokee ili kila Mmoja aanze upya safari ya Maisha Yake. Wakati tunaanza huu mwaka nilikuambia huenda mwaka huu tukaachana! Unakumbuka? Well, Lakini jambo moja nakusisitiza hapa, Nimekuomba sana uniachie biashara zangu nisimamie, ili na wewe usinamie biashara zako kutokana na Changamoto zetu hasa za kiuchumi. Wewe Pesa zako unazopata kwenye biashara zako hutaki kushea, Ila Pesa zinazotoka kwenye biashara zangu unataka tushee. Najua ni ujinga wangu wa kukupenda sana ndo umeniponza. Labda ningetenganisha Mapenzi na biashara tusingeishia huku.

    Wakati mimi nasajili Kampuni Yangu nilikuweka kwenye kampuni bila shida yoyote na wakati nafungua akaunti za bank nilikuweka pia. umekuwa ukijua kila ela inayoingia pamoja na matumizi yote kwa sababu lazima tusaini Wote na ndiyo Raha ya Mapenzi.

    Wewe ulipofungua Kampuni yako uliweka pia jina langu kitu ambacho nilipenda sana, lakini ulipokwenda kufungua akaunti ya bank HUKUNIWEKA. Kiukweli SIKUPENDA, mbaya zaidi ukataka kuwa unasaini Pesa zako kivyako.

    Japo nilianza kuona mashaka Lakini nilijipa Moyo, labda ukipata utanishirikisha pia kama Mimi nilivyoamua kukushirikisha kila kitu changu. PESA MWANAHARAMU buana, pale tuu ulipoanza kazi na kampuni yako Ndipo SHIIIDA ilipoanzia, hukutaka kushea hata senti Nyumbani wakati biashara zangu kwa Kipindi chote cha Miaka NANE zimeendesha familia yetu bila tatizo.
    Kuna Miradi mbalimbali ambayo ulikuwa ukionyesha NIA ya kuifanya lakini yote ilifeli. Hivyo haikuwa rahisi KUKUJUA kwa upande wa KIUCHUMI sura yako ikoje... Ulijaribu biashara hizo kwa mtaji wa Familia bila kuona matokeo chanya, Pesa zikawa hazirudi lakini tukajipa Moyo biashara ndivyo zilivyo. Mwisho nikakushauri mtaji wa biashara tukope Bank labda utakuwa na nidhamu zaidi ya Pesa ya Mkopo kuliko kutoa ela Nyumbani. Hukupenda huo Ushauri, ukaona nakubania.

    Sasa MWAKA huu 2018 tuliongea mengi pale Bahari beach, juu ya mahusiano Yetu na Changamoto zake! Pamoja na yote tuliyoongea nikakuomba kila mtu asimamie biashara zake, kisha tukubaliane kwenye MAJUKUMU ya Familia kwamba nani atafanya Kipi. Lakini pia nikakuambia kwamba Niko radhi kuendelea kutimiza hayo majukumu. [HASHTAG]#SIR[/HASHTAG]
Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona unaficha PESA zako. Ile Siku niliyokubamba unatoa Ela kwenye akauti yako kwa Siri na hapo tulikuwa hatuna ela kabisa NILIUMIA kuliko hata ningekufumania. Yaani nilikuona huna NIA na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI. Najua Kazi ulizofanya hata kama NI Ndogo hukukosa hata mkate au sukari ya kuleta Nyumbani. Lakini ukaamua kula bata, hutoki na Mimi, Mara nyingi ukiwa na ela unatoka peke yako unarudi mpaka asubuhi... ukijua kuna punda wako hapa nyumbani atafanya kila kitu.

Kilewo najua Haya siyo mageni kwako, tumeyaongea kwa muda mrefu sana. Tumewashirikisha watu wa karibu. Pamoja na hayo yote Kilichonishangaza sasa ni wewe kukataa kuniachia biashara zangu wakati wewe una za kwako. Tena unasaini akaunti yako peke yako halafu akaunti Yangu nimekuweka tunasaini Wote.

Kilewo kwa staili hiyo ya maisha nilianza kukosa Furaha sana na wewe kwa kuona unanitumia wala huna NIA Njema na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI, huku Ndani MAPENZI YAKAPOTEA KABISA. Mpaka juzi birthday yako sikuwa najiskia kukuwish. Lakini kwa ajili ya Watoto nikajilazimisha. Ngoja niishie hapa.

KILEWO baba Watoto wangu, Dunia inajua NINAVYOKUPENDA. Tatizo langu kubwa na wewe unajua fika siyo wewe kutokuwa na Pesa, BALI KUTUSHIRIKISHA KWA KIDOGO UNACHOPATA wewe kama BABA wa Familia. kwa Sasa nina tatizo kubwa na wewe la kunipiga baada ya kuamua 2018 nitakuwa natoka peke yangu kujipa raha. Unajua sehemu ninazokuwaga nikiwa nimetoka na ndo sababu ulikuja ukanikuta, lakini uliamua kunipiga. Kesi ipo Dawati.

Kilewo ningekuwa na NIA mbaya nisingekuweka kwenye biashara Yangu, nimenunua Viwanja Goba na Bagamoyo, bila uwepo wako, lakini nilikuja kukushirikisha na wewe ukaenda kuongeza majina yako. Sikuwahi kulalamika maana NAKUPENDA na wewe ndo Baba Watoto wangu. Nimetamani kuzaa mtoto wa Tatu lakini kwa ambushi zako nimeogopa. Mambo ya KOMAA KAMANDA hapana. Nikasema Wawili wanatosha.

Kilewo wangu nakuomba tena na tena uniachie biashara zangu niweze kuendelea kutunza hawa Watoto wetu. Toka unipige umeondoka siwezi kutoa ela, hatuna Chakula nyumbani, Madeni ya wafanyakazi, Nyumba nadaiwa n.k
[HASHTAG]#SIRIZANDANI[/HASHTAG]
Mwanamke awe Mtii kwa Mme na Mme awe na Akili
 
Umeelewa alikuwa analalamikia kitu gani Joy....? Anasema ni signatory kwenye kampuni so awezi toa pesa bila sign ya mmewe ...hata kama mke kakosea basi mme at least afanye kwa ajili ya watoto.... Na ulishawahi sikia wapi mme anakimbia nyumba yake yenye watoto na kumwachia mke, ujue alikuwa analelewa sanaa na huyo mwanamke.... Mara nyingi mke ndio anaondoka matatizo yakizidi, japo sijafurahishwa na Joy hili swala kulileta mitandaoni kama hawana wazazi au ndugu na jamaa....umejishushia usuperwomen
ce d


Hoyce Temu kamfunda Joyce kimtindo kila mtu anamwonea huruma... Hakuna mwanaume anayetaka kero. yaelekea huyo alishakuwa keroo sana kwa mmewe.

Mnakumbuka kuna kipindi alidhubutu kusema Kamanda Mbowe sijui nini... mke wa Mbowe alimfuata akamwambia your too young stay away with my family... aliufyata haswa... jinga la mwisho hilo. anadhani ndoa ni matangazo kanikera sana
 
ce d


Hoyce Temu kamfunda Joyce kimtindo kila mtu anamwonea huruma... Hakuna mwanaume anayetaka kero. yaelekea huyo alishakuwa keroo sana kwa mmewe.

Mnakumbuka kuna kipindi alidhubutu kusema Kamanda Mbowe sijui nini... mke wa Mbowe alimfuata akamwambia your too young stay away with my family... aliufyata haswa... jinga la mwisho hilo. anadhani ndoa ni matangazo kanikera sana
Mimi nseme tu kwamba mambo ya ndoa tusichekane kabisa lolote laweza tokea hata kama. Yy ni super woman ndo akomae tu kisabuni mpaka afe bora kuweka hadharani asaidiwe
 
hakuna kitu huwa nafurahi nikikuta jibwa jike lililokuwa linang'ata wenzie limekamatwa kwenye mtego, linapigwa kipigo cha mwizi, halina pa kwenda, linalialia tu. ni burudani. feminists wameharibu ndoa za watu wengi sana hapa tz, na ni halali yao wapigwe tu.
 
Wahaya wanawezana wenyewe kwa wenyewe maana kwa ngono hawajambo.Hata akiwa profesa tabia zake kwenye hio sekta hua ni zile zile kama za ambae hajasoma.

Endeleeni kuoana tu nyie kwa nyie mkuu.
Hahahah
 
Umesikiliza upande wa pili weka mizani ndipo utoe hukumu pengine kaamua tu kumzalilisha mwenza kisa kahama nymbn huyu mwanamke sio wa kuolewa hawezi kutunza siri za nymba anatisha kuliko ukoma huyu
Hii move ni kali sana sjui stelling atauwa ama vp
 
MKATOE HELA WAKATI HAKUNA! MLIANZA MITANDAONI NA NI LAZIMA MMALIZE MITANDAONI.Superwoman KIRIA.Bado IYOBO na ANTY wake
Hao nao kimeshabumburuka mbona hujaskia yale ya shirawadu kugongwa na gari ya ant na iyobo
 
Mimi kama nimemuelewa tofauti Joyce anisamehe. Lakini akili yangu inanituma kuamini kuwa baada ya Joyce kuanika sakata hili kwenye media na shutuma alizopata toka kwa wachangiaji, sasa ameamua kuja na episode 2 ili watu wajue chanzo cha ugomvi wao ni ubahili/ubinafsi Wa mumewe na hii anadhani itamsaidia ku atract public sympathy. Lakini ukisoma vizuri maelezo yake unamwonea huruma kwa sababu between lines ameficha tabia yake na anachotaka kiuhalisia toka kwa mumewe. Lakini pia angalau ameeleza chanzo cha kupigwa kwake kuwa ni yeye kwenda "kujirusha" peke yake kama anavyofanya mumewe ili ngoma iwe droo, na anataka jamii ione kuwa kipigo toka kwa mumewe hakikuwa sahihi kwa vile alimkuta sehemu anayoifahamu na hakuwa akifanya zinaa kama yalivyokuwa mawazo ya mumewe. Tatizo la pili la Joyce ni kutofanywa Second signatory kwenye akaunti za mumewe wakati yeye amemfanya signatory kwenye akaunti zake. Katika hili Hoja ya Joy ni ya msingi lakini siyo nzito. Anakiri wakati hili linafanyika hakuona tatizo kwa sababu alikuwa na mapenzi thabiti kwa mumewe. Kwa maana nyingine kinachomfanya ahoji sasa hivi ni kupungua kwa hayo mapenzi thabiti ya awali. Sasa ni kipi kimeyapunguza hayo mapenzi? Ni pale Kilewo alipoacha kumjali na kumthamini, yaani kutoka out peke yake bila mkewe.
Je, haya ni ya kuanika hadharani hata kama kweli yapo? Jibu rahisi ni no, tena big NO! Kinachofanya ayaanike haya kwa sasa ni dhamira yake anayosema alimwambia mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu, hajataja ni lini, kuwa "MWAKA HUU 2018 NI MWAKA WA KUACHANA".
Huwezi kudumu katika mahusiano kama akili yako umeshaiset kuachana. Ukilala unaota kuachana, ukiamka unawaza kuachana. Siku zote mawazo yanaumba dhamira na mwisho wa siku "UTEKELEZAJI". Joyce unatekekeza ulichokiwaza siku nyingi na sababu ulizotoa ni catalyst. Yaani ulitegesha kama wimbo mmoja Wa Mrisho Mpoto anaposema; "UKINIKANYAGA TU.....!"
Lakini Joy hujachelewa, la kwanza nakusihi acha kutumia njia hii ya kishamba kumdhalilisha mwanaume unayemuita baba Wa watoto wako, na sehemu nyingine umemuita "KILEWO WANGU". Tafuta wenye busara wakusaidie ama KUACHIKA kwa amani au KUREJESHA ndoa yako katika line.
Wasalaam;
Bila bin Bila!!
Hongera sana ndugu kwa fact za maana nmesoma michangk ming ya memba humu cjaona aliekufikia naishia hapa kusoma maoni ya watu najua sintakutana na maoni mazuri zaidi ya haya big up bro.
 
Hahhahaa mkuu we nouma sana nimecheka sana daa,ila kweli huyu dada ana shida ya kimaadilii hasa kwenye eneo la mke na mume,hujafundishwa hekima ya kuishi kwenye agano hasa zinapo tokea changomoto kama hii ya sasa aliyo nayo
 
Ume andika vizuri mkuu kama ata soma hapa nadhani itamsaidia kama ana shaurika,hongera sana kwa andiko lako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom