Hivi huyu anayejiita Nabii Mashimo, akili zake ziko sawa?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Mwezi mmoja uliopita nilimsikia akisema ana dawa ya corona. Na akaenda mbali zaidi akatoa wito kwa serikali impeleke China ili akatibu watu huko. Sijui aliishia wapi kwani sasa hata hapa Tanzania wagonjwa wamepatikana.

Jambo la ajabu sasa, ni leo katika kipindi cha Jahazi, nikiwa napita zangu mahali fulani, nimemsikia akikanusha kuwa hana dawa ya corona. Na kwamba watu wanajitoa akili na kumpigia simu kumuomba awape dawa ya corona.

Sasa nauliza, huyu mtu ana akili timamu kweli au ameamua kudhihaki hiyo kada ya kiroho kwa kujiita nabii? Najua anao wafuasi, hivi wanajisikiaje kuwa na mtumishi kama huyu?

Kwanini inakuwa rahisi namna hii kumdhihaki Mungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom