Hivi huwa unajiuliza maswali kama haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huwa unajiuliza maswali kama haya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sirgeorge, Mar 26, 2011.

 1. s

  sirgeorge Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF!
  Huwa najiuliza maswali mengi sana kichwani na huwa sipati picha halisi, na je kama kweli hali ingekuwa ni hivyo ingekuwaje?
  MOSI: Kama Mwenyezi Mungu angeamua mioyo yetu iwe inaonekana kwa nje kama vilivyo viungo vingine kama vile ( sikio, pua, mkono etc). Na kama pia ingewezekana kwa kila jambo unalolifanya au kulifikiria kulifanya, jambo hilo linaandikwa kwenye moyo/mioyo yetu (iliyo nje). Hivi kungekuwa na fisadi yeyote Tanzania? Au adui yako angeweza kusimama mbele yako?
  Kwa mafisadi: Kwa deal lolote lile atakalofanya au kulifikiria kulifanya (au hata kuonyesha dhamira tu), deal hilo lingeonekana kwenye moyo wake (ulio nje) tena na kiasi halisi kingeandikwa , je wa Tanzania wangekuwa wanawaacha tu wafanikishe hayo madeal yao?
  Mikataba Feki: Je, mawaziri wetu wanaoenda kusaini hiyo mikataba, na ten percent yao ingekuwa isomekana kwenye mioyo yao kabisa , je. Tungewaacha wawe wanaenda kusaini hiyo mikataba na ingali tukijua issue nzima? Je, ni nani angekuwa ana sain mikataba hiyo? Na je , unadhan na tume za kuchunguza mikataba mibovu zingekuwepo?
  Fikiria pia na matukio mengine ya namna hiyo. Kisha ujiulize Tanzania yetu ingekuwaje?
  Adui yako:Yeye huyu ingesomeka kabisa kwenye moyo wake kuwa anakuchukia. Maana adui yako anaweza kuja anakuchekea chekea na kukupiga mzinga (kuomba hela), ukidhani ni mtu mzuri kumbe si hivyo. Kama hali ndo ingekuwa hivyo (mioyo kuwa nje) sidhan mtu kama huyu angesimama mbele yako.
  PILI:Kama matumbo yetu yangekuwa ni ya vioo, hiyo ingewezekana kabisa kuona kila mtu alichokula. Je , ni watanzania wangapi matumbo yao yangekuwa yamewekewa tinted au mapazia meusi?kwa kuhofia kilichomo tumboni kutokana na mlo mmoja kutokana na hali ngumu ya maisha? Je, viongozi wetu wangekuwa wanahitaji kufanya research kujua hali ya maisha/uchumi ya/wa mtanzania mmoja mmoja?

  Endeleza list kwa kitu unachofikiria……………………

  Have a lovely weekend !
   
 2. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  watu wote wafuate amri zake Mungu. Kwanini tunatofautiana?
   
Loading...